A
Anonymous
Guest
Kamari imekuwa janga kubwa, hasa kwa vijana na watu wengi kwa ujumla. Imeua ndoto nyingi na kusababisha watu kupoteza mali, kazi na hata maisha.
Zaidi, michezo ya kubashiri mtandaoni kama casino, Aviator, JetX na mingine imekuwa changamoto kubwa kutokana na urahisi wa kuifikia.
Hakuna dalili kubwa ya Serikali kuingilia kati suala hili. Ni kweli Serikali inakusanya kodi kutoka kwa kampuni za betting, lakini kodi hiyo inakuja sambamba na madhara makubwa kwa wananchi.
Baadhi wamepoteza mali zao, wengine wamepoteza kazi, huku wengine wakikumbwa na matatizo ya afya ya akili na madeni yasiyoisha kutokana na uraibu wa kamari.
Familia zimeathirika, nyingine zimeteketea na ndoa zimevunjika kutokana na kushindwa kuhudumia familia kwa sababu ya uraibu wa kamari.
Soma Pia: Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center
Hivyo, pamoja na Serikali kupata mapato kupitia kodi, ni muhimu pia kuangalia gharama kubwa za kijamii na kiuchumi zinazotokana na kamari, hasa kwa vijana.