Kamati Kuu ya CCM yaielekeza Serikali kuchukua hatua kuhusu maoni ya TOZO

Kamati Kuu ya CCM yaielekeza Serikali kuchukua hatua kuhusu maoni ya TOZO

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa Wananchi kuhusu # Tozo za Miamala ya Kielektroniki.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu ya Taifa imeona kuna umuhimu wa kutafakari kuhusu Tozo iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni.

Amesema “Maelezo hayo yamezingatia Ibara ya 20 Kifungu kidogo B ya Ilani ya Uchaguzi 2025, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa gharama nafuu kwa kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA, kuchochea uwekezaji wa ndani na kukidhi mahitaji halisi ya Wananchi hususani waishio vijijini.”

Beberu anasema haijafanyika hadi iwe imefanyika.

Kauli hii ya walamba asali ingali ni maneno matupu.

Waondoe tozo zote benki na kwenye miamala ya simu.
 
Hii ndy Tanzania ambayo njaa, ya wasomi imefanya wanyongeee, wapapasweee na wala wasifurukute, nchi pekee yenye vyama vya wafanyakazi vibogoyo kabsaa.nchi yenye wananchi waliolala usingizi w pono,Nchi hii ndy the easiest Africa kuitawala hata kama huna manifesto.Nchi yangu nani amekulogha?
 
Tucta ni washenzi Sana!
 
CCM wanatuona Watanzania kama hatuna akili vile! Yaani Mwenyekiti wa hicho chama ndiye aliyebariki hizo tozo, halafu leo wanakuja na maigizo yao ili kutafuta attention.
Yani kuna mambo yanashangaza sana
 
Haya mazingaombwe hata kwetu kwa akina kalumanzila hatujafikia huko. Yaani labda yanapatikana kule "ilipoungua shoka mpini ukabaki"
 
Wakati wanaanzisha au pendekeza hizo tozo hawakujua Kama zitaumiza wananchi?

Vp zile kaul za wazir wa fedha tuhamie Burundi Wanasemaje ?

Nadhan tozo zilianzishwa na CHADEMA Bila shaka maana ndio chama tawala

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom