Uchaguzi 2020 Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana kujadili Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana kujadili Uchaguzi Mkuu 2020

Mlikutana kwa njia ya video? Kama siyo je, corona imeisha?
 
Tume huru haiwezi kuchaguliwa na mmoja wa washiriki wa uchaguzi. Tumeona kwa macho yetu tume ikiwa watiifu kwa chama cha mteule wa tume. Hapa tulipofikia hatuna uadilifu tena wa kumuamini kiongozi wa chama kishiriki, kuwa mteuzi wa viongozi wa tume.
Kwa kuwa washiriki wanateuliwa na mmoja wa washiriki ni kigezo cha wao kutokutimiza wajibu? Kwa maana hiyo Watendaji wote wa Serikali ni wanachama au wafuasi wa Chama Tawala au waoga ams hawajitambui kiasi cha kutotimiza wajibu wao.

Hayo ni matusi ya nguoni dhidi ya watendaji na utetezi wa kishamba na utoto, kwa upande wako.
 
Hapo namba 2 mwambieni na dj faru john atoe maelezo yanayoeleweka
 
Kwa kuwa washiriki wanateuliwa na mmoja wa washiriki ni kigezo cha wao kutokutimiza wajibu? Kwa maana hiyo Watendaji wote wa Serikali ni wanachama au wafuasi wa Chama Tawala au waoga ams hawajitambui kiasi cha kutotimiza wajibu wao.

Hayo ni matusi ya nguoni dhidi ya watendaji na utetezi wa kishamba na utoto, kwa upande wako.

Sina chembe ya shaka ya nilichokisema. Na kile kinachofanyika huwa tunakuona kwa macho wala hatuhadithiwi. Hata uje na jazba vipi utaishia tu kutapika hirizi, lakini ukweli uko wazi.
 
Tunajua kabisa hamuwez ingia kwenye uchaguz sababu hela za kampeni mmekula ivyo tume huru ni kichaka tu
 
Tudai tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi. Wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kujitokeza kupiga kura, chini ya tume inayoonyesha kuwa inafuata maelekezo ya chama tawala bila kificho.
Nimeipenda hiyo sehemu ya mwanzo ya bandiko lako, "Tudai tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi."

Lakini kwa sababu zisizofahamika, CHADEMA na wapinzani wenzao hata hili hawakulifanyia kazi hadi wakati huu, ambapo ni kama limepitwa na wakati kulifanikisha kabla ya uchaguzi. Sasa sijui kama mipango yao ni kulihimiza wakati wa kampeni? Sidhani.

Kwa hiyo hili limepitwa na wakati; lakini dalili zote bado zinaonyesha CHADEMA wanajiandaa kushiriki kwenye uchaguzi bila ya kuwepo na tume huru!

Je, wanayo mipango gani kuhakikisha kura zao zinalindwa, zinahesabika, na wagombea wao wanapata haki? Hili hawalielezi kama lipo.

Na kama halipo, wanashiriki kwenye uchaguzi kwa matumaini gani? Hili sijui kabisa.

Pamoja na hayo yote, binafsi ningewashauri watumie muda wao wa kampeni kuhimiza wapiga kura wajitokeze kwa wingi sana, kuliko ilivyowahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu.
Wapiga kura wapige kura zao jinsi wanavyoona wao wenyewe inafaa. Kama wanampa Magufuli kura zao zote bila ya shurti, sawa. Kama wapiga kura wataamua kumnyima kura Magufuli na kuwapigia wapinzani, nami nitakuwa mmojawapo katika kundi hilo.

Na baada ya kufanya hivyo, wacha Magufuli na vyombo vyake aziharibu hizo kura zetu zilizomkataa na ajipe ushindi wa lazima, kuliko kumpa ushindi bila ya kujitokeza na kupiga kura.

Kama CHADEMA watakuwa na mikakati ya kuzilinda hizo kura zetu kwa udi na ubani, tutawaunga mkono kwa kuwasikiliza wanataka tufanye nini ili kura zetu zisiharibike.
Ushahidi wa wingi wa kura zetu ndiyo itakayokuwa nguzo kuu ya kumpinga Magufuli, na sio kura ambazo hazipo kwa vile tuligoma kwenda kupiga kura na kumpa ushindi wa chee, kama ule wa serikali za mitaa.
 
Kamati Kuu kujadili agenda kubwa tatu na muhimu kiasi hiki kwa siku moja ni jambo la ajabu sana! Kamati Kuu imekuwa rubber stamp!
 
Tume huru haiwezi kuchaguliwa na mmoja wa washiriki wa uchaguzi. Tumeona kwa macho yetu tume ikiwa watiifu kwa chama cha mteule wa tume. Hapa tulipofikia hatuna uadilifu tena wa kumuamini kiongozi wa chama kishiriki, kuwa mteuzi wa viongozi wa tume.
Tume ni mali ya yesu wa checheme na malaika zake in lucifer makonda na wenzake.
 
Kamati Kuu kujadili agenda kubwa tatu na muhimu kiasi hiki kwa siku moja ni jambo la ajabu sana! Kamati Kuu imekuwa rubber stamp!
Kwa akili kiduchu utayaona makubwa, kwa akili kubwa kama CDM, these are simple issues!
 
Back
Top Bottom