Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahamoud Banga, ameendelea kukutana na makundi ya vijana kuhamasisha utulivu na kuwataka waripoti wote wanaofanya uchochezi pamoja na wageni wanaoingia nchini kinyume cha sheria
Aidha, amewaeleza vijana hao kuwa kile kilichotokea Oktoba 29 hakikumfurahisha mtu yeyote, na kwamba bado kuna uhamasishaji unaoendelea mitandaoni; hivyo amewasihi waendelee kudumisha utulivu.