Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Hiyo ya utayari wa kuchangia chama ni uongo. Mtajitahidi hapo mwanzo lakini ikiaikainen miezi miwili mtaacha kuchangia kwa kusingizia hamna imani na chama cha wachaga. Hamna nia njema na Chadema.

Amandla...
 
Wala hawakustahili kujiuliza. Jibu liko wazi. Haramu ni haramu tu. Waamue - wawe chama chenye msimamo ama ruzuku. Chaguo ni lao.
 
Wakawatete wananchi waliogoma kuyatetea maslahi yao? Wakatetee Maiti?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Watanzania siyo watu wa kuwapigania, muulize Mange Kimambi hana hamu nao kabisa....
 
Kura zipi wakati wamesema wameibiwa kura zao? Huwezi kusema umekamata kura feki halafu urudi tena useme nina kura halali za urais hivyo ni haki yangu kupata viti maalum. Yaani nyama ya nguruwe haramu lakini mchuzi wa hiyo nyama halali.
Kura halali zilizopigwa na walioipigia chadema, au unataka zipi?
Pitia vizuri ulichoandika.
 
Miaka mitano mmejiapiza kuwa Chadema itakufa itakufa sasa majuzi mmejionea kwenye mikutano ya Lissu. Msichoelewa ni kufikiri kwamba CHADEMA ni viongozi kumbe ni wananchi.
Nani aliyejiapiza? Hili ni jukwaa huru na si kila anayechangia anafanya reference kwa mavyama yenu hayo mnayo hangaika nayo usiku na mchana
 
Hivi si inawezekana viti maalum wakarudishwa wale wakongwe mfano mdee ,ester wote pamoja na wakina sugu,Heche plus kamanda mbowe?

Sema hivo vijembe vya spika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
That is not an offer , ni haki yao ya kikatiba , labda waamue kuiacha tu kwa sababu ya mikakati ya kisiasa , lakini hawajapewa na mtu , hii imepatikana kutokana na idadi ya kura za mgombea wao wa Urais
Kumbe huwa mnafuata katiba kama mnapata mnuso? Si kila siku mnalialia kwamba katiba ibadilishwe? Leo katiba imekuwa nzuri? Kweli wajinga huwa hawaishi.
 
Ruzuku sasa iondolewe kabisa kwa vyama vyote. Naona inawachanganya watu wasiweze kufanya maamzi sahihi kwa manufaa mapana ya Tanzania.
 
Marekani kuna kitu kinaitwa gerrymandering. Chama kilichopo madarakani kwenye majimbo wakati wa kuhesabu watu, kina mamlaka ya kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi. Republicans wametumia haki hiyo kuweka mipaka ambayo inawawezesha kushinda hata kama wanapata kura pungufu kuliko Democrats. Kila walipoweza, wameweka vikwazo ambavyo vimewalenga wasio weupe na vijana kupiga kura. Kwenye uchaguzi wa gavana wa jimbo la Georgia mwaka 2018 Secretary of State wake ( aliyekuwa pia mgombeaji) aliondoa majina ya wapiga kura zaidi ya 300000 kwenye orodha ya wapiga kura wengi wao wakiwa weusi. Baada ya kufanya haya na mengine mengi ya kuwadhulumu haki zao wapiga kura wa Georgia alishinda kwa takriban kura 50000. Democrats wa Georgia hawakususa kuingia bungeni kwa sababu wameibiwa! La hasha, waliingia bungeni wakati wale ambao walikuwa nje ya bunge walifanya kampeni kubwa ya kuandikisha wapiga kura wapya. Hao ndio waliompa Biden ushindi Georgia.

Amandla...
 
Sisi wananchi tumeona kila kitu kilichofanywa kwenye uchaguzi huu , kwahiyo basi Chadema msisubutu kabisa kuteua wabunge wa viti maalum ,hata wakiwapa msikubali , hao wabunge watawasaidia nini ? Pili huyo Aidah Kenan aliyepewa ubunge wa kuokotwa barabarani afukuzwe CDM mara moja , anajidai eti wananchi wamemtaka aende bungeni muongo mkubwa hivi unafikiri hii hali ya uonezi , uuaji na mateso watu wa Nkasi wameifurahia ? Hawakuiona nchi nzima ? Hata kama yeye ataenda huko bungeni ataenda kubadili kipi? Ataleta tija ipi? Huyo afukuzwe mara moja akajiunge na akina Silinde wabunge wa viti maalum vya Ndugai .Yaani huyo Kenan aende bungeni huko peke yake huku wenzake wameumizwa , wamedhulumiwa ushindi , wameporwa , wamefungwa , wamo ndani mpaka sasa hivi , halafu yeye anataka aende akakae kiti na meza moja na watesi wa wenzake? Blood foolish .
 
Kura zipi wakati wamesema wameibiwa kura zao? Huwezi kusema umekamata kura feki halafu urudi tena useme nina kura halali za urais hivyo ni haki yangu kupata viti maalum. Yaani nyama ya nguruwe haramu lakini mchuzi wa hiyo nyama halali.
nje ya mada
 
Kama wanataka tuwaone wajinga wa kutupa wakubali viti maalum .Watakuwa wamefanya ujinga wa hali ya juu sana , Yaani wasithubutu kufanya hivyo basi sisi wananchi tutakuwa hatuna imani nao tena , unaenda kukaa meza moja na muuaji , mporaji , dhulumati ? Aliyekupora ushindi hadharani .Watumieakili .Na mimi niliwaambia vyama vyote humu mwaka jana , wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wasishiriki uchaguzi huo maana watakuwa wanahalalisha uchaguzi haramu kuwa halali , niliandika thread tano ,unaweza kureview hawakusikia .Sasa ndio kama wana akili watajifunza kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya .Wawaache CCM waweke viti vyao maalum mbonawdna watu wengi tu .Kuna Alhad Musa Salim na kamati yake ya amani , kadinari Pengo , Wagombea uchwara wa urais ambao hawskupata kura hata mia , kina Queen Sendiga , Wana wake zao , watoto wao wawape hao .
 
That is not an offer , ni haki yao ya kikatiba , labda waamue kuiacha tu kwa sababu ya mikakati ya kisiasa , lakini hawajapewa na mtu , hii imepatikana kutokana na idadi ya kura za mgombea wao wa Urais
wamepata wabunge wangapi
 
Wasuse ili chama chenyewe kijifie natural death tuelekeze nguvu na mawazo yetu kwenye kujenga chama kingine cha upinzani
 
Wajitafakari, je wao ni chama cha siasa au kikundi cha wanaharakati?

Chama cha siasa lengo lake ni kupata fursa ya kuunda serikali. Kwahiyo kuwa Bungeni ni muhimu sana katika kufikia lengo hilo. Chama cha siasa au mwanasiasa hutegemewa kuwa flexible kutegemeana na hali halisi ya wakati husika ili aweze kutimiza lengo lake.

Kikundi cha uanaharakati kinakuwa na agenda moja au chache kinachozipigania. Hakiwezi kukubali kubadilisha msimamo kwenye masuala yoyote yanayoingiliana na agenda hiyo.

Kwahiyo mwanasiasa hujifunza mazingira yalivyo na kutafuta mafanikio bila kulazimika kubadili mazingira. Mwanaharakati hutumia nguvu na maarifa yake yote kubadili mazingira ili agenda yake itimie.

Kama Chadema ni chama cha siasa, hakiwezi kususia Bunge.
 
Umeandika pumba tuu hapa, linganisha sasa na wizi wa kura wa wazi kabisa kwamba kuumiza na kuuwa watu, wakurugenzi kukimbia ofisini nk hayo huko Marekani yapo?? Acha kulinganisha mbingu na ardhi jombaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…