Kamati kuu ya CCM ilipaswa kupendekeza IGP Sirro aondolewe, sio kutathmini mwenendo wa Tanpol. Ukiukwaji wa haki za binadamu umekithiri hapa nchini

Kamati kuu ya CCM ilipaswa kupendekeza IGP Sirro aondolewe, sio kutathmini mwenendo wa Tanpol. Ukiukwaji wa haki za binadamu umekithiri hapa nchini

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kila kukicha ni malalamiko ya wananchi juu ya ndugu zao kuumizwa au kuuawa wakiwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Mbaya zaidi hakuna hatua zinazochukuliwa ili kuwashitaki wanaofanya haya matendo maovu.

Rais Samia alishakiri hadharani kuwa kuna nguvu ya ziada inayotumika na inaleta madhara kwa raia kinyume kabisa na ibara ya 13 ya katiba ya JMT.

Kwanini CCM na kamati yake kuu wamulike tukio la Mtwara na huko Kilimanjaro tu? Mbona matukio ya polisi kuua raia na kuwatesa na kuwapa ulemavu ni mengi?

Kamati kuu ya CCM ilipaswa kuhakikisha jeshi la polisi linafanyiwa overhauling na Sirro anaondolewa. Iundwe tume huru kubaini waliovunjiwa haki zao na walipwe fidia.

Pitia hii link ili kupata ukatili wa Tanpol

Screenshot_20220313-062346.jpg
 
Igp ziro ni kada mtiifu wa ccm.kuwa IGp ni kuwa mtiifu wa ccm.
toka lini wezi wakasemana au kunyoosheana vidole.
akistaafu tu utasikia anagombea ubunge kupitia ccm
 
Kamati kuu ya CCM ilipaswa kuhakikisha jeshi la polisi linafanyiwa overhauling na Sirro anaondolewa. Iundwe tume huru kubaini waliovunjiwa haki zao na walipwe fidia.
Tuliyasema haya mwanzoni kabisa tulishambuliwa vikali kuwa tuna wivu
 
Wanamtoaje mtu aliyekuwa injinia wa kuwarudisha madarakani na kuzuia Chadema wasifurukute [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uozo wa jeshi la polisi ni zaidi ya IGP.

Chakula kikiwa kimeoza, ukibalisha sahani haisaidii kitu.

IGP kuondoka inaweza kuwa moja ya matokeo ya tathmini.
 
Wakiona vipi lifutwe hilo jeshi la polisi,tuwekewe JWTZ kwenye vituo vya polisi,nadhani malalamiko ya wananchi yataisha.Nawaza kwa sauti.Wafanye tu hivyo,wananchi tutainjoi sana,tena sana.
 
Kila kukicha ni malalamiko ya wananchi juu ya ndugu zao kuumizwa au kuuawa wakiwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Mbaya zaidi hakuna hatua zinazochukuliwa ili kuwashitaki wanaofanya haya matendo maovu.

Rais Samia alishakiri hadharani kuwa kuna nguvu ya ziada inayotumika na inaleta madhara kwa raia kinyume kabisa na ibara ya 13 ya katiba ya JMT.

Kwanini CCM na kamati yake kuu wamulike tukio la Mtwara na huko Kilimanjaro tu? Mbona matukio ya polisi kuua raia na kuwatesa na kuwapa ulemavu ni mengi?

Kamati kuu ya CCM ilipaswa kuhakikisha jeshi la polisi linafanyiwa overhauling na Sirro anaondolewa. Iundwe tume huru kubaini waliovunjiwa haki zao na walipwe fidia.

Pitia hii link ili kupata ukatili wa Tanpol

View attachment 2148529
ccm wanatafuta cheap popularity kwa wananchi.

Hao mapolisi ma RPC na Ma RCO na Makamishina si wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM taifa?? sasa wanamulika nini hapo?
 
Wakiona vipi lifutwe hilo jeshi la polisi,tuwekewe JWTZ kwenye vituo vya polisi,nadhani malalamiko ya wananchi yataisha.Nawaza kwa sauti.Wafanye tu hivyo,wananchi tutainjoi sana,tena sana.
Mimi nina uhakika nchii hii tunaweza kukaa kwa amani kabisa bila jeshi la polisi.
 
Naona makamishina CP ambao hawaivi na IGP wamesimamia kucha hadi kitu imetimba jikoni. So far naona yaliompata mangu yanampata mzee baba mwera mkuu. Ila injinia alipambana hadi jengo likasimama kwenye 2020. Ngoja tuone watamtoa aje pale au panga pangua teua tengua inakuja kwa kishindo.
 
Jeshi la polisi halitakaa liwe Safi wakati ccm wanaendelea kukaa madarakani kwa shuruti. Hilo jeshi la polisi ndio linawaweka madarakani hao wanaojifanya kuwajadili, na polisi wanajua fika walioko madarakani hawana uhalali wa umma. Katika mazingira hayo hiyo kamati ya ccm ni ni kama ina hadaa umma kuhusu maazimio yao.
 
Ukiwa na laki mfukoni polisi wakushike wako teyari ata kukupa kilema ili waondoke na laki yako
 
"Vyombo vingi vya usalama vina hulka na matendo ya kiharifu, tofauti ni moja viko kwa Mujibu wa sheria" -Unknown in the Law of Espionage
 
Back
Top Bottom