Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

CCM ina wenyewe
 

Kazi kweli kweli, hata kama ni ubaguzi huu wako umezidi. Kama ni watanzania lakini wana nasaba za kisomali haiwaondolei u Tanzania wao. Na wana haki kama watanzania wengine , kama ya kugombea nafasi kama Ubunge.

Lakini Kapuya, Nkumba, Mfutakamba, na Kingwangala ni wasomali?.
 
It looks like the guy trespassed into someone's territory. CCM hii tunayoijua inaangalia uraia, tuhuma na kesi mahakamani? Sababu zinazotolewa kuwatetea akina Chenge, Mramba hata haziingii kwenye kichwa cha mtu hai, let alone kama ana akili timamu au la!
LAKINI: Mlitarajia nini tofauti kutoka kwa CCM? Bila kuukomesha huu umwinyi, ni dhahiri kuwa tumebinafsisha nchi kwa watu wachache.
 
Tukichukulia kwamba habari hizi ni kweli swali la kujiuliza ni je mtu aki hisiwa si raia hatua inayochukuliwa ni kumfukuza uanachama tu? Hamna process ya kutafuta verification kupitia vyombo husika na kumchukulia hatua za kisheria?
 
Kwenye picha nawaona mafisadi wawili watoto in the making....Hussein Bashe na Francis Isack, former naibu katibu mkuu wa UVCCM taifa (sasa DC Bunda)....Kwa nchi yetu ilipofikia ni aibu hata kujitambulisha kuwa wewe ni mwanasiasa hasa kutoka chama tawala.....yule DC aliyekamatwa na PCCB suala lake kimya, mama Sitta kimya...Maskini Mwakalebela!
 
Je kuna anaefahamu kama ikiwa kwa sasa bwana Bashe hana uraia wa nchi yoyote mpaka atakapoomba upya uraia wa Tanzania, je ukaazi wake umesimamia wapi Tanzania au Somalia au ndio amepewa Grace Period ya mwezi mmoja?
 
Nadhani sheria zingine inatakiwa ziwe za kimataifa, Mtu kazaliwa Tanzania, leo unakuja kumwambia si raia wa hii nchi~sasa sijui yeye ni raia wa sayari gani, Mars?. Ni bora hawa CCM wangemtengenezea zengwe lingine lakini kwa hili la uraia mmhh...It doesn't make any sense to me!.
 
========

Nisamehe bure Mfumwa
Unajua CCM wamemwaga ugali nikaamua nimwage mboga! Kumwona Rage anaachwa wakati Bashe anaondolewa inachefusha. Lakini je Kapuya amebaki Tabora au ameenda mkoa mpya?
 
Dogo ndo kishaingia choo ya KIKE...elimu yake yote...matatani sasa..maana si Raia...Duuuuu SIASA mchezo mchafu
 
Yaani kuna wkt nikisoma habari za bongo zinachefua mpaka basi, why now?
 
CCM wanachemsha wanajitahidi kuweka watu wa mtandao kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.... Sijui wanamini vipi kuwa wana upata ushindi mwaka huu?....kama swal la uraia mbona hatuusikii kwa kina Dewji,Manji,Rostam,Kinana,Raage?
 
Bashe kazaliwa Tanzania; ana cheti cha kuzaliwa Tanzania! Hii haiingii akilini wala kisheria kwani anayezaliwa nchini anakuwa raia hadi hapo yeye atakapoukana huu uraia wa kuzaliwa. Hivyo Bashe hatakiwi kuomba uraia wa Tanzania kama hajaukana. Kama Bashe angezaliwa Somalia na akaja Tanzania hata kama angekuwa na umri wa siku moja; hapo angesitahili kuukana uraia wa Somalia na kuomba uraia wa Tanzania. Hii yote ni mizengwe tu; Bashe ni Mtanzania.
 
Baija Bolodi,

Hivi Kapuya, Mfutakamba, Saidi Nkumba na Selemani Zedi nao wote hawa ni wasomali? jamani hebu tuangalie maanishi tunayoandika vinginevyo tufute nenoi "The Home of Great Thinkers"
 
Wajameni, kwa nini hatutaki ku argue kwa kutafisiri sheria za uraia zilizopo uhamiaji? kwangu mimi haingii akilini kuhoji uraia wa Manji, RA na wengine bila kuwa na taarifa zaidi hii inatupotezea umakini wetu na kushusha hadhi ya jukwaa. Tujadili tukiwa na data siyo bifu na wivu binafsi.
 
Muzee, ukifikisha miaka 18 unatakiwa uukane uraia mmoja, hakuna uraia by default kwa wageni.
 

Ni mshangao kwa nini huyu Bashe miaka yote hiyo na nyadhifa zote hizo leo ndio aambiwe si raia.....kuhoji ni wajibu kwa vile yeye anakanusha ni Chilly ametoa data basi tungojee naye data zake.
 
Hawa nao wanawazuga watu tu.. hivi Chiligati akiulizwa Rostam alizaliwa wapi na lini anaweza kutoa jibu?
 
Hawa nao wanawazuga watu tu.. hivi Chiligati akiulizwa Rostam alizaliwa wapi na lini anaweza kutoa jibu?

Hah ha ha ha! hii ni kama ile ya Hassan Diria[marehemu] alikuwa msomali tena ukoo wake ni maarufu sana. Uliza wasomali wote wanamjua vizuri sana hasa wale kutoka Bosaso na Hangisa, hakuna aliye hoji!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…