macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Hivi watu wengine huwa mna akili zenu au mmeshavuta vya kuvuta. Yaani wewe kwa akili yako mtoto wa Rais ana nguvu/heshima ama hadhi yoyote kama kiongozi wa serikali ama vinginevyo? Yaani watu wengine kama hamna vya kuongea embu chukua pipi umng'unye uwaache watu wenye hoja waandike mambo ya maana. Ati kwa kuwa ni mtoto wa Rais basi afanye atakalo? EBO!. Nyamaza na tulia kabisa, usilete tena upuuzi kama huu jamvini, just shut the hell up.
Dark City,
Huyu anajimaliza tena vibaya, hata ulimwengu, Balozi Badora walipiga kelele hivi hivi vitu vilipowekwa hadharani walifayata. CCM hawawezi kukurupuka kiasi hicho, na kama hivyo vyeti ni feki basi wanamfunga.
mkuu nahisi alipost kwa maana ya kisengele nyumaHivi watu wengine huwa mna akili zenu au mmeshavuta vya kuvuta. Yaani wewe kwa akili yako mtoto wa Rais ana nguvu/heshima ama hadhi yoyote kama kiongozi wa serikali ama vinginevyo? Yaani watu wengine kama hamna vya kuongea embu chukua pipi umng'unye uwaache watu wenye hoja waandike mambo ya maana. Ati kwa kuwa ni mtoto wa Rais basi afanye atakalo? EBO!. Nyamaza na tulia kabisa, usilete tena upuuzi kama huu jamvini, just shut the hell up.
Kama ni jibu kwa mwalimu aliyeuliza swai hili, basi una max zote!!! SIMPLE AND CLEAR!Wataalamu wa phyisics wanasema there is no work done if there is no distance moved. Kwa mfano hata ukitumia maguvu kiasi gani kusukuma ukuta na usisogee, hakuna workdone yeyote hapo. Na mimi nasema, kujadili kauli za Makamba ni sawa na kusukuma ukuta. Makamba akitamka kitu, the best you can do ni kumshangaa!
. Maana kama CCM ni watu wa haki hawawezi kusema mtu aliyepata kura 2000 hakubaliki ila aliyepata kura 1500 ndiye anayekubalika hivyo kupitishwa kuchukua nafasi ya mtu aliyepata kura 14,000!!!!!.
mkuu nahisi alipost kwa maana ya kisengele nyuma
Hofstede,
Msimdanganye huyu kijana , CCM wameishamalizana naye wala hana sababu ya kubishana nao magazetini kama anataka tu kuchaguliwa si aende vyama vingine? kila chama kina utaratibu wake. S.M.P2503 katoa ufafanuzi mzuri saana, na si Tanzania tu hata nchi za ulaya wanayo hii ila wao tunapisha kuwa unakuwa raia moja kwa moja kama mama yako ni raia wa nchi hiyo, ila kama baba yako ni raia basi wewe ukifika 18 lazima uombe uraia. Kigezo kuwa mama yake ni mtanzania hakina nguvu kwani sheria zetu zinasema unakuwa mtanzania moja kwa moja kama baba yako ni mtanzania.
Mkuu... raia wa 'Somalia' wanaruhusuwa kugombea ubunge Tz?..ingekuwa mimi ndiyo Bashe, ningehama tu chama.
..kama ana nia ya kuwawakilisha wana Nzega siyo lazima iwe kupitia CCM.
Makamba si kiongozi wa kitaifa !
Kamati kuu ya chama cha mapinduzi imemtosa kijana mahili na chipukizi kwenye siasa Bwana Husein Bashe ambaye aligombea kura za maoni ccm kupitia jimbo la nzega na kumbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bwana lukas selelii kwa jumla ya kura 14,200 za Bashe,dhidi ya 2700 za selelii,na sababu yao kubwa ni kwamba ni kutokana na utata wa uraia wake na si raia wa jamuhuri ya muungano wa tanzania
Lakini tukirudi nyuma huyu bwana bashe ,NI MJUMBE WA BARAZA KUU UMOJA WA VIJANA TAIFA (UVCCM),NI MJUMBE MKUTANO MKUU WA CCM MKOA TABORA,AMEWAHI KUGOMBEA NAFASI YA NEC UVCCM TAIFA na AMEWAHI KUGOMBEA MAKAMO MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA.
Kinachoshangaza sehemu zote hizi ni lazima wapitie na kuthibitisha kuwa yeye ni raia na baada ya kuridhika ndipo hupewa ruksa ya kugombea ama kuwa kiongozi .
Swali gumu Ni kigezo kipi ambacho kilisahaulika leo ndio kimetumika?,kwa hisia za haraka hapa kuna mkono wa mtu
ILa kwa mbali kuna fununu kwamba huyu Bwana Bashe hana mahusiano mazuri na mtoto wa MH.Rais Ridhwani Kikwete hasa baada ya uchaguzi wa makamo mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambapo bwana Bashe alishiriki na Swahiba wa Ridhwani Bwana Beno Malisa..!!
Je CCM inatufunza nini? na Tunakwenda wapi..?