Uchaguzi 2020 Kamati Kuu (Halmashauri Kuu) walikosea sana kumpitisha Askofu Gwajima kugombea Ubunge Kawe

Uchaguzi 2020 Kamati Kuu (Halmashauri Kuu) walikosea sana kumpitisha Askofu Gwajima kugombea Ubunge Kawe

Heshima sana wanajamvi.

Tukubali tukatae CCM ni chama kikubwa,kikongwe,kina uzoefu katika medani ya siasa za Tanzania na wakati wa Mwl Nyerere kilikuwa na mitazamo iliyovuka mipaka ya Tanzania (Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika) na pia masuala ya utangamano wa kikanda na hatimaye Afrika nzima.

Kutokana na ukongwe na ukubwa wake unabaki kushangaa ilikuwaje Askofu Gwajima jina lake likapitishwa na vikao vizito vya chama !.Kamati kuu ilishindwa kupata ushahidi wa video za Askofu Gwajima akikashifu dini ya KiIslam,Catholic,Lutheran.......Eti kwake yeye dini ya maana ni Assemblies of God.

Ipo Video najaribu kuiweka hapa kwa kweli inashangaza kama si kusikitisha.Askofu Gwajima badala ya kuhubiri/mafundisho ya imani yake kajikita zaidi katika kukashfu imani nyingine tena kwa maneno ambayo hata mimi naogopa kuandika hayafai yamekosa ustaarabu wa kiwango cha kutisha.Ni ajabu sana Askofu Gwajima bado anaoujasiri wa kupita mitaani bila aibu wala uoga wa kuomba kura jimbo la Kawe.

CCM imefanya makosa makubwa,tukubali na kujisahihisha mapema.
Akili zako naona ata wewe mwenyewe hazikutoshi naona umekuwa mshauri wa chama tawala unadhani hawakuangalia ayo unayoyasema kweli wewe topolo Sasa Gwajima ameshapitishwa na anakwenda kushinda kwa kishindo subiri uone

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Waliamini Gwajima atakuwa kiboko ya Mdee (miscalculations), matokeo yake toka apitishwe amekuwa mtu wa kujisafisha sasa hivi ndio amekuja kujistukia he is not popular as he believed kwa watu wa dini zote na makabila yote (including wasukuma) he is just another ‘reprobate’.

Tatizo ni wafuasi wa CDM mtu yeyote akiwa upande wao ujinga wake wowote wana tetea matokeo yake ndio mtu kama Gwajima, bila ya CDM kumkuza wakati yupo upande wao si lolote si chochote.

Overall ukataji wa CCM umekuwa na mushkeli sana safari hii wengi wamepokonywa haki zao ila binafsi sijui kwanini nimemuonea huruma zaidi ‘Kulwa Biteko’ yaani amekatwa kisa pacha wake tayari mmbunge tu, that is not fair under any circumstances.
 
Jamani ifike wakati tuwe na maamuzi ambayo yataleta maendeleo na muache chuki binafsi za kidini
 
Hapo Paskali unakubali kwamba Gwaji alikosea. Na alikosea zaidi alipoapa mbele za Bwana na madhabahu yake kwamba yeye hawezi kugombea Ubunge au Uraisi na kwamba kazi hizo si size yake. Hawezi kugombea vyeo hivyo kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amejishusha chini. Hakuishia hapo aliapa kwamba yeye atamtumikia Mungu aliye hai siku zote za maisha yake. Amekiuka kiapo chake mbele za Bwana na kibaya zaidi aliamua kumla kondoo moja na kuwaacha wengine wengi wakihangaika kutafuta malisho baada ya yeye Mchungaji, kuingia mitini na kwenda kugombea Ubunge. Mtu asiyekuwa na msimamo thabiti, asiyeishi yale anayoyaamini, hatufai.
Huo ni mtazamo wa jicho la kibinaadamu kwa upande wa mipango ya Mungu ni tofauti, Gwajima yule aliyesema hayo na kutenda hayo ni Gwajima mwingine na Gwajima huyu mgombea wa Kawe ni Gwajima mwingine kama ilivyo kwa Sauli na Mtume Paulo.

Gwajima huyu ndie chaguo sahihi kwa Kawe.
P
 
Akili zako naona ata wewe mwenyewe hazikutoshi naona umekuwa mshauri wa chama tawala unadhani hawakuangalia ayo unayoyasema kweli wewe topolo Sasa Gwajima ameshapitishwa na anakwenda kushinda kwa kishindo subiri uone

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app

Si kila jambo lazima ujibu,ukikaa kimya pia ni busara.
 
Huo ni mtazamo wa jicho la kibinaadamu kwa upande wa mipango ya Mungu ni tofauti, Gwajima yule aliyesema hayo na kutenda hayo ni Gwajima mwingine na Gwajima huyu mgombea wa Kawe ni Gwajima mwingine kama ilivyo kwa Sauli na Mtume Paulo.

Gwajima huyu ndie chaguo sahihi kwa Kawe.
P
Nimekuekewa Paskali. Hapo ndio tunaingia kwenye sayansi ya "split personality". Rejea William Shakespeare, Dr. Jekyll and Mr. Hyde. Upande mmoja tunaye Gwaji ambaye ni Mtume Paulo na ule mwingine ni Saul. Hivyo unashauri tumchague Gwaji kama Mt. Paulo na tumwache Gwaji ambaye ni Saul. Tatizo linalojitokeza hapo ni lini utajua kwamba aliyepo leo ni Paulo na si Sauli ili watu waweze kumchagua. Ufumbuzi wake ni kuwaacha wote na si kucheza patapotea.
 
Wakuu nimewaomba moderator waipabdishe video iliyopo bandiko number 30 ili kunogesha mjadala zaidi.

Nimefanya hivyo kwasababu kuna baadhi ya wachangiaji wanatoa maoni yao pasipo kuelewa lengo la mada Hii.
 
Tar 28 octob ndo utajua kama ccm ilikosea maana halima mdee hana chake kawe, Gwajima ameshapita anasubir kuapishwa tu
 
Binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosea ni kawaida. Kufuatia ukongwe na uzoefu wa CCM, CCM, haikukosea kumteua Askofu Gwajima, ndiye chaguo sahihi kwa maendeleo ya jimbo la Kawe.

P
Tunawapenda wake zetu, kumchagua huyu ni hatari kwa ndoa zetu. Hatuwezi kufanya hivyo.
 
Binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosea ni kawaida. Kufuatia ukongwe na uzoefu wa CCM, CCM, haikukosea kumteua Askofu Gwajima, ndiye chaguo sahihi kwa maendeleo ya jimbo la Kawe.

P
Endelea kuota, awamu hii hamchomoki na nyie vibaraka mtapata tabu sana
 
Daaaah,aibu naona mimi,yaani hadi mimi kantukana,huyu kura yangu ataisikia motoni walahi,kwenye ukatoliki kanitukana,kwenyw uislam kanivua nguo,daaaah
 
Hawakukosea kumusimamisha Gwajima, Mungu aliwapiga upofu wamusimamishe Gwajima wapigwe vizuri.
 
Daaaah,aibu naona mimi,yaani hadi mimi kantukana,huyu kura yangu ataisikia motoni walahi,kwenye ukatoliki kanitukana,kwenyw uislam kanivua nguo,daaaah

Hapo ndio utaona tofauti ya CCM ya Dr Magufuli na ileee ya Mwl Nyerere
 
Back
Top Bottom