Nawashangaa Baadhi ya watu kuanza mijadala ya kupinga suala la chanjo kama vile serikali imelazimisha kila mtu achanjwe.
Hatuwezi kuwa na mawazo yanayolingana ndani ya nchi hii tupo tunaotaka chanjo na tuna sababu zetu kwa mfano. Biashara za kimataifa, working overseas n.k kwa sasa kama huna kinga huwezi kuingia katika nchi zingine.
Na wanaopinga chanjo nao wana sababu zao kwamfano wengine wanasema chanjo ni mpango wa mabeberu kutuua .sawa zote ni sababu.
Kimsingi naipongeza serikali kuweka Uhuru kwa kila mwananchi kuamua anaetaka sawa na asiyetaka sawa. TUSIPANGIANE.