CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 490
- 2,471
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imekutana leo Ijumaa, Juni 26, 2020, Jijini Dar Es Salaam katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2019, ibara ya 7.7.15, ambapo pamoja na masuala mengine, imejadili ajenda zifuatazo;
1. Mchakato wa Uteuzi wa Wagombea wa Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani
2. Taarifa ya Fedha na Bajeti
3. Maandalizi ya Ilani za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 (ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar).
Kikao hicho cha siku moja, kimekutana jijini Dar es Salaam chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohamed.
Taarifa kuhusu maazimio ya kikao hicho zitatolewa kwa umma kupitia kwa waandishi wa habari wakati muafaka.
Imetolewa leo Ijumaa, Juni 26, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema