Kamari zimeshanila pesa vya kutosha... sasa naona cha mwisho kiwe Forex

Kamari zimeshanila pesa vya kutosha... sasa naona cha mwisho kiwe Forex

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298

​

Wakuu, Mimi ni mmoja wa wale watu ambao hawawezi kuja hapa kujifanya ni mkali wa kamari.kiukweli kamari imeshanila hela ya kutosha. nadhani wakamaria wote tunajua huu mchezo wetu mfano mdogo juzi niliwapa england kushinda nikaweka laki 9 na nusu nikala million 2.5 sasa jana argentina akanipiga makofi ya kutosha yaani game nimeomba kwa bet bulder argentia score 0.5+ pia itoe cards 2 over pia itoe total 1.5+ nilitia million 1.7 aiseee noma sana ila kwa jinsi tulivyokuwa sugu hatuna hata vwasiwasi kana kwamba hakuna kilichotokea ila wakamaria

Lakini niseme ukweli, kuna ile furaha ya kishenzi... uko umefulia halafu ghafla unaboom. Sasa ile boom ndiyo inafanyaga mtu arudi tena na tena mpaka unagundua umetoa zaidi ya ulichowahi kushinda. Hapo ndipo akili inakaa sawa.

Ok tuje kwenye topic Kwa sasa niko nje ya nchi nasoma. Bahati nzuri kila mwezi napata allowance ambayo ukiibadili ni kama milioni 1.2 za Kitanzania. Mbali na hiyo, nina mshahara wangu Tanzania kama kawaida . Kwa hiyo sometimes nikiishiwa huku huwa navuta kidogo kule maisha yanaendelea.

Kifupi sina bills za maana. Kodi silipi, watoto wa kulipa ada hakuna, umeme na maji sihangaikii. Matumizi yangu makubwa ni kula, kutembea, kunywa kidogo na kupoteza muda maana hata mademu nimejikuta ile wenge nalo limepungua naweza kukaa hata mwezi sijatafuta manzi na ni fureshi tu kimsingi sihongi hela zangu..nina vipesa havina kazi..

Nikikaa nikajibana vizuri naweza hata nisiguse kabisa allowance ya huku nikawa naishi kwa fedha zinazoingia Tanzania.

Sasa shida ndiyo inaanzia hapo.

Hizi hela zikikaa tu account zinaniona kama zimekaa bure. na siunajua sisi wakamaria walevi ili tupate amani ni mpaka hela ziishe..Ngoja nibeti game mbili tu.

Baada ya siku tatu najikuta nauliza, "Hela zimeenda wapi tena?na ndipo sasa moyo unapata amani hahahah

Sasa nina jamaa yangu dogo tu kwao ni Myanmar anafanya Forex. Kitu kimoja ninachomkubali ni mkweli. Akipigwa anasema nimepigwa. Hakuwahi kuniambia eti kila siku anatengeneza pesa.

Kwao maisha yako vizuri kidogo kila mara safari nyingi na familia yao singapore ,australia hazikauki. Mama yake anauza magari, hivyo matumizi yake ya kila mwezi yanazidi hata milioni 3 za Kitanzania anatumiwaga za kula tu na mafuta maana kapewa gari na mama yake Lakini nilichonishangaza ni malengo yake.

Yeye anasema account ikisoma USD 10,000 bado haoni kama ana pesa. Ndoto yake ni siku moja account isome USD 1,000,000. nikajua huyu anaishi sayari nyingine. 😂

Sasa nami nikasema ngoja nijaribu hii Forex.

Lakini kuna kitu kinanifanya nirudi nyuma.

wanaosema eti lazima ujifunze miaka miwili, usome price action, support, resistance, liquidity, market structure, candlestick, psychology, risk management, ICT, SMC, order block, Fair Value Gap... jamani akili yangu imechoka. 😂

Mimi kwa sasa nikipata muda nataka kusoma JF, kunywa wine, kulala na kuendelea na maisha. Sitaki kukaa mbele ya laptop masaa manne naangalia mishumaa ya kijani na mekundu inagombana.

Kinachonipa moyo ni kwamba safari hii siingii nikiwa mjinga kama zamani. Nimeshasikia hadithi nyingi za utapeli wa Forex, account managers, signal za miujiza, robot zinazodai hazipotezi, na watu wanaokodisha Lamborghini kwa ajili ya Instagram. Hayo angalau najua nitayakwepa.

Kuhusu risk management hapo ndiyo naona naweza kujifunza.

Mimi nikiamua kuingia, nafikiria kuanza na kama USD 400. Nikipoteza, sitaenda kukopa wala kuuza kiwanja. Nitahesabu ni ada ya kujifunza kwa sababu kila mwezi bado kuna kipato kinaingia.

Mpango wangu ni kujipa miezi mitatu. Nikiona sifiki popote naona bora nirudi kutumia hizo hela kunywa na kutembea kuliko kuzichoma nikiwa na matumaini ya utajiri wa haraka.

Sasa naomba ushauri wa wale ambao mmefanya Forex kwa muda mrefu.

Maswali yangu ni haya:

Je, kweli lazima mtu akae miaka mingi akisoma graph ndipo aanze kupata matokeo?mbona hata waliosoma sometimes bado wanapoteza hela,
Kama nataka basic tu, nijifunze vitu gani vitatu au vitano vya muhimu kabisa?
Je, USD 400 au 500 hivi inaweza kuwa ada nzuri ya kujifunzia bila kujiumiza?

Au mnanishauri kabisa nisiingie, niendelee kula maisha yangu ya kawaida na kuacha kutafuta matatizo mapya?

Na je hamna kitu kinachoitwa bahati nasibu katikA forex yaani huwezi tu kuwa na zali ukawa una trade randomly kama kichaa na bado ukaotea kama ukiwa na luck siku hiyo?maana hata kwenye sport betting tunasema knowledge muhimu ujue stats sijui uangalie head to head lakini kanji akiamua kukushangaza anakushangaza na hakuna kitu utafanya na wewe ukiamua kumshangaza unamshangaza je forex nayo haiko hivyo?maana target yangu nataka kwa siku iwe hata dollar 20 au 30 tu sasa hadi hio hela natakiwa niisome forex miezi na miezi?
 
Kubet chance ya kuwin ni 1-3% kwenye 100.
kuwa profitable kwenye betting ni lazima MTU auze mikeka au awe na sure lead.

Forex na Luck havikai meza moja, Kuna MTU nilimnkuu.

Kabla ya kufanya biashara zenye high risk ni muhimu MTU awe na solid cash flow angle hiyo biashara zenye high risk zitakupa stress za kawaida au kurisk 1% ya mtaji
 
Ingia mtandaoni tafuta mechi moja yenye uwezo mkubwa kupata draw (tumia Ai kuuliza kama wewe mvivu, mwambie akupe mechi moja tu yenye high posibility ya kutoa draw kwa siku hiyo). Ukitumia utaratobu huu uwezi kukosa mara tano mfululizo..

Mara nyingi odds zake ni 3.24 hadi 3.37, nini cha kufanya?

Day one mfano weka
50, 000/= inamaana utapata 150,000 ukikosa

Day two weka tena
50,000/= inamaana utapata 150,000/=
hapo kama ulikosa day one inamaana faida ya leo itakua imefidia hadi ya jana, ikitokea day one na two umekosa

Day three weka
100,000 hapo utapata 300,000
Ambayo inafidia hela uliyo weka siku zote tatu na faida ya laki juu..
Day four hivohvo kikubwa utenge mtaji wako ukae pembeni.

Ukitaka kuamini nnacho kwambia wewe tafta daftari utafte hiyo mechi yenye uwezo mkubwa wa kudraw kwa siku hiyo anza kurekodi kabla ujaanza kubeti alafu utaniambia.
 
kwa kuwa una hela za kuchezea kitu pekee ninachokushauri endelea kubet
mkuu capital ya usd 500 ukiamua ku trade na target kila siku iwe dollar 10 tu haiwezekani?yaani tamaa ukaachans nayo ni wewe tu kucheza ikifika dollar 10 basi....sio rahisi kama navyofikiria au?
 
Ingia mtandaoni tafuta mechi moja yenye uwezo mkubwa kupata draw (tumia Ai kuuliza kama wewe mvivu, mwambie akupe mechi moja tu yenye high posibility ya kutoa draw kwa siku hiyo). Ukitumia utaratobu huu uwezi kukosa mara tano mfululizo..

Mara nyingi odds zake ni 3.24 hadi 3.37, nini cha kufanya?

Day one mfano weka
50, 000/= inamaana utapata 150,000 ukikosa

Day two weka tena
50,000/= inamaana utapata 150,000/=
hapo kama ulikosa day one inamaana faida ya leo itakua imefidia hadi ya jana, ikitokea day one na two umekosa

Day three weka
100,000 hapo utapata 300,000
Ambayo inafidia hela uliyo weka siku zote tatu na faida ya laki juu..
Day four hivohvo kikubwa utenge mtaji wako ukae pembeni.

Ukitaka kuamini nnacho kwambia wewe tafta daftari utafte hiyo mechi yenye uwezo mkubwa wa kudraw kwa siku hiyo anza kurekodi kabla ujaanza kubeti alafu utaniambia.
nimekuelewa naijua hio strategy...ni fibbonacci pia martingale ila sometimes ukienda draw zaidi ya 7 hujala inakuwa hatari unaweza kupata stroke
 
@Fb

duh kanji ukisema upige hesabu lost na won kila mwisho wa msimu lazima uwe umechezea wewe
Watu wa IT wangekuwa wametutengenezea kweny account za kubetia sehemu ya kufanya calculation hesabu za ulizo win na kuloose na kutoa jibu kwamba unapata hasara au faida
 
Mleta mada peleka hzo pesa kwenye viwanda.... Usaidie madogo mtaani
ni hela ndogo tu million kwa mwezi kweli nikagawe..mimi nipo tayari ku risk japo na mimi nitateseka kwa mwezi mzima hakuna starehe...forex kwa saa watu wana trade zaidi yadollar billion 300...kweli mahela yote hayo ushindwe ku make dollar 30 tu kwa siku..dollar 30 tu hata zikiwa 10 au 20 sawa
 
Anza kutrade mara moja kikubwa Risk management.
Pia wewe ni muajiriwa unaingiza pesa kila mwezi utafanya bila mihemko. GOOD LUCK kwenye upambanaji wako.
 
Anza kutrade mara moja kikubwa Risk management.
Pia wewe ni muajiriwa unaingiza pesa kila mwezi utafanya bila mihemko. GOOD LUCK kwenye upambanaji wako.
yeah target me ni kupata dollar 30 tu kwa siku zinanitosha..ndo maana nauliza kuna haja hata hizo dollar 30 nianze kusoma deep sijui nifanye demo account
 
Kama unaona uvivu kukaa mbele ya laptop kujifunza achana nayo utapoteza pesa
 
Pesa za kudanlodi sio
lengo ni dollar 20 au 30 tu kwa siku..mtaji dollar 500 je nahitaji kuanza kusoma madude deep kwa ajili ya kuja kugombanisha buy na sells tu..si heri nijue basic tu
 
Back
Top Bottom