Tudai tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi. Wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kujitokeza kupiga kura, chini ya tume inayoonyesha kuwa inafuata maelekezo ya chama tawala bila kificho.
Nimeipenda hiyo sehemu ya mwanzo ya bandiko lako, "Tudai tume huru ya uchaguzi,
hakuna uchaguzi bila kuwa na tume huru uchaguzi."
Lakini kwa sababu zisizofahamika, CHADEMA na wapinzani wenzao hata hili hawakulifanyia kazi hadi wakati huu, ambapo ni kama limepitwa na wakati kulifanikisha kabla ya uchaguzi. Sasa sijui kama mipango yao ni kulihimiza wakati wa kampeni? Sidhani.
Kwa hiyo hili limepitwa na wakati; lakini dalili zote bado zinaonyesha CHADEMA wanajiandaa kushiriki kwenye uchaguzi bila ya kuwepo na tume huru!
Je, wanayo mipango gani kuhakikisha kura zao zinalindwa, zinahesabika, na wagombea wao wanapata haki? Hili hawalielezi kama lipo.
Na kama halipo, wanashiriki kwenye uchaguzi kwa matumaini gani? Hili sijui kabisa.
Pamoja na hayo yote, binafsi ningewashauri watumie muda wao wa kampeni kuhimiza wapiga kura wajitokeze kwa wingi sana, kuliko ilivyowahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu.
Wapiga kura wapige kura zao jinsi wanavyoona wao wenyewe inafaa. Kama wanampa Magufuli kura zao zote bila ya shurti, sawa. Kama wapiga kura wataamua kumnyima kura Magufuli na kuwapigia wapinzani, nami nitakuwa mmojawapo katika kundi hilo.
Na baada ya kufanya hivyo, wacha Magufuli na vyombo vyake aziharibu hizo kura zetu zilizomkataa na ajipe ushindi wa lazima, kuliko kumpa ushindi bila ya kujitokeza na kupiga kura.
Kama CHADEMA watakuwa na mikakati ya kuzilinda hizo kura zetu kwa udi na ubani, tutawaunga mkono kwa kuwasikiliza wanataka tufanye nini ili kura zetu zisiharibike.
Ushahidi wa wingi wa kura zetu ndiyo itakayokuwa nguzo kuu ya kumpinga Magufuli, na sio kura ambazo hazipo kwa vile tuligoma kwenda kupiga kura na kumpa ushindi wa chee, kama ule wa serikali za mitaa.