Kamati kuu CHADEMA ni batili kukaimisha ni batili na waliokaimishwa ni batili

Kamati kuu CHADEMA ni batili kukaimisha ni batili na waliokaimishwa ni batili

Kwani kukaimisha nini si ni kushikilia tu nafasi by the way. Mpaka hapo wametii maelekezo ya Msajili.Baraza kuu litaitishwa na kukamilisha zoezi
Kwani kukaimu lazima awe Mnyika? Kwani mnyika na na wenzake waliokuwa na hati chafu hawawezi kuwekwa pembeni kidogo hadi pale jambo litakapothibitika sio kweli na hofu ya msajili sio ya kweli.
 
Zandaaaaani kabisa zinasema hata kamati kuu iliyokaimisha waliokaimishwa akidi haikutimia.
 
Msajili wa vyama vya siasa ametengua uongozi wa CHADEMA uliopatikana kwa mkutano na uchaguzi batili.

Kama viongozi wote wale ni batili maana yake hata kamati kuu ni batili pia, hivyo haiwezi kuwa na uhalali wa kukaimisha viongozi,

Kama msajili ametegua uongozi uliopo maana yake uongozi uliokuwepo mwanzo wa akina Mbowe inatakiwa urudi madarakani hadi hapo itakaopothibitika vinginevyo kama uongozi mpya ni sahihi.

Au nakosea?
Umetumwa na Mrema😅😅😅
 
Umetumwa na Mrema😅😅😅
Tena Umenikumbusha jambo, ninachokumbuka mm Mbowe, Lema, Lissu, sugu, Mnyika, Heche, mdee, Nasari, Elizabeth waliwahi kuwa wabunge wa kuchaguliwa, wakati huo wanatangazwa kushinda viti vya ubunge tume ya uchaguzi iliteuliwa na nani?

Hebu tuseme ukweli, kama akina Lissu wangekuwa bungeni wakati wa Magufuli Leo hii tungekuwa na bwawa la umeme la Nyerere, reli ya SGR, ndege zetu, daraja la busisi? Naelewa kwanini ilikuwa lazima wagombea kuenguliwa wote wakati wa Magufuli, wanachelewesha maendeleo.
 
Eleza kwa ufasaha kile msajili asichopenda kwenye uongozi wa cdm ili kuongeza ufahamu wa wadau.
Hoja ya Msajili kwa madai yake ni kwamba uteuzi wao haukuthibitishwa na wajumbe waliowengi....Hicho hakiondoi wao kurudishwa tena kwa njia iliyotumika na kamati kuu this time
 
Kwani kukaimu lazima awe Mnyika? Kwani mnyika na na wenzake waliokuwa na hati chafu hawawezi kuwekwa pembeni kidogo hadi pale jambo litakapothibitika sio kweli na hofu ya msajili sio ya kweli.
Huo ni uamuzi wa uongozi wa juu wa chadema ni hiari yao
 
Unakosea mno, mkuu.

Rejea suala la James Mbatia - ule utenguzi wa msajili umebatilishwa mahakamani.

Huku ni kupotezeana muda, nguvu na malengo - kutumia mamlaka isivyotakiwa.

Mambo haya yote ndiyo yanazidi kukoleza ajenda za Sidiemu za NRNE na Katiba Mpya.
Kazi kweli kweli bandugu
 
Msajili wa vyama vya siasa ametengua uongozi wa CHADEMA uliopatikana kwa mkutano na uchaguzi batili.

Kama viongozi wote wale ni batili maana yake hata kamati kuu ni batili pia, hivyo haiwezi kuwa na uhalali wa kukaimisha viongozi,

Kama msajili ametegua uongozi uliopo maana yake uongozi uliokuwepo mwanzo wa akina Mbowe inatakiwa urudi madarakani hadi hapo itakaopothibitika vinginevyo kama uongozi mpya ni sahihi.

Au nakosea?
Waliompitisha Samia kugombea ni batili.
 
Huo ni uamuzi wa uongozi wa juu wa chadema ni hiari yao
Vyama hivi lazima vifuate sheria, kanuni na miongozo, maana ruzuku ni Kodi za wananchi. Lissu ndiye chanzo cha tabu za chadema. Lissu haamini kama Kuna Rais, polisi, usalama wa taifa, muungano na uongozi wenye maana Tanzania. Hii itamchelewesha sana yeye pamoja na chadema.
 
Waliompitisha Samia kugombea ni batili.
CCM wamejipambanua tangu zamani kuwa wanao utamaduni wao wa vipindi viwili kwa kila Rais, ni utaratibu ambao hata Nyerere aliufahamu na kuubariki. Kwanini utaratibu huo uwe haramu kwa Samia tu?
 
Back
Top Bottom