BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza amesema hayo leo Jumatano Septemba 21, 2022 wakati akiwasilisha uchambuzio wa taarifa za maazimio ya Bunge kuhusu sheria ndogo.
“Kamati ilibaini dosari ya kukinzana na masharti ya sheria inayotoa mamlaka ya kutungwa kwa sheria ndogo inayohusika na sheria nyingine za nchi imebainika katika sheria ndogo saba,”amesema.
Dosari nyingine walizobaini ni sheria hizo ndogo kutoendana na misingi ya uandishi wa sheria imebainika katika sheria ndogo nane, kuweka masharti yasiyo na uhalisia imebainika katika sheria ndogo sita na nyingine ya uandishi wa majedwali imebainika katika sheria ndogo tatu.
Amependekeza mamlaka ambazo hadi kufikia Machi, 2022 hazikuwa zimekamilisha hatua ya marekebisho ya sheria ndogo zilizoazimiwa na Bunge, zihakikishe zimekamilisha mchakato huo ifikapo Novemba 1, 2022.
Pia amependekeza mamlaka zinazohusika na sheria ndogo zilizowasilishwa bungeni wakati wa mkutano wa sita na wa saba wa Bunge na kubainika kuwa na dosari, zikamilishe mchakato wa marekebisho ya sheria ndogo ifikapo Desemba Mosi, 2022.