mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Kiufupi HATAKI
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuwa lazima afe,ili Watanzania tupumue na kupata uelekeo ulio sahihi.Hata kifo cha JPM ninakihusisha na Katiba ya 1977.
Kuna uwezekana mkubwa agebadili katiba Angekuwa Hai Leo
Watanzania wapole sana, tena tunakuwa wapole zaidi tunapozidi kuchokozwa, hii species yetu inatakiwa ipelekwe maabara kuchunguzwa ni ya sampuli gani.
Ww mende huna hoja .Wewe mbwa hujui chochote hapa kaa kimya, utapata katiba vipi bila kupitishwa na wabunge?
Au umejitowa akili hujui bunge ni Magufuli ndio kateuwa Wabunge? kama mpaka Chadema walichaguliwa wabunge wa viti maalum hapo kuna bunge au kundi la mahoka?
Magufuli tutaendelea kumsema kwa miaka mingi ijayo na mbele ya safari tutataka haki ya kumshtaki marehemu, huyu ni shetani aliyeacha damage kubwa kwa Taifa ambayo itaendelea kutugharimu kwa miaka mingi ijayo.
Hilo ni bunge la Ccm.Hivi tuseme mama leo aseme haya tuandike katiba, kwa bunge lipi la kufanya endorsement?
Hilihili bunge aliloliteuwa Magufuli la kina babu Tale?
Ni kweli kazi ya Bunge la katiba ilishakwisha (japo rasimu ya Warioba ilifinyangwa na wenye nchi) kilichobaki ni kura ya maoni tu.Tunaenda kwny kura ya maoni
Bunge lilishakaa na Rais wa sasa ndie alikuwa Naibu Spika…hawezi kufuta kazi ya kihistoria aliyosimamia
Hahahahaaaa.. kamati yenyewe nimeona na yule Mufti wa Dar yumo naye, akitabasamu ulaji waliopewa.... kaaazi kwelikweli na tuwe wapole tu ...Kwakweli ni batili kwa asilimia mia moja na haina weledi hata chembe wa kujiita kamati ya kusimamia jukumu kubwa kama hilo
Kwa Tume ipi ?!Katiba Mpya,itapatikana kwa njia rahisi kwa kupiga Kura Za hapana kwa Samia.
Pia tutaondokana na Muungano.
tupunguzeni upole maana ukizidi tunaambiwa unaleta uzuzu - tujaribu kuwa serious kwenye mambo yenye maslahi ya taifa. Suala la katiba si la kuchezea namna hii - Katiba ndimo haki ilipo ya kila raia wa nchi hii.Watanzania wapole sana, tena tunakuwa wapole zaidi tunapozidi kuchokozwa, hii species yetu inatakiwa ipelekwe maabara kuchunguzwa ni ya sampuli gani.
Utaendaje kwenye kura ya maomi kwa kitu unachojua kilifinyangwa.Naamin ata hiyo rasimu ya warioba ina mambo mengi muhimu yakurekebisha maana kwa miaka tu ya hivi karibuni yamejitokeza mengi yakutufundisha.Ni kweli kazi ya Bunge la katiba ilishakwisha (japo rasimu ya Warioba ilifinyangwa na wenye nchi) kilichobaki ni kura ya maoni tu.
Mutungi tangi ashike hiyo nafasi, kitu pekee alituhakikishia ni unafuki wake na kupenda kuwa kibaraka wa watawala.Maana ya Mutungi ni mfugaji .
Lakini kwa kweli Tanzania imekosa viongozi wenye kujua nchi inahitaji nini na nini kifanyike ,tuna viongozi ambao hawana dira na maono Sasa kwa Hali hiyo hawawezi kuleta maendeleo.
Pasko Mayala Juzi alisemaje hili Jambo kwamba Tanzania kama taifa hatuna vipaumbele Kila kiongozi akiingia ni kufanya yake anayoona anayaweza .Tujisahihishe kwa kweli kama Tunataka kwenda mbele
Chief hangaya ameishanogewa ikulu hataki kuondoka kirahisiKuna mambo katika Taifa hili huwa yanafanyika mpaka unajiuliza, sisi ni Taifa la namna gani?
Mojawapo ya mambo yanayoonekana kutudhalilisha wote kama Taifa ni hili la katiba mpya.
Katiba ni ya wananchi wote, siyo ya wanasiasa na siyo ya vyama vya siasa.
Kinachoitwa kamati ya katiba, hiyo iliyotoa taarifa yake kwa Rais Samia, wajumbe wake na miongozo yake ya kufanya kazi, vimeandaliwa na Mutungi. Mutungi ni msajili wa vyama vya siasa. Ni sheria ipi, ni katiba gani imempa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kushughulika na mambo ya katiba mpya? Mutungi ni nani kwenye suala la katiba mpya?
Tume ya Jaji Warioba, kuanzia kuundwa kwake na mchakato wote viliongozwa na sheria iliyotungwa na Bunge, haka kamati kalikoundwa na Mutungi, kameundwa kwa sheria gani?
Msajili wa vyama ashughulike na mambo yanayomhusu. Watanzania tusifanywe wajinga kwa kiwango hiki. Haya ni matumizi mabaya ya easilimali za Taifa.
Tume ya Warioba ilikwishatoa ripoti yake, na ilitamka wazi kuwa WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA. HATA WALE AMBAO HAWAKUSEMA MOJA KWA MOJA KUWA WANATAKA KATIBA MPYA, MABADILIKO WANAYOYATAKA YANAAMAANISHA UWEPO WA KATIBA MPYA.
Kauli ya Rais Samia kusema kuwa wanaotaka katiba mpya ni watumiaji wa mitandao, watanzania hawataki katiba mpya, nayo ni kauli iliyokosa weledi. Kwani wanaotumia mitandao siyo Watanzania? Rais mwenyewe anatumia twitter, ina maana na yeye siyo Mtanzania?
Kauli na matendo ya viongozi yanaondoa kuaminiana. Tuheshimu maamuzi ya wananchi, hata kama hatuyapendi. Kiongozi mwenye busara na hekima, ni lazima, siku zote uangalie maamuzi ya wananchi, wananchi wanataka nini. Wanachokitaka wananchi, na ambacho walikwishakitolea maamuzi, ni lazima iwe ajenda ya kipaumbele cha kwanza kwa kiongozi yeyote mwenye busara na anayetambua majukumu ya kiongozi.
Hakuna haja ya vijikamati kwenye suala la katiba. Kamati iliyoundwa na Mutungi, msajili wa vyama vya siasa, halafu ikaenda kushughulika na suala la katiba mpya, ni ubatili, kamati yenyewe ni batili na hata maamuzi yake ni batili. Wananchi tunatakiwa kuyapuuza maana wananchi hawakuwahi kumpa Mutungi kazi ya kushughulikia katiba mpya iwe kwa kupitia sheria ya usajili wa vyama vya siasa, au kwa sheria nyingine yoyote ile.
Mod: naomba isomeke
MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU KATIBA MPYA, KISHERIA NA KIMANTIKI, NI BATILI.
Wakifikiria jinsi Uwepo wa Tume huru na katiba mpya utakavyoleta mabadiliko huku wakiamini hawajaacha ufisadi na wizi vichwa vinawauma sanaKuna mambo katika Taifa hili huwa yanafanyika mpaka unajiuliza, sisi ni Taifa la namna gani?
Mojawapo ya mambo yanayoonekana kutudhalilisha wote kama Taifa ni hili la katiba mpya.
Katiba ni ya wananchi wote, siyo ya wanasiasa na siyo ya vyama vya siasa.
Kinachoitwa kamati ya katiba, hiyo iliyotoa taarifa yake kwa Rais Samia, wajumbe wake na miongozo yake ya kufanya kazi, vimeandaliwa na Mutungi. Mutungi ni msajili wa vyama vya siasa. Ni sheria ipi, ni katiba gani imempa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kushughulika na mambo ya katiba mpya? Mutungi ni nani kwenye suala la katiba mpya?
Tume ya Jaji Warioba, kuanzia kuundwa kwake na mchakato wote viliongozwa na sheria iliyotungwa na Bunge, haka kamati kalikoundwa na Mutungi, kameundwa kwa sheria gani?
Msajili wa vyama ashughulike na mambo yanayomhusu. Watanzania tusifanywe wajinga kwa kiwango hiki. Haya ni matumizi mabaya ya easilimali za Taifa.
Tume ya Warioba ilikwishatoa ripoti yake, na ilitamka wazi kuwa WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA. HATA WALE AMBAO HAWAKUSEMA MOJA KWA MOJA KUWA WANATAKA KATIBA MPYA, MABADILIKO WANAYOYATAKA YANAAMAANISHA UWEPO WA KATIBA MPYA.
Kauli ya Rais Samia kusema kuwa wanaotaka katiba mpya ni watumiaji wa mitandao, watanzania hawataki katiba mpya, nayo ni kauli iliyokosa weledi. Kwani wanaotumia mitandao siyo Watanzania? Rais mwenyewe anatumia twitter, ina maana na yeye siyo Mtanzania?
Kauli na matendo ya viongozi yanaondoa kuaminiana. Tuheshimu maamuzi ya wananchi, hata kama hatuyapendi. Kiongozi mwenye busara na hekima, ni lazima, siku zote uangalie maamuzi ya wananchi, wananchi wanataka nini. Wanachokitaka wananchi, na ambacho walikwishakitolea maamuzi, ni lazima iwe ajenda ya kipaumbele cha kwanza kwa kiongozi yeyote mwenye busara na anayetambua majukumu ya kiongozi.
Hakuna haja ya vijikamati kwenye suala la katiba. Kamati iliyoundwa na Mutungi, msajili wa vyama vya siasa, halafu ikaenda kushughulika na suala la katiba mpya, ni ubatili, kamati yenyewe ni batili na hata maamuzi yake ni batili. Wananchi tunatakiwa kuyapuuza maana wananchi hawakuwahi kumpa Mutungi kazi ya kushughulikia katiba mpya iwe kwa kupitia sheria ya usajili wa vyama vya siasa, au kwa sheria nyingine yoyote ile.
Mod: naomba isomeke
MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU KATIBA MPYA, KISHERIA NA KIMANTIKI, NI BATILI.
Kwli kabisa. Hapa tunahitaji akina "Okiya Omtatah" kupeleka suala hili mahakamani!Waulizeni kina Zitto Kabwe ndio wamepewa jukumu na uhakika wa posho kwa miaka 9 ijayo.
Mtungi mtamwonea tu anatumikia maslahi binafsi kama wanavyofanya viongozi wengineMutungi tangi ashike hiyo nafasi, kitu pekee alituhakikishia ni unafuki wake na kupenda kuwa kibaraka wa watawala.
Watawala walipoamua kumtumia Lipumba kuiua CUF, yeye akawa zuzu hadi kumpa pesa Lipumba huku kukiwa na zuio la baraza la wadhamini.
Leo watawala wamemweka pembeni Lipumba, na kumkumbatia Zito, naye kamweka Zito kwenye kamati yake isiyotambulika popote kisheria ili Zito aweze kupokea hongo ya watawala kupitia hiyo kamati.
Uchaguzi wa 2025 Mama hapati usingizi kabisa.Rais Samia, kama anataka kufanya kazi yake vizuri, aache kila mara kuufikiria uchaguzi wa 2025. Aliwazuia wenzake wasifikirie uchaguzi wa 2025 ili abakie yeye pekee yake wa kufikiria uchaguzi wa 2025?
Aiweke akili na moyo wake huru, atapata heshima ya kudumu. Aamini kuwa anaweza kuchaguliwa kuwa Rais mwaka 2025, na anaweza asichaguliwe.
Anaweza kuwepo 2025, anaweza pia asiwepo (tunaoamini katika Mungu, tunatambua kuwa maisha yetu yapo mikononi mwa Mungu wakati wote, hatujui siku wala saa ya kuondoka katika Ulimwengu huu). Anatakiwa kufanya yaliyo mema sasa maana ndio wakati alio na uhakika nao.