Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi
Yule mzee alituona mazwazwa sana...

Kamati inasemaje kuhusu ule uwanja wa kimataifa wa Chato? Njiwa zinatua pale au tufanye uwanja wa ng'ombe kuotea jua wapate vitamin D kwa wingi?
 
Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi
Kamati ya Bunge la nchi gani! Kamati za Bunge hutokana na wabunge na ni wabunge haohao wanaosifu kwa asilimia mia wakati wa bajeti, leo kutuambia wameshituka ni kutufanya sisi mataahira.
 
Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi

Kwanini ATCL isipate hasara wakati zinatumika na Top three kama boda boda! Utasikia Rais yupo Rwanda na lile dege kubwa Dreamliner, Makamu yupo Burundi na Airbus, huku PM yupo kwao kusalimia kwa Bombardier. Nchi imepoteza dira kabisa.
 
Bado Samia anasema wameagiza ndege nyingine tano. Kwanini Ofisi ya rais watumie ndege ya ATCL wakati wakijua ndege hizo ni za biashara na wakiruka tu juu mamlaka za anga za kimataifa (ICAO na IATA) zinataka walipe? Kwanini wasitumie ndege ya rais ambayo ina some tax exemption pamoja na mambo ya kidiplomasia?
 
Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi
wao walifikaje bungeni?? walidhani wanafika hivi hivi bila kuchota pesa na kulipa mapololiccm na vyombo vingine? au ndio Nyani haoni.......
 
Bado Samia anasema wameagiza ndege nyingine tano. Kwanini Ofisi ya rais watumie ndege ya ATCL wakati wakijua ndege hizo ni za biashara na wakiruka tu juu mamlaka ya anga ya kimataifa inataka walipe? Kwanini wasitumie ndege ya rais?
Ndge zile zilishanunuliwa na mwendazake. Hawana pa kuzipeleka.
 
Bado samia anasema wameagiza ndege nyingine tano. Kwanini Ofisi ya rais watumie ndege ya ATCL wakati wakijua ndege hizo ni za biashara na wakiruka tu juu mamlaka ya anga ya kimataifa inataka walipe? Kwanini wasitumie ndege ya rais?

Acha watumie hizi hizi kwanza wansimamisha uchumi wao kwanza kama kipaumbele
 
Akili zitarudi tu. Hivi kuna shirika kama hilo hapa nchini? Kwa kuanzia halina ndege zake lenyewe kwani karibia zote ni za kukodi. Hivyo basi wanapaswa kwanza kuwalipa hao waliowakodisha hizo ndege.

Watoe na fedha za uendedhaji wa hizo shughuli zao ndiposa wabaki na faida! Mkodishaji anafaidika zaidi. Enzi zetu tukiuita uhusiano huu kuwa wa kinyonyaji. Unakaa tu nyumbani, Una majumba 10 mjini uliyoyapangisha na unavuta pesa kiulaini!
 
Back
Top Bottom