KERO Kamari imekuwa janga kubwa, Vijana tuungane kutokomeza janga hili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kamari imekuwa janga kubwa, hasa kwa vijana na watu wengi kwa ujumla. Imeua ndoto nyingi na kusababisha watu kupoteza mali, kazi na hata maisha.

Zaidi, michezo ya kubashiri mtandaoni kama casino, Aviator, JetX na mingine imekuwa changamoto kubwa kutokana na urahisi wa kuifikia.

Hakuna dalili kubwa ya Serikali kuingilia kati suala hili. Ni kweli Serikali inakusanya kodi kutoka kwa kampuni za betting, lakini kodi hiyo inakuja sambamba na madhara makubwa kwa wananchi.

Baadhi wamepoteza mali zao, wengine wamepoteza kazi, huku wengine wakikumbwa na matatizo ya afya ya akili na madeni yasiyoisha kutokana na uraibu wa kamari.

Familia zimeathirika, nyingine zimeteketea na ndoa zimevunjika kutokana na kushindwa kuhudumia familia kwa sababu ya uraibu wa kamari.

Soma Pia: Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center


Hivyo, pamoja na Serikali kupata mapato kupitia kodi, ni muhimu pia kuangalia gharama kubwa za kijamii na kiuchumi zinazotokana na kamari, hasa kwa vijana.
 
Mimi nipo hapa nasubiri pesa zangu 😁
 

Attachments

  • Screenshot_20260829-201644_SportyBet.jpg
    143.4 KB · Views: 15
Kabla kuondoa kamari inatakiwa kuondolewa sisiemu...je unajua wamiliki wa kamali wapo bungeni,wapo wizara nyeti asa michezo,unajua kama wamiliki wa kamari wanadhamini hadi.....?
 
Hoja ya maana kama hii haikubaliki na hao mboga mboga.

BTW, who are you....!?
 
🤣 Kamari si mchezo tena, wengine wameweka “bet” hadi kwenye hela ya vocha! Aviator ikipaa, na ndoto zao zinapaa nayo—tatizo ikidondoka, wanadondoka wote! 😂🎰
 
Kamari kamari narudia tena inamaliza vijana kwa wazee,watu wapo na changamoto ya afya ya akili, madeni,ndoa zinayumba tusaidiane wanajamii kupunguza madhara yake
 
Wako kwenye uwekezaji😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…