Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga Desemba 25, 2024 alipotembelea Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha "Hope Group" kilichopo chini ya Kanisa la Uinjilisti (Evangelistic Church of Tanzania) Mbalizi Mbeya akiwa ameongozana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Veronica Ponera.
Kamanda Kuzaga amewataka watoto wa kituo hicho kuepuka kujihusisha na uhalifu, kuwa watoto wema na kutimiza wajibu wao wawapo nyumbani kwa walezi wao ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.
Naye, Mfadhili wa kituo hicho Bi.Susanna Joos amesema kuwa kituo hicho kina jumla ya watoto 136 huku jukumu kubwa la kituo ni kupokea watoto wasiojiweza na kuhakikisha wanakwenda Shule ikiwemo vyuo vikuu.
Bi.Joos ameongeza kuwa kituo hicho ni cha kutwa (Day Care) kikitoa malezi kwa watoto wenye mahitaji maalum, wapo waliofiwa na wazazi, wapo wanaotoka kwenye familia zisizojiweza hivyo wanahitaji kupata mahitaji mbalimbali kama chakula, malezi na mahitaji mengine ya Shuleni.
Kwa upande wake Mratibu na Mlezi wa Kituo cha "Hope Group" ndugu Mussa Sinienga amesema kuwa ni faraja kubwa kwa Watoto wa kituo chao kutembelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga hasa katika siku kubwa hii ya sherehe ya Krismasi.
Kamanda Kuzaga mbali ya kujumuika katika chakula cha pamoja na watoto hao na kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia, pia alipata nafasi ya kuwakabidhi zawadi ikiwemo nafaka (mchele) na mahitaji mengine kwa ajili ya kuwawezesha kwenda kusherehekea na ndugu zao nje ya kituo hicho.