Kamati tendaji Yanga mtuambie, ni nini chanzo cha ukata unaoikumba Yanga?

Kamati tendaji Yanga mtuambie, ni nini chanzo cha ukata unaoikumba Yanga?

Wapige hesabu inapokea tsh ngapi za udhamini na gate collection inatumia kiasi gani kulipa wachezaji pamoja na benchi la ufundi, inalipa kiasi gani kwaajiri ya kambi pamoja na watendaji wa timu.

hesabu zipigwe kisha waangalie kimepungua kiasi na namna gani ya kukiongeza.

Kama kuna jini(deni) linakunywa pesa za Yanga muwaweke wazi washabiki na wanachama wa Club sio kuficha ficha Vyura nyie.
Japo umeandika kipinzani ila umeandiaka iliyo hakika. Yanga lazima irudi kwa wanachama na mashabiki. Bila umoja na hamasa mashabiki mengi watakwepa kwenda uwanjani hivyo timu haitapata mapato.
 
Naunga mkono hoja, ni aibu kiongozi kuendelea kujamba kwenye kiti cha ofisi wkt huna mpango wowote wa maendeleo. Kuliko kulalamika kila siku hebu achia nafasi mawazo mapya yaingie.
 
hizi timu zetu kila zinapofika kwenye hatua nzuri za mashindano ya kimataifa basi matatizo ndani ya timu yanaongezeka..bado najiuliza ni nani aliye turoga????? kama yupo tumtafute jamani na kama kafa tuonyeshwe kaburi lake !!!!!
Soka letu lina mambo ya hovyo sana! Viongozi wa vilabu wanaona kama vilabu ni mali yao. Hawajali maslahi ya wachezaji wala walimu. Ndo maana siwaonei huruma wanavyopandisha ngazi za mahakama ya kisutu.
 
Yanga ni timu ya jalalani tu, pesa mpaka wafadhali....Yanga kama timu haina hela na haina tofauti na timu zingine za ligi yetu isipokuwa baba yao Azam tu.
Yanga haijawahi kutafuta wafadhili ila wafadhili ndo walikuwa wanaifuata yanga. Wao ndiyo walikuwa wanaitumia yanga kupiga deal. Lakini kwa vile sasa deal hamna ndo maana huoni wadhamini tena. Pamoja na hayo ukweli unabaki kuwa yanga inaweza kujiendesha kwa faida bila kutegemea hao wadhamini.
 
Tatizo la Yanga ni uongozi. Viongozi wa Yanga siyo wasomi na wanachama wasomi wa Yanga wanaogopa kuiongoza. Majungu na ugomvi mwingi. Makundi ya kukaa getini (maninja) ndiyo yanayoamua nani awe kiongozi.
Bayern Munich wana Board of Directors yenye watu tisa.
Kuna mtu wa Adidas, Audi, Allianz na wanachama wana watu wao sita.
Yanga wauze angalau 30% stake ya club ili kuvutia investment na utaalam wa uongozi.
Hiyo kuuza stake ni malengo ya muda wa kati. Kwa hali ya sasa, nini kifanyike ili timu irudishe furaha na umoja kwa mashabiki wake?
 
Umegonga penyewe mkuu. Hapa ndio tatizo linaanzia
Inaelekea watiifu wa kanjibhai wanakuza matatizo ili waonyeshe kanjibhai ndo kila kitu yanga. Ndiyo maana tunahoji ili waweke wazi tatizo la timu. Na kama wanakuza matatizo hesabu zitawaumbua.
 
Umegonga penyewe mkuu. Hapa ndio tatizo linaanzia
Hizo ni propaganda za watu waliokuwa wanaitumia yanga kupiga deal. Ila ukweli ni Yanga imekuwepo kabla mbaazi hazijaanza kulimwa bongo.
 
Japo umeandika kipinzani ila umeandiaka iliyo hakika. Yanga lazima irudi kwa wanachama na mashabiki. Bila umoja na hamasa mashabiki mengi watakwepa kwenda uwanjani hivyo timu haitapata mapato.
Hivi nani aliyewadanganya mapato ya klabu ni viingilio pekee?
 
Naunga mkono hoja, ni aibu kiongozi kuendelea kujamba kwenye kiti cha ofisi wkt huna mpango wowote wa maendeleo. Kuliko kulalamika kila siku hebu achia nafasi mawazo mapya yaingie.
Hamna namna, itabidi tuwabane! Kama hawana uwezo wakautafute kupitia Njombe Mji ila siyo yanga.
 
Hivi nani aliyewadanganya mapato ya klabu ni viingilio pekee?
Mimi sijaongelea viingilio nimeongelea mapato. Kama hujui uwepo wa mashabiki uwanjani una multiplier effect kwenye mapato ya timu. Mosi ni viongilio, pili mauzo ya jezi, tatu matangazo ya ndani ya uwanja na hata haki za TV na wadhamini inategemea fans base ya timu. Fans base unaipima kwa muitikio wa hao mashabiki kwenda uwanjani. Hivyo kazi ya pili ya kiongozi wa timu baada ile ya kuhakikisha timu inaenda uwanjani ni ile kuhakikisha mashabiki wanaenda uwanjani kwa wingi.
 
Hiyo kuuza stake ni malengo ya muda wa kati. Kwa hali ya sasa, nini kifanyike ili timu irudishe furaha na umoja kwa mashabiki wake?
Kwa sasa hivi, timu imeshaharibika.
Hatuchukui VPL ila tunaweza kutengeneza kikosi kwa ajili ya confederation cup. Kikosi hicho ni lazima kiwe na wachezaji vijana, ambao siyo majeruhi.
Wanachama tutoe fedha kwa ajili ya mechi hizi za karibu, kwa mfano mechi na Rayon, tujiweke hali na mali tuchukue ushindi.
Ila, itabidi uongozi utujuze wanahitaji nini? Wasitufiche, watuambie kuna matatizo gani?
Kuhusu medium na long term goals, nina uhakika kuna mashirika na kampuni nyingi Tanzania ambazo zitataka kuingia ubia kuiendesha Yanga. Ni faida kwao. Mfano Halotel wanaweza kupata 10% ya Yanga kwa kutoa kiasi fulani (lets say 10bn) na kuwa na nafasi kwenye bodi ya watu kiasi fulani. Hii haihitaji muda mrefu, ni kwa sababu tu hatujui thamani ya hii klabu.
 
Yanga haijawahi kutafuta wafadhili ila wafadhili ndo walikuwa wanaifuata yanga. Wao ndiyo walikuwa wanaitumia yanga kupiga deal. Lakini kwa vile sasa deal hamna ndo maana huoni wadhamini tena. Pamoja na hayo ukweli unabaki kuwa yanga inaweza kujiendesha kwa faida bila kutegemea hao wadhamini.

Sasa kwanini kila mwaka wanasaka hela kama kweli wanaweza kujiendesha kama usemavyo?
 
Chanzo ni Mkemi, Frank Chacha na genge lao. Wanachama pia ni chanzo kwani wanawalea hao jamaa
 
Hizi klabu ni njia nzuri ya kudownload pesa bila jasho
 
Mimi sijaongelea viingilio nimeongelea mapato. Kama hujui uwepo wa mashabiki uwanjani una multiplier effect kwenye mapato ya timu. Mosi ni viongilio, pili mauzo ya jezi, tatu matangazo ya ndani ya uwanja na hata haki za TV na wadhamini inategemea fans base ya timu. Fans base unaipima kwa muitikio wa hao mashabiki kwenda uwanjani. Hivyo kazi ya pili ya kiongozi wa timu baada ile ya kuhakikisha timu inaenda uwanjani ni ile kuhakikisha mashabiki wanaenda uwanjani kwa wingi.
Kwa hiyo unataka kusema Yanga itapoteza hizo rights kwa mashabiki kutokwenda uwanjani? Na ni nani alyesema mauzo ya jezi ni uwanjani tu? Mtazamo huu ndio unayageuza matawi kiwa uwanja wa majungu na kupanga mapinduzi ya uongozi badala ya kuhamlea fans base hatakusudii waenda uwanjani pekee. Wengi zaodi hata hawafiki uwanjani.
 
Back
Top Bottom