Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Napata moyo tu kwa kuwa Mh. Mbowe yumo katika hiyo kamati na tayari keshaeleza tokea awali kuwa laki tatu zinatosha sana. Sina wasiwasi kuwa kiwango cha posho kitabakia kama kilivyo au kitapungua. Sina kawaida ya kumsifia mbowe lakini kwa hili amekuwa mkweli na mzalendo. Tutegemee sana kuwa wabunge posho watafedheheka.
 
Mwenyekiti wa muda wa ‪Bunge La Katiba ‬ameunda kamati ndogo ya wajumbe 6 kuchunguza suala la malalamiko ya posho juu ya bunge hilo la katiba.
Wajumbe wanaounda kamati ya kuchunguza posho ni Lukuvi, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Mohamed Aboud, Asha Makame na Jenista mhagama.
Kwa taarifa ya nyongeza ni kwamba wanataka iPad siyo masuala ya makaratasi.
 
Yanawaza kwenda kula nyama mnadani na kutafuta dada poa
 
Hili bunge la kihuni na hovyo hovyo livunjwe ,mchakato wa uteuzi uanze upya kwa njia nyingine.
 
Hapo nafika mahali najiuliza je ni muhimu kuwa na bunge,je bila bunge nchi haiwezi kuendelea,je bunge lina mamlaka kamili kama mhimili unaojitosheleza.
Tuna wabunge wakuchaguliwa gharama za kumsimamisha mgombea ni kubwa sana,huyo akisha chaguliwa nakuingia mjengoni anatafuta jinsi yakurudisha hela alizotumia kwenye kampeni kwa maana hiyo wamejirundikia marupurupu kibao kufidia hizo gharama,na wakimaliza miaka mitano wamejiandalia mafao makubwa kwa ajili ya kuwawezesha kupambana tena kwenye uchaguzi unaofata.
Inasemekana mbunge mpaka anamaliza kipindi cha miaka mitano anakuwa amejikusanyia takriban milioni 500,ukiangalia idadi ya wabunge tuliokuwa nao hizo hela zote wanazojilimbikizia kama wasingekuwepo,pamoja na za kampeni za vyama vyao zikaelekezwa kwenye majimbo yao nadhani zingeleta maendeleo chanya kwa wananchi badala ya kuwanufaisha wao na familia zao tu.
Kwa mfumo tulionao bunge ni kama sehemu ya serikali badala ya kuisimamia serikali kinyume chake ni watetezi wa serikali.
Fikiria shs bilioni 8 na ushee zimetumika kukarabati jengo la bunge,Kashilila alikuwa analipwa posho ya shs 1.5 millioni kutwa kwa kazi ya kufuatilia ukarabati huo.
Kwa chombo ambacho hakina ubavu wa kunyooshea serikali kidole hata pale inapovurunda hakina uhalali wakuwepo kuwanyonya wananchi ambao wanapashwa kuwatetea na kuona maisha yao yanaboreshwa.
 
Mwenyekiti wa muda wa ‪Bunge La Katiba ‬ameunda kamati ndogo ya wajumbe 6 kuchunguza suala la malalamiko ya posho juu ya bunge hilo la katiba.
Wajumbe wanaounda kamati ya kuchunguza posho ni Lukuvi, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Mohamed Aboud, Asha Makame na Jenista mhagama.
Wameanza na posho watamaliza na posho. Wanasiasa lao moja tu, ULAJI. Eti shs 300,000 (alfu mia tatu) posho kwa siku haitoshi! Kweli wanasiasa nchini ni kama mchwa. Mnaweza kuona kwa nini wanasiasa calibre ya zzk hawana nafasi kila upande.
 
Mbunge yeyoye mwenye akili asingekubali kuteuliwa kuingia kwenye hiyo kamati!

Mbowe maadam umeingia kwenye hiyo kamati,we pia utakuwa sehemu ya maamuzi yatakayofikiwa.

Nini ambacho hakieleweki hapo mpaka kamati iuendwe?!

Swala la sh 300,000 kwa siku kuwa ni anasa halina ubishi!

Mbowe hakupaswa kukubali huo uteuzi!

Leo wakisema CHADEMA mmeshiriki Mbowe utapinga vipi kauli hiyo?!

Wanasiasa kwenye hela ni wanafiki sana!
 
Kamati ndogo ya walimu pia iundwe kuchunguza malalamiko ya walimu juu ya mishahara midogo na kuminywa marupurupu yao...
Pia kamati ndogo ya askari iundwe kuchunguza malalamiko ya askari kuhusu mishahara midogo

mbona wanapoteza muda maana hizo posho sio kama ni tatizo sisi tunachotaka waanze kufanya kazi ya kututengenezea katiba mpya.

kumbe hawa ni wachumia tumbo,hakuna katiba hapa.CCM ni janga

Kusanyiko la wahuni wa posho

Hiyo kamati ichunguze na posho za kada zingine, maccm yanawaza posho tu
Wamejitolea kwa nia njema kabisa ya kuhakikisha katiba mpya inapatikana lakini ajabu wamepewa posho ya laki 3 ambayo inawawezesha kukaa Dodoma vizuri bila shida ajabu wanakuja na ajenda ya posho haitoshi, hapa dhana ya kujitolea hakuna kabisa, wajumbe wengine pia ni wepesi mno maana niliangalia wakati imetolewa hoja ya kuzidi kwa kura, mjumbe mmoja mwanadada akatoa hoja nyepesi "tusirudie uchaguzi tuchukue hizo kura zilizozidi tuwagawanishe wagombea"(nilivyoona kauli kama hii imetoka kwa mjumbe nikasema tumeliwa maana mtu kama huyu sidhani kama atakuwa na upeo mkubwa wa kuangalia mambo mazito ndani ya katiba alafu leo tena wanakuja na hoja ya posho haitoshi
 
Si mlikuwa humu ndani mnamuona Zito ni msaliti sa sa bora mliwe ndo mkome jk ongeza wape 1.5 kama ya kashilililah
 
Nasikia kuna wabunge wa Zanzibar wanalipwa 420,000 @ siku badala ya laki tatu wanazolipwa wabunge wanaotoka bara!Na hii ni moja ya sababu ya kuundwa kamati hiyo.Mimi najiuliza,iwapo Dodoma maisha ni magumu ya kuhitaji zaidi ya laki 3 kwa siku,vipi wanafunzi wa vyuo kama Udom,st Johns nk wanaolipwa 7500/= tu kwa siku? Ama inakuwaje watumishi wengine wa serikali wanalipwa 65,000 kama perdiem wakiwa hapo Dodoma?Watumishi wa Bunge ambao wanaishi Dodoma eti nao wanalipwa perdiem wakati hawatofautiani na watumishi wengine wa serikali wanaoishi Dodoma na wakifanya kazi masaa ya ziada wanalipwa extra duty allowance ambayo haizidi elfu 30,000 kwa siku.Watu wanaoipenda hii ccm na wana mioyo gani?ama wanafaidika na ujinga huu tunaolalamikia?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ikija tu habari ya pesa Mbowe habaki nyuma, huyu kiongozi tumbo kweli kweli.
 
Hivi katiba si ya watanzania wote? Sasa kama wameanza hivi mambo ya posho. Ni kwamba posho isipoongezwa hiyo katiba itakuwa bora liende?
Posho ya laki 3 inatosha kwa siku, kuna watu wanaipata hiyo kwa mwezi na hawalalamiki.
Ifike sasa watanzania tuamke, tuseme imetosha asiyetaka hiyo arudi kwake.
 
Wajumbe wengi wanatoka CCM, Hawa kwao dili sio katiba. Dili kwao ni posho na kutetea upuuzi uingizwe kwenye katiba. Hakuna lingine.
 
Kamati tena...kweli posho ni janga la taifa..sasa kamati ya nini...wafanye kazi huko!

Enzi za Mwalimu hiki kipande cha dunia kinachojulikana rasmi kama Tanganyika/Tanzania kilikuwa na sifa ya wananchi kutumia BONGO zao to make ends meet na hatimaye kikajulikana kwa jina la utani BONGOLAND. Hizi enzi za watawala mafisadi POSHO ndio imegeuka kuwa mtaji. Matokeo yake BONGOLAND imegeuka kuwa POSHOLAND!!
 
Back
Top Bottom