Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Muongo sana huyo,tushamzoe alikataa gari mwisho wa siku akalichukua,tapeli mkubwa huyo.
 
Kama ni kweli huo ndiyo msimamo wake basi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza, lakini sijui kama hii habari ina ukweli wowote!!!
 
Kama ni kweli huo ndiyo msimamo wake basi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza, lakini sijui kama hii habari ina ukweli wowote!!!

Mkuu subiri taarifa ya saa mbili, au magazeti ya kesho.
 
Awaambie na kina shibuda na lema wanaotaka ujira wa mwiha uongezwe.
 
dah! kichwa kinauma kila nikifikiria huu uhuni wanaoufanya hawa wajumbe.
 
Ivi rais mbona amekaa kimya juu ya hili? nakumbuka madaktari, waalimu na TUCTA walipogoma kudai nyongeza ya mishahara a
iwajibu mapema tu kuwa anayeona mshahara mdogo hana sababu ya kugoma bali aache kazi akatafute yenye mshahara mkubwa sasa hawa wateule wake anawaogopa ama inakuwaje?
 
Katba inaanza kujadiliwa lini jamani mwenye kiti wa muda tuu ameanza kuunda matume au ni bunge la tume na si katiba?
 
Nyambafu mnaosema lak 3 ni kidogo kwa cku wakati kuna walimu hata hyo hawafikish kwa mwez. Km vp jitoeni au nenden hostel za udom mkalale. Make hata mm nimeish dom najua nn mnawadanganya wananch
 
RAIS wa Zanzibar naye ana mamlaka kwenye nchi yake. Hivi unajua nani anaidhinisha malipo ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi?

Hapo ni kama nchi mbili zinakutana kujadili, hawa wakiwa na posho toka kwao na pia wanakuja kulamba za kwetu! Wazanzibar bwana Chao Chao Chetu Chao.

Sasa CCM wanaona hili sawa? Kwa muundo wa serikali tatu mambo yananyooka tu hakuna ujuha hapa mkuu.
 
Sasa CCM wanaona hili sawa? Kwa muundo wa serikali tatu mambo yananyooka tu hakuna ujuha hapa mkuu.

Mkuu serikali tatu hakuna kitu hapo. Muungano wa maana ni serikali moja tu basi vinginevyo kila munu ave na kwao.
 
Mkuu serikali tatu hakuna kitu hapo. Muungano wa maana ni serikali moja tu basi vinginevyo kila munu ave na kwao.
Historia inatukataza kuwa na serikali moja, hili hata mmoja wa waasisi wa muungano wao huu aliliona na mpaka anaondoka madarakani hakulitekeleza. Kwa kuwa tunataka kuimarisha muungano wa watu basi serikali tatu ndo mujarabu hapa mkuu. Vinginevo sasa ni wakati sahihi kwa kuchukua maamuzi sahihi dhidi ya wapora demokrasia.
 
Mkuu Zanzibar wanataka soveregnity yao na kwa serikali ta
tu hawawezi kuipata. Hata kama katiba yenye muundo wa serikali tatu bado kutakuwa na kero tena zitaongezeka. Tanganyika itakuwa na Bunge lake ambapo Wazanzibar hawataingia, Tanganyika itakuwa na serikali yake ambapo Wazanzibar hawataingiakama ilivyo sasa.

Hii kwao itakuwa kero.
 
Tusubiri tuone ila kitendo cha CCM kuwaamulia wananchi suala la katiba sasa iwe mwisho mkuu. Hawa wanataka nguvu ya umma itumike na machafuko yawepo ndio itakuwa faraja yao.
 
Posho hazitaongezwa, badala yake wamefanya marekebisho kidogo kwenye padiem na Sitting allowance.
Kamati imeona kwamba posho wanazopokea wajumbe wa bunge la katiba ya sh 300,000 ni kubwa kulinganisha na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hivyo kwa kuzingatia uhalisia wamefikia uamuzi kuwa Padiem badala ya kuwa 80,000 na Sitting allowance kuwa 220,000, sasa itakuwa hivi;

Sitting Allowance 70,000
Padiem itakuwa 230,000.

Ieleweke kuwa hakuna pendekezo lolote lililopelekwa kwa mh. rais, na hakuna itakayopelekwa kwa ajili ya mjadala wa posho.

Mwisho Mbowe amewaomba wabunge badala ya kujadili posho na kulipwa allowances, wajikite kwenye rasimu ya katiba ambayo kimsingi ndiyo imewaleta Dodoma.

Say no to Nyongeza ya Posho.

Habari hii kwa hisani ya mtu wa Tanganyika
 
Hiyo si ndio itakuwa tiketi ya watu kutoroka vikao ambao vinalipiwa sitting ya 70,000/=huku akiwa ana uhakika wa kuata per diem ya 230,000/=. Any way kama wamekubaliana hivyo sio mbaya sana, HATUTAKI NYONGEZA HATA YA SHILINGI MOJA
 
Mbona kama ni yale yale? Kuongeza Per Diem Allowance kutoka 80,000.00 hadi 230,000.00 bado ni wizi. Hebu ngoja nikokotoe hapa chini;

Sitting Allowance 70,000.00
Per Diem 230,000.00
Posho 300,000.00
JUMLA 600,000.00

Bado tunarudi kule kule tulikokukataa.
 
Back
Top Bottom