Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi.
Tukubali tukatae CCM ni chama kikubwa, kikongwe, kina uzoefu katika medani ya siasa za Tanzania na wakati wa Mwl Nyerere kilikuwa na mitazamo iliyovuka mipaka ya Tanzania (Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika) na pia masuala ya utangamano wa kikanda na hatimaye Afrika nzima.
Kutokana na ukongwe na ukubwa wake unabaki kushangaa ilikuwaje Askofu Gwajima jina lake likapitishwa na vikao vizito vya chama. Kamati kuu ilishindwa kupata ushahidi wa video za Askofu Gwajima akikashifu dini ya KiIslam, Catholic, Lutheran. Eti kwake yeye dini ya maana ni Assemblies of God.
Ipo Video najaribu kuiweka hapa kwa kweli inashangaza kama si kusikitisha.Askofu Gwajima badala ya kuhubiri/mafundisho ya imani yake kajikita zaidi katika kukashfu imani nyingine tena kwa maneno ambayo hata mimi naogopa kuandika hayafai yamekosa ustaarabu wa kiwango cha kutisha.Ni ajabu sana Askofu Gwajima bado anaoujasiri wa kupita mitaani bila aibu wala uoga wa kuomba kura jimbo la Kawe.
CCM imefanya makosa makubwa,tukubali na kujisahihisha mapema.

Gwajima akiendeleza anayoyaamini.
View attachment 1585654