Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,265
- 4,735
Hapana, hakuwa kadaalikua kada wa chama huyu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana, hakuwa kadaalikua kada wa chama huyu?
A non biased comment, well-done mkuuOkay sisi hatuna la kusema mbele ya kazi za Mungu. Yeye anaona ya nuruni na ya gizani. Kamanda alale mahali pema peponi Amina.
Inapendeza Marehemu asemwe vizuri. Lakini Kamanda huyu alijishushia heshima yake mwenyewe wakati wa uhai wake. Inatupa shida Sana kumpa heshima sasa Kwa vile Tu ni Marehemu. Mwenyezi Mungu amsamehe.Amefanya nini zaidi ya kuwa polisi kada wa chama cha mapinduzi? Na yeye kupitia nafasi yake amekuwa akiunyanyasa upinzani. Ametumika vibaya kisiasa,pia amesababisha niichukie kada yote ya polisi. Naombeni mnisamehe kama nimewakwanza.
R.I.P kamanda kada w CCM
Haaaaaa jamani, si kwa mzunguko huo sijui wanataka nini kwanini asikae pamoja au ndiyo kutaka kujulikana kuwa wote wana umuhimu na marehemu walimsaidia mpaka hapo! Familia zetu jamani shida sana.Marehemu asije amka tu na kulalamikia route ndefu
SiyoooooNdio
Labda alikuwa hawatembelei akiwa haiHaaaaaa jamani, si kwa mzunguko huo sijui wanataka nini kwanini asikae pamoja au ndiyo kutaka kujulikana kuwa wote wana umuhimu na marehemu walimsaidia mpaka hapo! Familia zetu jamani shida sana.
Sijutii kutompa heshima kama marehemu. God forbidInapendeza Marehemu asemwe vizuri. Lakini Kamanda huyu alijishushia heshima yake mwenyewe wakati wa uhai wake. Inatupa shida Sana kumpa heshima sasa Kwa vile Tu ni Marehemu. Mwenyezi Mungu amsamehe.
Ni huzuni & majonzi
Ameumaliza mwendo
Kazi ya Mungu Haina makosa
Mshiriki, Mzee wa Kanisa na Muinjilisti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mjini Kati Arusha
Alishiriki vema akitoa Zaka na Sadaka
Aliishi vizuri sana na washiriki Wenzake
Alikuwa Mnyenyekevu na mwenye hofu ya Mungu
Aliongoza kwa mafanilio makubwa harambe ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mjini Kati Arusha
RIP Kamanda Shana
=====
TANZIA: KAMANDA JONATHAN SHANA AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu
Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu
Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemoRPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Simiyu.
ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi
Updates: RATIBA YA USAFIRISHAJI WA MWILI NA MAZISHI
Taarifa.
Mwili utachukuliwa Muhimbili Mortuary siku ya Alhamis 17 September 2020 na kupelekwa kilwa Road kwa ajili ya kuagwa.
Baada ya utapekekwa kwa Dr. Musika Mbweni na kulala uko.
Siku ya Ijumaa wataanza safari kuelekea Ikizu Bunda watafika Dodoma majira ya Mchana saa Saba na utafikia nyumbani kwake watakaa kwa Nusu saa yaani saa 7:30 Mchana wataondoka nyumbani kwake Dodoma Ipagala kuelekea Kanisani Dodoma Kati watafika saa 8:00 Mchana. Kanisani kutakuwa na Chakula kwa Wageni na waombolezaji ; itafanyika Ibada fupi; Salamu za Kijeshi na kuaga mwili watu Wote.
Saa Kumi na Moja Jioni wataanza safari kutoka Dodoma Baada ya mapumziko kwenda Kijijini Ikizu mission . Wanatarajia kufika Bunda Asubuhi na watashinda Kwa Mama yake pale CCM Bunda Mjini na Jioni siku hiyo ya Jumamosi wataondoka na kwenda Ikizu Mission kwa Mzee Samwel Musika Waryoba Kaka yake na Marehemu Baba yake aliye mlea Shana.
Asubuhi Jumapili mwili utaondoka kwa Mzee Samwel kwenda kwa Kaka yake Shana Bukama Ikizu Mission ( Ikizu Secondary).
MAZISHI YA MPENDWA WETU SHANA NI JUMAPILI
Pia soma >>> RPC Shana anavyotikisha Arusha, awadaka Majangili hatari, AK 45, Meno ya Tembo
Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa