Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna mambo katika Taifa hili huwa yanafanyika mpaka unajiuliza, sisi ni Taifa la namna gani?
Mojawapo ya mambo yanayoonekana kutudhalilisha wote kama Taifa ni hili la katiba mpya.
Katiba ni ya wananchi wote, siyo ya wanasiasa na siyo ya vyama vya siasa.
Kinachoitwa kamati ya katiba, hiyo iliyotoa taarifa yake kwa Rais Samia, wajumbe wake na miongozo yake ya kufanya kazi, vimeandaliwa na Mutungi. Mutungi ni msajili wa vyama vya siasa. Ni sheria ipi, ni katiba gani imempa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kushughulika na mambo ya katiba mpya? Mutungi ni nani kwenye suala la katiba mpya?
Tume ya Jaji Warioba, kuanzia kuundwa kwake na mchakato wote viliongozwa na sheria iliyotungwa na Bunge, haka kamati kalikoundwa na Mutungi, kameundwa kwa sheria gani?
Msajili wa vyama ashughulike na mambo yanayomhusu. Watanzania tusifanywe wajinga kwa kiwango hiki. Haya ni matumizi mabaya ya easilimali za Taifa.
Tume ya Warioba ilikwishatoa ripoti yake, na ilitamka wazi kuwa WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA. HATA WALE AMBAO HAWAKUSEMA MOJA KWA MOJA KUWA WANATAKA KATIBA MPYA, MABADILIKO WANAYOYATAKA YANAAMAANISHA UWEPO WA KATIBA MPYA.
Kauli ya Rais Samia kusema kuwa wanaotaka katiba mpya ni watumiaji wa mitandao, watanzania hawataki katiba mpya, nayo ni kauli iliyokosa weledi. Kwani wanaotumia mitandao siyo Watanzania? Rais mwenyewe anatumia twitter, ina maana na yeye siyo Mtanzania?
Kauli na matendo ya viongozi yanaondoa kuaminiana. Tuheshimu maamuzi ya wananchi, hata kama hatuyapendi. Kiongozi mwenye busara na hekima, ni lazima, siku zote uangalie maamuzi ya wananchi, wananchi wanataka nini. Wanachokitaka wananchi, na ambacho walikwishakitolea maamuzi, ni lazima iwe ajenda ya kipaumbele cha kwanza kwa kiongozi yeyote mwenye busara na anayetambua majukumu ya kiongozi.
Hakuna haja ya vijikamati kwenye suala la katiba. Kamati iliyoundwa na Mutungi, msajili wa vyama vya siasa, halafu ikaenda kushughulika na suala la katiba mpya, ni ubatili, kamati yenyewe ni batili na hata maamuzi yake ni batili. Wananchi tunatakiwa kuyapuuza maana wananchi hawakuwahi kumpa Mutungi kazi ya kushughulikia katiba mpya iwe kwa kupitia sheria ya usajili wa vyama vya siasa, au kwa sheria nyingine yoyote ile.
Mod: naomba isomeke
MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU KATIBA MPYA, KISHERIA NA KIMANTIKI, NI BATILI.