Kamati imetumia 'siasa’ suala la Fei Toto

Tumechoshwa sasa na haya malalamiko yenu yasiyoisha kuhusu huyo dogo. Mkiona hamjaridhika, kateni rufaa ngazi zinazofuata.

Kulalamika tu pasipo kuchukua hatua madhubuti, haisaidii chochote.
 
Uhuni wake upi kuvunja mkataba au kuangalia maslahi yake ????
Kwani mkataba alisaini na nani? au kwenye mkataba wake kuna saini za pande zipi?

So ukijua ndipo utajua kwamba kama kulikuwa na pande mbili wakati mkataba uliposainiwa hata kwenye kuvunjwa lazima pande mbili zihusishwe ndizo taratibu za mkataba.

Hakatazwi kuvunjwa kwani kwenye mpira mchezaji yoyote mkataba wake unaweza kuvunjwa haijalishi amebakisha miaka mingapi, ila lazima pande mbili zihusihwe na taratibu za usajili zifuatwe.
 
Sasa upande wa pili ilikuaje mpaka hakuwahusisha kaka??
 
Nasikia yeye hataki kurudi yanga kapata timu nyingine
Yeye hataki ila mkataba unambana. Sijajua kama unafuatilia mpira, umemuona Mane ,Bayern walikuwa na uwezo wa kucheza rafu kumchukua Mane (sema ulaya kuna taratibu na si uhuni huu wa Fei),ila Mane aliwapa options Liverpool wamuongezee mzigo kwenye mkataba mpya Liverpool wakakataa.

Mane kwa kuwa bado alikuwa na mkataba na Liverpool aliuheshimu mkataba aliousaini, hakugomea mazoezi wala mechi na baada ya mkataba wale kuisha akaondoka FREE. Sasa yy hawezi kuondoka sabau bado anamkataba mwaka na nusu na hataki kufuata taratibu yy na timu inayo mtaka.

Afuate taratibu la sivyo yeye ndiye atakaye umia maana hana sababu ,mshahara mpaka sasa haidai Yanga, TFF kachemka japo ana room ya kukata rufaa CAS.Mwisho wa yote yeye ndiye atakaye umia kwani kwa sasa hawezi cheza timu yoyote na muda si mrefu Yanga wakipeleka malalamiko yao TFF dogo anaweza akala ban na akishamaliza hiyo adhabu atarudi tena kuutumia mkataba wake wa mwaka na nusu.

Sisi tukiongea mnatuambia sababu ni mashabiki wa Yanga nazani juzi ulimsikiliza Rage akimshauri Feitoto arudi Yanga au afuate taratibu za usajili la sivyo yy ndiye ataye umia.
 
Wana simba kwanini mnateseka na suala la fei toto?
Kama mna uchungu sana nendeni CAS
Ukweli mchungu ;
Yanga hana uwezo wa kushinda kesi yoyote ile ikipelekwa CAS kwa kutumia hao wanasheria wake vilaza.

Kesi anazoziweza Yanga ni za hapa Tz kwa kuwatumia wanasiasa kuiwekea vitisho tff.

Kesi ya morisson vigogo wa simba nao wasingeingilia Kati Morisson hapa Tz kwa tff angeshindwa na haki angeenda kuipata CAS .Kwakuwa ili suala la fei limekuwa kama lake binafsi ndo Maana kaminywa kimya kimya.



Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa maumivu unayo pitia jikaze utazoea
 
Mbona maneno mengi point zero, kama mna uhakika atashinda uko cas kwanini msiende nae kama mlivyofanya kwa Morrison?
Kama mlimrubuni kuvunja mkataba nini kinawazuia kwenda cas?
 
Kwanini msiende kumlazimisha arudi kambini? Si mmepewa hiyo haki na Kamati kuwa ni mali ya Yanga?
Hakuna mfanyakazi analazimishwa kwa nguvu kurudi kazini. Anabanwa na sheria tu
 
We ni mwanasiasa? We ndio una shida hujui hata maana ya siasa. Chombo halali kitumie sheria zilizopo mbele ya wanasheria wanaoeleweka leo kirahisi tu limeamuliwa kisiasa. Hivi siasa mnaichukuliaje? kwamba ni jambo la hovyo. Acha ushabiki wa hovyo wacha dogo avune alichopanda. Tatizo la vitoto vya kiswahili vikipata mafanikio kidogo hawajui cha sheria wala taratibu, hawajuikm kuna wakubwa tena. Feitoto ana tabia za kitoto tena za hovyo kabisa.
 
Uwe na tabia za kuaminika mamlaka halali za nchi siyo kila kitu ujuaji, ubishi ni tabia isiyo na heshima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…