Kamati ya Bunge yatoa sababu ya kucheleweshwa kwa mradi wa Dege ECo Village wa Kigamboni

Hapo penye red palinitia moyo kweli. Nilidhani na mimi ninaweza kuwekeza kwenye miradi mikubwa kiasi hicho na nikawa na share kubwa tu. kumbe ilikuwa ni makosa ya uandishi. Kuweni makini mnapoandika.
 
Pole sana mkuu na hivi tunahamia Dodoma, things will never be the same again!! Biashara gani itafanyika pale tena? Nani atapanga pale na nchi ishahama? Sad!

Ni kweli kabisaaa kila kitu kimeharibika mkuu ila always nyumba za kupanga hazikosi wateja kabisaaa especially karibu na barabara ya Rami
 
Taarifa kumbukizi kuhusu mradi :

11 Dec 2014
Real Madrid Football Player Visit Dege Eco Village in Kigamboni area Dar es Salaam , Tanzania

Mradi huo mkubwa wa kijiji cha kisasa ulioanza mwaka 2013. Hali halisi katika video kama ulivyotembelewa na mwakilishi wa Real Madrid hapo December 2014 na uongozi wa NSSF kuelezea mipango yao kabambe kuvutia wadau mbalimbali kama timu hiyo kubwa ya soka nchini Spain. Mradi huo wenye nyumba elfu saba unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.

 
Habari kumbukizi mwaka 2017, mradi wa Dege Beach Eco Village wapigwa mnada

Yono Auction Mart madalali maarufu Tanzania watangaza mnada wa mradi mkubwa baada ya NSSF kuishiwa fedha na hivyo mradi kukwama kuendelea.

Dhima ya mnada huo ni kupata mwekezaji awe wa ndani au nje ya nchi ili kuwezesha mradi huo uweze kukamilika.

Mradi huo una thamani wa USD 350 milioni hivyo anatafutwa mwekezaji kutia kiasi hicho cha fedha ili ukamilishwe kupitia mnada huo.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutasaidia pia uchochezi wa kiuchumi ktk mradi huo na maeneo ya Kigamboni, Dar-es-Salaam.
 

Mbona mnashangaa PPP ya ajabu kati ya Jambazi na Serikali ya CCM anapewa ardhi Dege Beach bure kama shamba analipima na kugwa plots mara anakuwa strategic investor na NSSF wao watoe fedha Azimio atoe ardhi kwenye PPP ardhi is a sunken cost huwezi kuipa thamani kubwa kwa vile umiliki ni 66 years kwa estate na 99 year kwa shamba it doesn’t add any value to the project. Hiyo ardhi angepewa NSSF na huyo Mbia wao angetoa fedha kilichofanyika ni Wizi wa mchana.
Daraja la Kigamboni ni mradi bomu kwanza njia ya kutokea kwa upende wa Kigamboni haijakamilika hiyo speed limit ya 30km/ H ni tatizo hakuna mradi pale !
To add salt to the wound go back and review the ppp between Caspian na Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye miradi ya majengo ya Police , Oysterbay , Mikocheni na zile nyumba zaidi ya 300 nasikia Jiwe ana tafuta mbinu za kuvunja mkataba nyumba na kituo cha Police vimeshakilika tayari kukizindua hataki anazindua madaraja na kuzindua vibanda walivyojengewa Polisi kule Arusha haya kazi kwenu. Madudu ni mengi ndio maana kuna kasi ya kufungia social media ili watu wavikwe mewani za mbao kama enzi ya Mchongameno ! Wizi uko pale pale hakuna cha kutumbua ilikuwa ni justification ya kuweka watu wake kwenye mfumo but mind you it’s only for ten years baada ya hapo akija mwingine atatumbua wote na kwenda Mahakamani but always ushahidi huwa kama machozi ya Samaki baharini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…