Kamati ya Bunge itakayomuhoji Gwajima ijiandae kukutana na majibu yatakayowaacha wakiangaliana

Hapa naona Mr. Gwajiboy watambana kwa vipengele viwili

(1)Kutoa uthibitisho juu ya viongozi kuopokea rushwa ili kukubali chanjo.
Hapa watamkamata kwa kukosa uthibisho sababu issue ya rushwa ni ngumu sana kuithibitisha kati ya mtoaji na mpokeaji

(2)Viongozi kuchanjwa chanjo feki;
Hapa watamkamta sababu atathibitisha vipi kuwa mh. Rais alichanjwa chanjo feki kuwadanganya wananchi ili waikubali chanjo. Hii ina maana pale kwenye zile chonjo zilimotolewa kichupa ambacho rais alidungwa kilitegeshwa ili tuzuga wananchi. Hapa atathibitishaje sindano ya Rais ilikuwa feki!.

Kwa mtazamo wangu hapa naona kwenye hii kona hatawéza kuchomoka kirahisi.
 
Hakuna wa kujibu hoja za Askofu Gwajima. Hata wakikesha na madesa bado ni ngumu kusimama na mtu anayesimamia anachoamini.

Duh 🙄 nimebaki kinywa wazi “ Anayesimamia anachoamini” .Hapa tuma mzungu mzima Askofu Dr Rashid au Askofu Gwajima au Mheshimiwa Mbunge Gwajima au Mtumishi wa Mungu ambaye ni Mkubwa kuliko Rais,Waziri hata Mbunge.

Tafadhali nisaidie labda tunamzungumzia mwekezaji wa Train 🚊 ya umeme na jengo refuuu kuliko yote Tanzania.

Tafadhali nisaidie tunayemzungumzia ni nani !.
 
Kenya mahojiano kama haya yanakuwaga live

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Huyo rais wako hapingwi?
Mbona wao wanatumia nguvu kuhamasisha chanjo
Munashindwa kujibu hoja za gwajima mnaanza porojo na janja zenu.
 
Kauli za ndani ya Kanisa tafsiri yake ni tofauti na huko duniani.

Kupokea rushwa maana yake ni kutenda kama " kipofu"

Chanjo feki alimtaja yule afisa elimu wa Arusha, hilo la Rais wewe ndio unalianzisha hapa Jf
 
Kwa hiyo akipatwa na hatia adhabu yake inakuwa ni ipi!!?
 
Sidhani Kama itakuwa hivyo
 
Kesho Gwajima analazwa amini nakwambia
 
Whether Gwajima atashinda au atashindwa lkn huku nje taarifa itakayokuja Gwajima kaadhibiwa au kaambiwa aombe radhi hadharani.Hukumu tayari ipo
 
Baba Askofu Gwajima watamshugulikia vibaya sana,hawezi kushinda serikali yake mwenyewe.Vinginevyo kesho atangaze kujiuzuru uanachama wa CCM.Hiyo itampa fursa ya kutapika.
Aanze kutapika mambo ya Siri halafu wamuache salama? Labda itakuwa sio Tanzania
 
Maswali ya Gwajima au hoja ya Gwajima Ni za kipuuzi lkn nashangaa watu wanasema hazijibiki.Kesho atachanjwa mtu mbele yake halafu watasema aweka balbu iwake au aonyeshe usumaku.Kesho ataambiwa athibitishe rushwa aliyochukua Rais.Sioni Kama Gwajima atachomoka
 
Tupe uzoefu unavyoona Gwajima kesho anachomoka au hachomoki.Predict
 
Endeleeni kuongopeana. Unawezaje kulisukuma gari ukiwa ndani? Yani mbunge mmoja wa CCM aishinde CCM nzima? Tatizo hamna kumbukumbu.

Mmeshasahau ya Professor Assad. CCM wanao uwezo mkubwa sana, na hawana mpinzani linapokuja suala la kujitoa ufahamu!
Ushabiki unawasumbua watu
 
Sasa na wewe si unafanya upuuzi huohuo .. Ya nini uhamasishe kuchanja kama ni hiari !!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…