Wakuu!
Baada ya ahirisha ahirisha sasa ndio muda wenyewe wa kujua mbivu na mbichi huko CCM
Majina ya wagombea wa Ubunge wa Majimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Viti Maalum vya Ubunge na Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yanatarajiwa kutangazwa mchana huu baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kulichomalizika usiku wa kuamkia Julai 29, 2025.
Majina hayo yatatangazwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika kuanzia saa sita mchana.
Awali, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makala, aliitisha kikao na waandishi wa habari kilichotarajiwa kufanyika saa 11:00 jioni ya Julai 28, 2025. Hata hivyo, kikao hicho hakikufanyika kutokana na mchakato wa kuchuja wagombea kutokamilika kwa wakati.
Waandishi wa habari walilazimika kusubiri kwa muda mrefu, kuanzia saa 11:00 jioni hadi majira ya saa 10:00 alfajiri ya leo, walipofahamishwa na Afisa Habari wa CCM, Aboubakar Liongo, kwamba mchakato bado unaendelea na kwamba kikao hicho sasa kitaanza rasmi saa 6:00 Mchana leo, Julai 29, 2025.
Soma zaidi
Taarifa hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa, kwani itabainisha majina ya wagombea waliopenya katika hatua za awali za uteuzi kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama hicho tawala.
Updates
CCM wameongeza tena muda, CPA Makalla atafika ukumbini dakika 35 zijazo (1:25Pm)