Rais Samia, kama anataka kufanya kazi yake vizuri, aache kila mara kuufikiria uchaguzi wa 2025. Aliwazuia wenzake wasifikirie uchaguzi wa 2025 ili abakie yeye pekee yake wa kufikiria uchaguzi wa 2025?
Aiweke akili na moyo wake huru, atapata heshima ya kudumu. Aamini kuwa anaweza kuchaguliwa kuwa Rais mwaka 2025, na anaweza asichaguliwe. Anaweza kuwepo 2025, anaweza pia asiwepo (tunaoamini katika Mungu, tunatambua kuwa maisha yetu yapo mikononi mwa Mungu wakati wote, hatujui siku wala saa ya kuondoka katika Ulimwengu huu). Anatakiwa kufanya yaliyo mema sasa maana ndio wakati alio na uhakika nao.