Kamanda Ronald Mapunda

Kamanda Ronald Mapunda

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nilikuwa naangalia video hii (ina ubora wa chini sana) lakini ujumbe unafika.

Video inaonyesha matukio yaliyotokea siku ya kukaribisha askari wa Tanzania waliokuwa wakirudi kutoka vitani Uganda na matukio ya sherehe za siku ya mashujaa mwaka 1980 pale uwanja wa taifa wa zamani. Ndege moja ya kichina-Shenyang ilianguka pale pembeni mwa Chuo cha Chang'ombe na kumwua rubani wake ambaye alijitahidi kuhakikisha ndege haiangukii kwenye jukwaa kuu alipokuwa Nyerere. Kwenye dakika ya 1:17, kuna brigedia anatambulishwa kama Brigedia Ronald Mapunda. Kwa nini Kamanda huyu hajulikani sana katika historia zetu? Hata mimi niliyekuwa mfuatiliaji sana wa mambo ya kijeshi, sikuwa namfahamu. Je kuna mtu wa kuweza kutusaidia kumfahamu kamanda huyu na kuweza kurudisha jina lake katika kumbukumbu zetu kitaifa kwa mchango wake?
 
Labda nikusahihishe haitwi Ronald mapunda anaitwa Ronald makunda ni mkazi wa mtwara alishafariki watoto wake wakike ni walimu pia alikuwa mwenyekiti bodi ya korosho na mbunge wa temu moja WA masasi no mpole na hakuwa fisadi
 
Hiyo video haionekani kafanyaje na anahusika vp na hiyo ndege iliyoanguka
 
Jina la kimapigano aliitwa kamanda torpedo
Asente sana; hilo jina la Torpedo nalikumbuka ila sielewi kwa nini sikuweza kuchukua jitihanda za kumfahamu yeye binafsi. Wakati huo tulizama kwa hao makamanda sita wa kwanza na hivyo yeye kusahauliwa. hao wengine wopte walijulikana sana nchini kote.
 
Labda nikusahihishe haitwi Ronald mapunda anaitwa Ronald makunda ni mkazi wa mtwara alishafariki watoto wake wakike ni walimu pia alikuwa mwenyekiti bodi ya korosho na mbunge wa temu moja WA masasi no mpole na hakuwa fisadi
Asante kwa masahihisho; ni jambo la ajabu kuwa wengi hatukumfahamu kijeshi ingawa aliongoza brigade nzima wakati wa ukombozi wa nchi dhidi ya uvamizi wa Uganda. Kumbe jina lake halisi ni Rowland Makunda; alifariki mwaka 2014
 
Back
Top Bottom