GE2025 Kamati Kuu CCM yatangaza rasmi majina ya watia nia Ubunge 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Viongozi Yanga na Simba yaani Arafat Haji , Hersi Said na Mangungu wote wamekatwa 😂
 
Naona awamu hii mama na mwanae hawana washindani kwenye kaya zao ?
Yaani hata aibu hawana, wameshindwa hata kuwaadaha watanzania kwa kuweka mpinzan wa kusindikiza tu.

Oyo sana wale watu.
 
Aisee,
Leo nilikua na majukumu magumu nimekua mbele ya computer 💻 macho yanauma ngoja kichwa kipoe Poe nione majina.

NImefurahi kuona jina la gentleman Tlaatlaah
Hongeraa sana Kila la kheri gentleman
Shukran sana gentleman,
Tupo watia nia 6, kivumbi cha kampeni kinaanza kutimua mapema kesho,
Tuombeane kheri 💪🙏
 
Hakuna tija yoyote ile, ni ufujaji wa fedha za Kodi za Wananchi
 
Yaani hata aibu hawana, wameshindwa hata kuwaadaha watanzania kwa kuweka mpinzan wa kusindikiza tu.

Oyo sana wale watu.
Yaani Jah kaya kabisa akubali mke na mwanaye wapate washindani naye ndiye mwenye nchi? Thubutuu
 
Watajuana wenyewe, mambo Yao tuwaachie wenyewe maana hakuna atakayekuletea mkate mezani usipoutafuta mwenyewe.
Hii ndiyo point muhimu sana ya kwenda nayo mkuu. Hawa wanatafuta ajira kivyao, nasi tujitafutie ajira kivyetu
 
Familia ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN
1. Mtoto - Wanu Hafidh Ameir
Jimbo: Makunduchi, Zanzibar



Familia ya RAIS MSTAAFU MRISHO KIKWETE
1. Mke - Salma Kikwete
Jimbo - Mchinga

2. Mtoto - Ridhiwani Kikwete
Jimbo - Chalinze



Familia ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo pinda
1. Mtoto - Geophrey Privatus Mizengo Pinda
Jimbo - Kavuu

2. Mtoto - Sylivanus Mizengo Ole Pinda
Jimbo - Ngorongoro



Familia ya Mzee Wasira
1. Mtoto - Kambarage Masato Wasira
Jimbo - Bunda Mjini


Familia ya Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi ambaye pia mtoto wake ni Rais wa Zanzibar (Hussein Mwinyi )
1. Mtoto - Abasi Ali Mwinyi
Jimbo - Fuoni, Zanzibar

2. Mtoto - Fahmy Ali Mwinyi
Jimbo - Mwanakwerekwe, Zanzibar

3. Mtoto - Asma Ali Mwinyi
Jimbo - Welezo, Zanzibar

4. Mtoto - Abdulla Ali Mwinyi
Jimbo- Mahonda, Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…