Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro azindua kampeni ya "Ongea na kamanda

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro azindua kampeni ya "Ongea na kamanda

Joined
Jul 27, 2024
Posts
35
Reaction score
13
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Afande SACP Simon Maigwa, Tar 20/10/2026 amezindua rasmi Kampeni ya "ONGEA NA KAMANDA".

Kampeni hii inalenga kuwapa fursa wananchi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwasiliana moja kwa moja na Kamanda. Kupitia kampeni hii, wananchi watapata nafasi ya kueleza changamoto zao, kuwasilisha kero mbalimbali, kutoa tuhuma za vitendo vya unyanyasaji wa aina zote, pamoja na kutoa maoni na ushauri juu ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulio hudhuriwa na Viongozi wa Bajaj na bodaboda mkoa,Wilaya na zone zote za Moshi mjini, Afande Maigwa amewataka Viongozi wa Bajaj na Bodaboda kuwa mabalozi wazuri wa amani.. Amewasisitiza kutumia barabara kwa kufuata kikamilifu Sheria za Usalama Barabarani ili kupunguza ajali zisizo na tija zinazopoteza maisha na mali...

Aidha, Kamanda Maigwa amewaomba viongozi hao kufikisha ujumbe kwa maafisa usafirishaji wote walioshiriki uzinduzi huo kuhusu mambo yafuatayo:

Kukemea vitendo vya ukatili, kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, pamoja na kutoa taarifa za wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya ili Jeshi la Polisi liweze kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria..

Kamanda amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi si adui wa mwananchi, bali ni chombo cha ulinzi wa raia na mali zao. Amesema Jeshi la Polisi ni rafiki wa wote wanaofuata na kuheshimu Sheria za nchi.

Vilevile, amewataka viongozi hao kuhamasisha maafisa usafirishaji kutumia barabara kwa usalama, kujiepusha na matendo ya kihalifu na viashiria vyote vya uhalifu, na kujiepusha kabisa na kubeba dawa za kulevya au wahalifu wa aina yoyote. Iwapo dereva atabeba abiria anayemtilia mashaka, ameelekezwa kutoa taarifa haraka katika kituo cha polisi kilicho karibu au kama inawezekana, kumpeleka moja kwa moja kituo cha polisi.

ONGEA NA KAMANDA KUTATUA CHANGAMOTO NA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA MKOA WETU NA NCHI KWA UJUMLA.


ONGEA NA KAMANDA KWA NAMBA +255715009923


Imetolewa na mwandishi Bora
 

Attachments

  • IMG-20261026-WA0007.jpg
    IMG-20261026-WA0007.jpg
    195.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom