Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja.
Kwa sababu hiyo, tarajieni kuona wale wale waliowadhulumu haki zenu wakigeuka wema kwenu na kuanza kuonyesha upendo wa kinafiki kwenu na hata wako wataojidai kuwahurumia ila kamwe msiwaamini na wala msiwasikilize.
Hata hill Bunge likianza mtarajie wabunge hawa hawa wa CCM waliofaidika na matokeo haya, wakaanza kutoa kauli za kukumbuka michango ya wapinzani Bungeni, na hata wanaweza kuja na mapendekezo ya kuwapa mialiko ya kwenda Bungeni kama wageni. Kumbukeni baadhi yao pia nafsi zao zitakuwa zinawasuta na watayatenda haya katika kujaribu kutuliza nafsi zao.
Sio hivyo tu,wanaweza kubadili sheria kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Raisi, na pia kubadili kanuni/sheria kuongeza wabunge wa vitu maalumu ili nyinyi mpewa nafasi, ila nawambieni kamwe msikubali bali waachieni wao na Bunge lao watimize azima yao na zaidi wakose kisingizio cha kuja kusema wapinzani wanachelewesha/wanakwamisha maendeleo.
Nawaambia angali mapema kabisa kuwa, mkiwa tayari kupeleka wabunge katika Bunge hili, basi pia muwe tayari na masimango: bila huruma ya Raisi au Spika, wengine msingekuwa humu ndani, tumewabeba, hamna shukurani na kauli zingine za aina hiyo pale mtapopishana nao mitazamo ndani ya hilo Bunge.
Pia, iwapo mtapeleka wabunge katika hili Bunge, matapoteza haki na uhalali wa kupinga huu uchaguzi na watatumia uwepo wenu katika hilo Bunge kama hoja ya kujibu tuhuma zozote zinazohusu makandokando ya huu Uchaguzi.
Pia, tambueni hata wao wanaelewa mna wafuasi wengi sana katika nchi hii, hivyo ili kutuliza hasira na machungu ya mashabiki wa upinzani na zaidi chuki inayoweza kujengeka, watataka muwepo Bungeni walau kwa uchache na hapa viongozi wa juu wa vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kujikuta katika mtihani wa kukubali ubunge wa kuteuliwa na hata kupewa vyeo serikalini.
Kwahiyo, Kamati Kuu ya CHADEMA, mkikaa myatafari haya yote na mengine ambayo sijayataja hapa kabla ya kufikiri kukubali kuteua wabunge wa vitu maalumu kuingia katika hili Bunge kwani mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana la kisiasa kwa kukubali kuwa sehemu ya hili Bunge ambalo uhalali wake ni wa kuhojiwa.
Agenda kuu inapaswa kuwa ni kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi na si kufikiria kuteua wabunge wa vitu maalumu kwenda katika hili Bunge.
Wapinzani, kama kweli mnataka kushika dola, basi lazima muwe tayari ku-sacrifice baadhi ya mambo vinginevyo msahau kuingia Ikulu.
No easy walk to freedom.