Wakitoka hapo wanakwambia corona haijapungua watu kibao bado wanakufa lakin nao wamevua masks kama sie wa hovyo hovyo
Mbwembwe za kukutana ki teknolojia zimeishia wapi tena!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbwembwe za kukutana ki teknolojia zimeishia wapi tena!?
Hahahhaha... Zile zilikuwa kiki tu, na vile vi computer vyao vya mtumbaKweli Corona imekwisha chadema hawakutani tena kiteknolojia hahaahaha
Halafu hapo kwenye pesa hapo ni hatari sana
Siku moja tu baada ya Lisu kutumia masaa 4 akiwahutubia watanzania na kuwapa sababu za kwa nini anatangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania, huku nyuma Mbowe akaibuka na igizo la kuvamiwa na watu wasiojulikana, kisha kukanyagwa kanyagwa na kuvunjwa mguu wa kulia bila mtoto wake James aliyekuwa ndani kusikia chochote ,badala yake akasikia Joyce Mkuya aliyekuwa umbali wa kilomita
5!!
Lengo la hili igizo ilikuwa ni kufunika habari ya Lisu kuandikwa na vyombo vya habari.
Kana kwamba haitoshi Mbowe baada tu ya kuruhusiwa kutoka hospitali ,huku akichechemea akatangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania!
Yani watanzania wakiwa na hamu ya kusikia report kutoka kwa Mbowe mwenyewe kwamba alivamiwaje, ilikuwaje ,badala ya kujibu hizo hoja ,yeye akaja na igizo jingine la kwamba kuna wazee wameenda nyumbani kwake kumshawishi awanie urais wa Tanzania!!.
Hivi Lisu unataka ufanyiwe nini ndiyo ujue kwa sasa hauhitajiki Chadema?
Haya maigizo ya mwenyekiti wako wa chama kufunika utangazaji wako nia hayajakuamsha tu?.
Shituka
[/QUOTE
Etwege unaona Mbowe ni mjinga sana, asingizie kukanyagwa!!
Mbona mnashupalia kukanyagwa hadi bungeni spika anafunika kuwa Mbowe ni mlevi!!
Kazi yenu kuuwa watu hata Lissu mlisema Mbowe kampiga risasi, wala hamkuangaika kutafuta wauwaji, mlijitahidi kufunika kama ilivyo kawaida yenu!!
Mnamwogopa saana Tundu Lissu, mnafanya kila hila ili kumtisha na kumkatisha tamaa!!
Lissu anakuja kaa tayari ufalme wenu tuub omoe sasa!!
TUNDU LISSU FOR PRESIDENCE 2020!!
Ya ccm imetoka lini ?Kila a kheri, Hadi Leo Ilani ya Chama bado?
Hapa hata mm nimetilia mashakaKila a kheri, Hadi Leo Ilani ya Chama bado?
Nimeipenda hiyo sehemu ya mwanzo ya bandiko lako, "Tudai tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi."
Lakini kwa sababu zisizofahamika, CHADEMA na wapinzani wenzao hata hili hawakulifanyia kazi hadi wakati huu, ambapo ni kama limepitwa na wakati kulifanikisha kabla ya uchaguzi. Sasa sijui kama mipango yao ni kulihimiza wakati wa kampeni? Sidhani.
Kwa hiyo hili limepitwa na wakati; lakini dalili zote bado zinaonyesha CHADEMA wanajiandaa kushiriki kwenye uchaguzi bila ya kuwepo na tume huru!
Je, wanayo mipango gani kuhakikisha kura zao zinalindwa, zinahesabika, na wagombea wao wanapata haki? Hili hawalielezi kama lipo.
Na kama halipo, wanashiriki kwenye uchaguzi kwa matumaini gani? Hili sijui kabisa.
Pamoja na hayo yote, binafsi ningewashauri watumie muda wao wa kampeni kuhimiza wapiga kura wajitokeze kwa wingi sana, kuliko ilivyowahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu.
Wapiga kura wapige kura zao jinsi wanavyoona wao wenyewe inafaa. Kama wanampa Magufuli kura zao zote bila ya shurti, sawa. Kama wapiga kura wataamua kumnyima kura Magufuli na kuwapigia wapinzani, nami nitakuwa mmojawapo katika kundi hilo.
Na baada ya kufanya hivyo, wacha Magufuli na vyombo vyake aziharibu hizo kura zetu zilizomkataa na ajipe ushindi wa lazima, kuliko kumpa ushindi bila ya kujitokeza na kupiga kura.
Kama CHADEMA watakuwa na mikakati ya kuzilinda hizo kura zetu kwa udi na ubani, tutawaunga mkono kwa kuwasikiliza wanataka tufanye nini ili kura zetu zisiharibike.
Ushahidi wa wingi wa kura zetu ndiyo itakayokuwa nguzo kuu ya kumpinga Magufuli, na sio kura ambazo hazipo kwa vile tuligoma kwenda kupiga kura na kumpa ushindi wa chee, kama ule wa serikali za mitaa.
Hapa hata mm nimetilia mashaka
Mmewezaje kuikwepa intelijensia ya polisi? Kwa hilo huenda mkatakiwa kukabidhi nyaraka za mkutano.CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imekutana leo Ijumaa, Juni 26, 2020, Jijini Dar Es Salaam katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2019, ibara ya 7.7.15, ambapo pamoja na masuala mengine, imejadili ajenda zifuatazo;
1. Mchakato wa Uteuzi wa Wagombea wa Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani
2. Taarifa ya Fedha na Bajeti
3. Maandalizi ya Ilani za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 (ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar).
Kikao hicho cha siku moja, kimekutana jijini Dar es Salaam chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohamed.
Taarifa kuhusu maazimio ya kikao hicho zitatolewa kwa umma kupitia kwa waandishi wa habari wakati muafaka.
Imetolewa leo Ijumaa, Juni 26, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Mfano Jeche wa Zanzibar alikuwa na mahaba na CCM si unaona anachofanya sasa, ati na yeye anagombea urais Zanzibar kupitia CCM. Mtu aliekuwa kiongozi wa Tume ya uchaguzi!Tume huru haiwezi kuchaguliwa na mmoja wa washiriki wa uchaguzi. Tumeona kwa macho yetu tume ikiwa watiifu kwa chama cha mteule wa tume. Hapa tulipofikia hatuna uadilifu tena wa kumuamini kiongozi wa chama kishiriki, kuwa mteuzi wa viongozi wa tume.
Umenena vema. Ni kazi bure kushiriki uchaguzi wala kupiga kura chini ya tume hii.Tudai tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi. Wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kujitokeza kupiga kura, chini ya tume inayoonyesha kuwa inafuata maelekezo ya chama tawala bila kificho.
Eeenh, basi SAWA. CCM na iendelee!Kushiriki uchaguzi huu bila tume huru ya uchaguzi inaweza kuwa uamuzi mzuri kwa cdm, lakini sio uamuzi sahihi. Mimi bado msimamo wangu uko palepale, siwezi kwenda kupiga kura bila kuwa na tume huru uchaguzi maana ni kupoteza muda.