#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Kwani kipindi JPM yupo corona haikuua? Mbona wazazi wangu ni wapenda dini sana lakini waliponea ICU....tulipoteza viongozi wawili wa Dini kwenye kanisa letu hapo usisahau mapadri 25 wa RC walifariki?? Sasa ina maana hao hawakuwa na Mungu??

Kuhusu kutovaa barakoa ni sababu ya kumuogopa JPM tu hakuna Kingine. Hvi JPM na uhuni wake tu maombi yake yangesikilizwa na Mungu gani? Alikua amezindikwa na majini ya kumlinda je Mungu gani alitegemewa hapo?

JPM alikufa, kma kweli alimtegemea Mungu hakupona ?
Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanjo iletwe kwa anayetaka hatutaki kuchanjwa kwa kulazimishana hapa. Sisi wengine tumaini na tegemeo letu ni Bwana Yesu wa Nazareti aliye hai, ndiye chanjo yetu na mlinzi wetu wa uhakika hatuhitaji kuhusishwa na kuwa sehemu ya huu upuuzi.

Team ya madaktari inashauri wachanjwe waongoza watalii kwa nini wasianze wenyewe hao madaktari kuchwanjwa? Maana wao pia wako ftont line. Hatutakubali kuwa sehemu ya kumdharaulisha Mungu tuliye mtegemea siku zote katika janga hili. Mungu wa mbinguni hadhihakiwi na wala watutokubali kuwa sehemu ya kumdhihaki Mungu wetu.
Jpm is dead and gone..rudisha akili zako wewe.

Vaccine inakuja iwe ni kwa kodi zetu au laah..hutaki andamana.

Madaktari wanapambana na wagonjwa wanakuwa exposed unataka na wajinunulie?
 
Katika makundi waliyo shauri eti viongozi wa dini wako katika mazingira hatarishi hivyo wachanjwe. Nitampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika.

Viongozi wa Kiroho kuweni makini mlifunga na kuomba mkiongoza waumini wenu kumtegemea Mungu wa Mbinguni. Shetani mjamjanja na mhila sasa anamtumia Rais na tume ya wataalamu kutaka kuwaingiza choo cha kike kuwa maamuzi yale yalikuwa ni ujinga.
Kwahiyo wachungaji huwa hawaendi hospitali wakiugua??
 
Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni mjinga tu asiyeona kuwa Mungu wa Mbinguni kajitukuza kupitia kifo cha MAGU. Wengi huko duniani wanatushangaa kwamba pamoja na sacrifice hii ya MAGU tunafanya haya yanayoendelea nchini kuhusu corona. Dunia inatushangaa narudia tena.
 
Hakuna aliyekuwa mbishi Kama Trump mwisho wa siku alitinga barakoa.
Trump fisadi aliambiwa jifanye una corona tatizo lionekabe kubwa tupige pesa ndio akajifanya kwenda kujilaza hospitali ya jeshi

Hizi porojo za ooh Corona IPO ni ujanja tu mifisadi serikalini inataka kupiga pesa tu

Kuepusha hill bunge shaurini hospitali binafsi ndio ziagize hizo chanjo iwe Agha khan au hospitalli yeyote ila isiwe ya serikalini

Kuna wizi mkubwa Wa kupiga pesa unaandaliwa kwa kisingizio cha Corona.Wote mashahidi Corona ingekuwepo ule umati uliokuwa ukibanana kuaga marehemu Magufuli njiani na viwanjani SAA hizo maiti zingezagaa kila kona

Mijizi serikalini inataka pa kuibia kupitia mradi Wa gonjwa hewa LA Corona walilojitungia wenyewe ambalo mitaani halionekani lakini wao wanashupalia kuwa lipo!!!!

Dawa ni Chanjo isiagizwe na serikali iachiwe sekta binafsi.Hiyo mijizi ikose hela
 
Alikufa Mtume Mohamad na Yesu waliokatumwa na Mungu sembuse Magu apone asife kisa tu akimtumania Mungu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtume na Yesu walikamilisha kilichowaleta duniani kwa ushindi ssa JPM alichopinga ndio kimemuondoa duniani ssa hapo utalinganisha vp??

Then JPM alikua na vimada je Mungu huwa anajimix na wahuni? JPM alikua anazindikwa kimila ili asidhurike na wabaya wake hvi Mungu hujichanganya na wachawi? JPM hakuwahi kuwa mcha Mungu hata alipokuja pale BCIC alisema mke wake ndio huwa anamforce kuja kanisani ingawa huwa hatakagi kuja!! Nashangaa sana mnayemuona ni mcha Mungu
 
Mimi naamini Mungu alishatushindia Corona
Sitachanjwa na wala sitaki barakoa wavae wapagani wasio amini Mungu

Kuvaa barakoa kwanza kunaharibu sura MTU USO unaonekana kama wa kinyago cha kimakonde
Eti wavae wspagani wasiomwsmini Myngu! Ins maana maaskofu wanaovaa hawamwamini Mungu
 
Wewe wasema! Suala ni unaendaje hospitalini? Hukawii kupasuliwa goti badala ya kichwa ama vice versa tumesha wahi ya shuhudia hayo.
Huyo JPM anayemtegemea Mungu mbona alitumia kifaa cha mzungu kusukuma damu badala ya kutegemea moyo alioumbwa nao? Si angekichomoa afu tuone!!!

Tuache kumtania Mungu.....
 
Taifa lilioonesha msimamo wa kuigwa Dunia mzima kuwa linamtegema Mungu wa Mbinguni sasa linageuzwa kuwa kituko cha duniani na linaenda kumuabisha na kumdhalilisha Mungu wa Mbinguni kwa shetani na mawakala wake. Heri ukosema mali za dunia hii kuliko kukosa hekima na busara ya kumheshimu Mungu wa Mbinguni.
Ni Kweli kanisa hii serikalini ya sasa in dharau kubwa kwa Mungu aliyetushindia Corona inafanya sala na dua zote zikizofanywa na mashehe na Viongozi Wa dini zote na watanzania wote kuwa ni ujinga mtupu
Nchi ilishakuwa inipigiwa mfano kuwa oneni Tanzania wategemea Mungu Corona walivyoipiga mieleka

Kilichopo serikalini kwa sasa ni kampeni ya kumdharau Mungu kuwa hana lolote na hakuna Cha maana alichofanya kuhusiana na Corona!!!

Sisi wananchi tunabaki na Mungu wetu, mibarakoa na michanjo tunaiachia ikulu mama Samia na wenzao wasiamini Mungu na uwezo wake
 
Watu wanapinga chanjo ya Corona sijui wanafanya shughuli gani ambayo utafanya awe salama miaka yote bila kinga wakati miaka inasonga mbele na mwili unaanza kuzeeka polepole na kinga ya mwili inapungua huku magonjwa nyemelezi yakisogea. iwapo kama watu wengine watachanjwa na wengine hawatachanjwa corona itakwishaje?. pinga leo ukijiona una nguvu na utakubali badaye wakati huna uwezo kuongeza nguvu.Je miaka 5 ijayo utakuwa na nguvu na afya kama mwaka huu. utakwenda mwenyewe kulazimisha uchanjwe.Dunia Duara
 
Trump fisadi aliambiwa jifanye una corona tatizo lionekabe kubwa tupige pesa ndio akajifanya kwenda kujilaza hospitality ya jeshi

Hizi porojo za ooh Corona IPO ni ujanja tu mifisadi serikalini inataka kupiga pesa tu

Kuepusha hill bunge shaurini hospitali binafsi ndio ziagize hizo chanjo iwe Agha khan au hospitalli yeyote ila isiwe ya serikalini

Kuna wizi mkubwa Wa kupiga pesa unaandaliwa kwa kisingizio cha Corona.Wote mashahidi Corona ingekuwepo ule umati uliokuwa ukibanana kuaga marehemu Magufuli njiani na viwanjani SAA hizo maiti zingezagaa kila kona

Mijizi serikalini inataka pa kuibia kupitia mradi Wa gonjwa hewa LA Corona walilojitungia wenyewe ambalo mitaani halionekani lakini wao wanashupalia kuwa lipo!!!!

Dawa ni Chanjo isiagizwe na serikali iachiwe sekta binafsi.Hiyo mijizi ikose hela

Trump na wanao jielewa wote Dunia wamechwanjwa placebo maana wanajua siri ya hii agenda yao ya corona. Wakwetu hapa anachezeshwa ngoma asiyo ijua atachanjwa virusi, poor Tanzanians!
 
Mkuu unafananisha na mlipuko wa kuambukizwa kwa hewa tena unaikumba dunia nzima kwa mkupuo na magonjwa ambayo yameshapata control strategies??

Hta kipindu pindu kikilipuka huwa takwimu karbu kila cku zinatoka coz ni mlipuko so takwimu ni muhim kujua tunacontrol vp.
Mkuu najua unajua ila unataka kujua zaidi.. stay tuned mdogwangu...
 
Huyo JPM anayemtegemea Mungu mbona alitumia kifaa cha mzungu kusukuma damu badala ya kutegemea moyo alioumbwa nao? Si angekichomoa afu tuone!!!

Tuache kumtania Mungu.....

Hujielewi wewe maarifa ya kifaa hicho yalitoka kwa Mungu au kwa shetwani? Corona na chanjo yake sina shaka hata chembe nivya shetwani.
 
Duh,yaani ukisoma coments za watu humu unashangaa.Yaani watu hawapendi kujua wala kujifunza,watu wanakasirka sababu corona imeongelewa,takwimu zitatolewa.Yaani wengi wanaamini kutojua ndo kusalimika! watu wanapenda kupelekwa kama gari bovu hawataki jukumu la kufikiria au kuwa responsible.
Mh. Rais Samia ana kazi kubwa kuwaongoza hawa watu wanaosubiri kuitwa wanyonge,lakini akaze hapo hapo asikubali kuyumbishwa na hao walozoea hadithi za abunuwasi.Mambo anayofanya ilibidi yafanyike zamani,ilibidi watu waelimishwe na wataalamu wapewe nafasi,lakin Magu alilifumbia macho tatizo na hakupenda mawazo ya wengine wakati yeye hakuwa na ujuzi wowote na hili.wakati dunia inalia na kupambam na Corona yeye alikiwa anakebehi na watu wanachekelea,sasa mda umefika ku face realities watu hawapo tayri,kweli kamwachia mwenzake zigo la mavi.
 
Hujielewi wewe maarifa ya kifaa hicho yalitoka kwa Mungu au kwa shetwani? Corona na chanjo yake sina shaka hata chembe nivya shetwani.
Kwahiyo mzungu akitengeneza mashine akampatia JPM inatoka kwa Mungu. Ila mzungu huyo huyo akitoa chanjo akimletea JPM inageuka ya shetani.

Hahahahahaha aisee uwe na siku njema mkuu
 
Back
Top Bottom