PreGE2025 Kamati ya bunge yakagua mradi wa nyumba NSSF mtoni kijichi, Kikwete asifu ustahimilivu NSSF

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
397
Reaction score
445
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wametembelea na kukagua Mradi wa Nyumba za Mtoni Kijichi awamu ya Tatu unaomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo Machi 16, 2025 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq amesema Kamati hiyo imeridhishwa na kupongeza uwekezaji huo wenye tija ambao utawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata makazi bora yaliyopo katika mradi huo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, amehimiza uwepo Zahanati, Maduka na maeneo ya michezo kwa ajili ya watoto katika eneo hilo ili wapangaji waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa karibu.

Awali akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema NSSF imeendelea kuwa stahimilivu kwa kusajili idadi kubwa ya Wafanyakazi kwenye sekta binafsi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema mradi wa Nyumba wa Mtoni Kijichi tayari umetoa makazi kwa familia 390 ambapo nyumba zimenunuliwa.

Pia, amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia familia 1,105 pindi nyumba zote zitakapo kamilika na kuuzwa, hivyo kuchangia katika kupunguza uhaba wa makazi kwa wakazi wa Dar es salaam.

FB_IMG_1742155291013.jpg
FB_IMG_1742155296006.jpg
FB_IMG_1742155299292.jpg
 
Attachments

  • FB_IMG_1742155305051.jpg
    FB_IMG_1742155305051.jpg
    60.8 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1742155309099.jpg
    FB_IMG_1742155309099.jpg
    78.1 KB · Views: 34
  • FB_IMG_1742155311954.jpg
    FB_IMG_1742155311954.jpg
    60.9 KB · Views: 32
  • FB_IMG_1742155320538.jpg
    FB_IMG_1742155320538.jpg
    110.3 KB · Views: 36
  • FB_IMG_1742155323811.jpg
    FB_IMG_1742155323811.jpg
    75.6 KB · Views: 32
  • FB_IMG_1742155327879.jpg
    FB_IMG_1742155327879.jpg
    69.7 KB · Views: 41
Hii haikubaliki kabisa yaani hajasiwa mtu hapo.hii ni feki news
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wametembelea na kukagua Mradi wa Nyumba za Mtoni Kijichi awamu ya Tatu unaomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo Machi 16, 2025 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq amesema Kamati hiyo imeridhishwa na kupongeza uwekezaji huo wenye tija ambao utawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata makazi bora yaliyopo katika mradi huo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, amehimiza uwepo Zahanati, Maduka na maeneo ya michezo kwa ajili ya watoto katika eneo hilo ili wapangaji waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa karibu.

Awali akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema NSSF imeendelea kuwa stahimilivu kwa kusajili idadi kubwa ya Wafanyakazi kwenye sekta binafsi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema mradi wa Nyumba wa Mtoni Kijichi tayari umetoa makazi kwa familia 390 ambapo nyumba zimenunuliwa.

Pia, amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia familia 1,105 pindi nyumba zote zitakapo kamilika na kuuzwa, hivyo kuchangia katika kupunguza uhaba wa makazi kwa wakazi wa Dar es salaam.

View attachment 3273201View attachment 3273202View attachment 3273203
Hivi nyumba zenyewe nizile zinazo ishi POPO. Mbona nikipita pale sioni,, i dalili kama wanaishi watu. Alafu lile eneo kama vile ni sehemu au karibu na bonde si kutakuwa na mazalia ya mbu sana, ila kwa muonekano wa nje nyumba zimepangiliwa vizuri sijui ndani. Ila kwanini sasa haziishi watu?
 
Wapande na miti ya vivuli sasa!
 
Hivi nyumba zenyewe nizile zinazo ishi POPO. Mbona nikipita pale sioni,, i dalili kama wanaishi watu. Alafu lile eneo kama vile ni sehemu au karibu na bonde si kutakuwa na mazalia ya mbu sana, ila kwa muonekano wa nje nyumba zimepangiliwa vizuri sijui ndani. Ila kwanini sasa haziishi watu?
Majumba yana miaka hayo wanaishi popo tu
Sio sahihi.kuchukua pesa za pension za watu.na kuwekeza kwenye mradi kama huo wa popo kulala

Nssf ni wahujumu uchumi pamoja na hiyo.kamati ya bunge
 
Tatizo Bei mzee.. Hizo bei wanazouza ni kwaajili ya viongozi wakubwa kwenye Idara za serikali...Mawinga wenzangu kumiliki hizi nyumba ni sawa na ndoto tu..
 
Changamoto ni BEI kua kubwa MNO!! Hz ni kutupa PESA za wachangiaji wa mfuko tu.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Tatizo Bei mzee.. Hizo bei wanazouza ni kwaajili ya viongozi wakubwa kwenye Idara za serikali...Mawinga wenzangu kumiliki hizi nyumba ni sawa na ndoto tu..
Duuu sasa si hasara hii kwasababu jinsi zinavyokaa mda mrefu bila watu zinachakaa na miundo mbinu inaharibika hata wizi unaweza kufanyika
 
Majumba yana miaka hayo wanaishi popo tu
Sio sahihi.kuchukua pesa za pension za watu.na kuwekeza kwenye mradi kama huo wa popo kulala

Nssf ni wahujumu uchumi pamoja na hiyo.kamati ya bunge
Halafu ukitaka kuchukua NSSF yako vikwazo vingi kumbe pesa zinajenga miradi ya nyumba za kuishi popo
 
Back
Top Bottom