#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jpm is dead and gone..rudisha akili zako wewe.

Vaccine inakuja iwe ni kwa kodi zetu au laah..hutaki andamana.

Madaktari wanapambana na wagonjwa wanakuwa exposed unataka na wajinunulie?
 
Kwahiyo wachungaji huwa hawaendi hospitali wakiugua??
 
Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni mjinga tu asiyeona kuwa Mungu wa Mbinguni kajitukuza kupitia kifo cha MAGU. Wengi huko duniani wanatushangaa kwamba pamoja na sacrifice hii ya MAGU tunafanya haya yanayoendelea nchini kuhusu corona. Dunia inatushangaa narudia tena.
 
Hakuna aliyekuwa mbishi Kama Trump mwisho wa siku alitinga barakoa.
Trump fisadi aliambiwa jifanye una corona tatizo lionekabe kubwa tupige pesa ndio akajifanya kwenda kujilaza hospitali ya jeshi

Hizi porojo za ooh Corona IPO ni ujanja tu mifisadi serikalini inataka kupiga pesa tu

Kuepusha hill bunge shaurini hospitali binafsi ndio ziagize hizo chanjo iwe Agha khan au hospitalli yeyote ila isiwe ya serikalini

Kuna wizi mkubwa Wa kupiga pesa unaandaliwa kwa kisingizio cha Corona.Wote mashahidi Corona ingekuwepo ule umati uliokuwa ukibanana kuaga marehemu Magufuli njiani na viwanjani SAA hizo maiti zingezagaa kila kona

Mijizi serikalini inataka pa kuibia kupitia mradi Wa gonjwa hewa LA Corona walilojitungia wenyewe ambalo mitaani halionekani lakini wao wanashupalia kuwa lipo!!!!

Dawa ni Chanjo isiagizwe na serikali iachiwe sekta binafsi.Hiyo mijizi ikose hela
 
Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtume na Yesu walikamilisha kilichowaleta duniani kwa ushindi ssa JPM alichopinga ndio kimemuondoa duniani ssa hapo utalinganisha vp??

Then JPM alikua na vimada je Mungu huwa anajimix na wahuni? JPM alikua anazindikwa kimila ili asidhurike na wabaya wake hvi Mungu hujichanganya na wachawi? JPM hakuwahi kuwa mcha Mungu hata alipokuja pale BCIC alisema mke wake ndio huwa anamforce kuja kanisani ingawa huwa hatakagi kuja!! Nashangaa sana mnayemuona ni mcha Mungu
 
Mimi naamini Mungu alishatushindia Corona
Sitachanjwa na wala sitaki barakoa wavae wapagani wasio amini Mungu

Kuvaa barakoa kwanza kunaharibu sura MTU USO unaonekana kama wa kinyago cha kimakonde
Eti wavae wspagani wasiomwsmini Myngu! Ins maana maaskofu wanaovaa hawamwamini Mungu
 
Wewe wasema! Suala ni unaendaje hospitalini? Hukawii kupasuliwa goti badala ya kichwa ama vice versa tumesha wahi ya shuhudia hayo.
Huyo JPM anayemtegemea Mungu mbona alitumia kifaa cha mzungu kusukuma damu badala ya kutegemea moyo alioumbwa nao? Si angekichomoa afu tuone!!!

Tuache kumtania Mungu.....
 
Ni Kweli kanisa hii serikalini ya sasa in dharau kubwa kwa Mungu aliyetushindia Corona inafanya sala na dua zote zikizofanywa na mashehe na Viongozi Wa dini zote na watanzania wote kuwa ni ujinga mtupu
Nchi ilishakuwa inipigiwa mfano kuwa oneni Tanzania wategemea Mungu Corona walivyoipiga mieleka

Kilichopo serikalini kwa sasa ni kampeni ya kumdharau Mungu kuwa hana lolote na hakuna Cha maana alichofanya kuhusiana na Corona!!!

Sisi wananchi tunabaki na Mungu wetu, mibarakoa na michanjo tunaiachia ikulu mama Samia na wenzao wasiamini Mungu na uwezo wake
 
Watu wanapinga chanjo ya Corona sijui wanafanya shughuli gani ambayo utafanya awe salama miaka yote bila kinga wakati miaka inasonga mbele na mwili unaanza kuzeeka polepole na kinga ya mwili inapungua huku magonjwa nyemelezi yakisogea. iwapo kama watu wengine watachanjwa na wengine hawatachanjwa corona itakwishaje?. pinga leo ukijiona una nguvu na utakubali badaye wakati huna uwezo kuongeza nguvu.Je miaka 5 ijayo utakuwa na nguvu na afya kama mwaka huu. utakwenda mwenyewe kulazimisha uchanjwe.Dunia Duara
 

Trump na wanao jielewa wote Dunia wamechwanjwa placebo maana wanajua siri ya hii agenda yao ya corona. Wakwetu hapa anachezeshwa ngoma asiyo ijua atachanjwa virusi, poor Tanzanians!
 
Mkuu najua unajua ila unataka kujua zaidi.. stay tuned mdogwangu...
 
Huyo JPM anayemtegemea Mungu mbona alitumia kifaa cha mzungu kusukuma damu badala ya kutegemea moyo alioumbwa nao? Si angekichomoa afu tuone!!!

Tuache kumtania Mungu.....

Hujielewi wewe maarifa ya kifaa hicho yalitoka kwa Mungu au kwa shetwani? Corona na chanjo yake sina shaka hata chembe nivya shetwani.
 
Duh,yaani ukisoma coments za watu humu unashangaa.Yaani watu hawapendi kujua wala kujifunza,watu wanakasirka sababu corona imeongelewa,takwimu zitatolewa.Yaani wengi wanaamini kutojua ndo kusalimika! watu wanapenda kupelekwa kama gari bovu hawataki jukumu la kufikiria au kuwa responsible.
Mh. Rais Samia ana kazi kubwa kuwaongoza hawa watu wanaosubiri kuitwa wanyonge,lakini akaze hapo hapo asikubali kuyumbishwa na hao walozoea hadithi za abunuwasi.Mambo anayofanya ilibidi yafanyike zamani,ilibidi watu waelimishwe na wataalamu wapewe nafasi,lakin Magu alilifumbia macho tatizo na hakupenda mawazo ya wengine wakati yeye hakuwa na ujuzi wowote na hili.wakati dunia inalia na kupambam na Corona yeye alikiwa anakebehi na watu wanachekelea,sasa mda umefika ku face realities watu hawapo tayri,kweli kamwachia mwenzake zigo la mavi.
 
Hujielewi wewe maarifa ya kifaa hicho yalitoka kwa Mungu au kwa shetwani? Corona na chanjo yake sina shaka hata chembe nivya shetwani.
Kwahiyo mzungu akitengeneza mashine akampatia JPM inatoka kwa Mungu. Ila mzungu huyo huyo akitoa chanjo akimletea JPM inageuka ya shetani.

Hahahahahaha aisee uwe na siku njema mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…