Ili upate uhalali wa ku - argue, kwanza uielewe katiba ya CHADEMA
Ndani ya katiba ndo kuna composition ya wajumbe wa kamati kuu
Na kwa kadiri ya ufahamu wangu kamati kuu ina zaidi ya wajumbe 30
Msajili wa vyama anadai kutowatambua wajumbe wasiofika 10.
Maana yake nini, hata kama hao 10 hawana uhalali wa kushiriki vikao vya maamuzi, kolamu inayobaki inatosha kufanya uamuzi wowote kisheria na kikatiba.
Sasa tuambie, kwanini maamuzi ya kamati kuu ni batili? Wajumbe (kolamu) haitoshi? Nini msingi wa hoja yako?