#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Ni Kweli kanisa hii serikalini ya sasa in dharau kubwa kwa Mungu aliyetushindia Corona inafanya sala na dua zote zikizofanywa na mashehe na Viongozi Wa dini zote na watanzania wote kuwa ni ujinga mtupu
Nchi ilishakuwa inipigiwa mfano kuwa oneni Tanzania wategemea Mungu Corona walivyoipiga mieleka

Kilichopo serikalini kwa sasa ni kampeni ya kumdharau Mungu kuwa hana lolote na hakuna Cha maana alichofanya kuhusiana na Corona!!!

Sisi wananchi tunabaki na Mungu wetu, mibarakoa na michanjo tunaiachia ikulu mama Samia na wenzao wasiamini Mungu na uwezo wake

Na wasipo tubu huu ujinga, hapa na tumia neno zuri 'UJINGA' wao, wajue Mungu wa Mbinguni hadhihakiwi hata kidogo.
 
Eti wavae wspagani wasiomwsmini Myngu! Ins maana maaskofu wanaovaa hawamwamini Mungu
Ndio hawaamini Mungu hao ni wapagani

Ona hata Siku ya kuaga Magufuli uwanja Wa Taifa watu wote hawakuvaa barakoa isipokuwa Askofu mkuu Wa katoliki na mapadri wake!! Waumini hawaogopi Corona wanamtegemea Mungu Maaskofu na mapadri wanavaa mibarakoa kuogopa Corona!! Viongozi Wa serikali wana gari zao binafsi barakoa haziwatoki midomoni uswahili watu wanashonana barabara kwenye daladala na huoni mtu mwenye barakoa .Hakuna anayeogopa na huoni vivo mitaani vya Corona!!!

Corona ni ugonjwa Wa Ikulu labda na serikalini huko wizara ya afya labda ambao wana maslahi nao.Mitaani haupo tusidanganyane MTU kama anataka kuiba hela atafute sehemu zingine sio kusingizia Corona
 
Watu wanapinga chanjo ya Corona sijui wanafanya shughuli gani ambayo utafanya awe salama miaka yote bila kinga wakati miaka inasonga mbele na mwili unaanza kuzeeka polepole na kinga ya mwili inapungua huku magonjwa nyemelezi yakisogea. iwapo kama watu wengine watachanjwa na wengine hawatachanjwa corona itakwishaje?. pinga leo ukijiona una nguvu na utakubali badaye wakati huna uwezo kuongeza nguvu.Je miaka 5 ijayo utakuwa na nguvu na afya kama mwaka huu. utakwenda mwenyewe kulazimisha uchanjwe.Dunia Duara
Mungu ndiye aliyetoa uwezo wa kutengeneza chanjo na kutibu maradhi. Alifanya hivo tusimchoshe kila kitu kuomba tu.
 
Mungu ndiye aliyetoa uwezo wa kutengeneza chanjo na kutibu maradhi. Alifanya hivo tusimchoshe kila kitu kuomba tu.

The agenda behind corona is what matters the most. Haya mambo yako wazi katika Neno la Mungu. Na Mungu hakufanya hivyo ili mwisho wa siku tusimtegemee na kumtumaini yeye au tuone kufanya hivyo ni ujinga.
 
Mtume na Yesu walikamilisha kilichowaleta duniani kwa ushindi ssa JPM alichopinga ndio kimemuondoa duniani ssa hapo utalinganisha vp??

Then JPM alikua na vimada je Mungu huwa anajimix na wahuni? JPM alikua anazindikwa kimila ili asidhurike na wabaya wake hvi Mungu hujichanganya na wachawi? JPM hakuwahi kuwa mcha Mungu hata alipokuja pale BCIC alisema mke wake ndio huwa anamforce kuja kanisani ingawa huwa hatakagi kuja!! Nashangaa sana mnayemuona ni mcha Mungu
Alikua mwafrika kama wewe na mimi..na hivyo ndivyo waafrika hufanya..wewe brainwashed creature.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trump na wanao jielewa wote Dunia wamechwanjwa placebo maana wanajua siti ya agenda yao. Wa kwetu hapa anachezeshwa ngoma asiyo ijua atachanjwa virusi, poor Tanzanians!
Bora kumdanganya mtu kisayansi kuliko kumdanganya kiimani. Waafrika wengi ni wehu kiimani na wanaendelea kudanganyana. Hii ni pandemic tosha kuwaangamiza
 
Chanjo iletwe kwa anayetaka hatutaki kuchanjwa kwa kulazimishana hapa. Sisi wengine tumaini na tegemeo letu ni Bwana Yesu wa Nazareti aliye hai, ndiye chanjo yetu na mlinzi wetu wa uhakika hatuhitaji kuhusishwa na kuwa sehemu ya huu upuuzi.

Team ya madaktari inashauri wachanjwe waongoza watalii kwa nini wasianze wenyewe hao madaktari kuchwanjwa? Maana wao pia wako ftont line. Hatutakubali kuwa sehemu ya kumdharaulisha Mungu tuliye mtegemea siku zote katika janga hili. Mungu wa mbinguni hadhihakiwi na wala watutokubali kuwa sehemu ya kumdhihaki Mungu wetu.
Hapo utakuta ukilala hua unashusha net ili usipate Malaria,ukiugua hua unaenda Hospitali kutibiwa!
 
Bora kumdanganya mtu kisayansi kuliko kumdanganya kiimani. Waafrika wengi ni wehu kiimani na wanaendelea kudanganyana. Hii ni pandemic tosha kuwaangamiza

Kama kiongozi wa nchi anashindwa kujiuliza na kujitafakarisha jambo dogo tu la kwa nini jinsi huduma za kiafya zilivyo modern and advanced USA na Ulaya lakini bado vifo vimetokea kwa idadu hiyo ya makumi elfu anasaidika vipi huyu?
 
Maajabu ni kwamba wapo watu hapa Tanzania hawataki chanjo na hawajalazimishwa .lakini pia hawataki wengine wanaotaka chanjo wapate. Wanaamini ni mpango wa mabeberu kutuuwa. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Akili Ndogo sana za Mwendazake
 
Hivi havifanani wala kufananishwa hata kidogo na yale yote yatokanayo na corona. Wala usijifanye hamnazo.
Naona akili zako umeamua kuziweka kwenye mfuko wa shati,ukizirudisha kichwani njoo tujadili kwa akili na sio kwa kuendeshwa na mihemko kama ulivyo sasa hivi.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona....
Inatia moyo kuona serekali kuanza kuwa sikivu na makini. Nadhani wengi tulio nje ya TZ tulikuwa tunaona wanasiasa wakicheza mchezo wa hatari na maisha ya wenzao. Mapendekezo hayo sio mageni kwa wale ambao wanafuatilia nchi zengine zimepitia hatua gani katika janga hili.
 
Inatia moyo kuona serekali kuanza kuwa sikivu na makini. Nadhani wengi tulio nje ya TZ tulikuwa tunaona wanasiasa wakicheza mchezo wa hatari na maisha ya wenzao. Mapendekezo hayo sio mageni kwa wale ambao wanafuatilia nchi zengine zimepitia hatua gani katika janga hili.

Tuchukue akili ya USA kwa mfano wenye vifo takribani 600, 000 pamoja na kuwa na huduma bora sana za kuafya? Na chelea kusema, Huu si umakini na usikivu bali ni ujinga katika ubora wake.
 
Kama COVID-19 utakuwa ugonjwa wa kujirudiarudia kwa msimu au kwa mawimbi mbalimbali kama wanasayansi wengi wanavyotabiri itakuwa habari mbaya sana kwa wapinga chanjo na mataifa yanayozembea kuwachanja raia wake.

Kila wimbi litakalokuja litaondoa idadi kubwa ya wazee na watu mbalimbali wenye matatizo makubwa ya kiafya. Pia wapo watakaoumwa na kuteseka kwa wiki kadhaa mahospitalini.

Wanawake wengi zaidi watabaki wajane na wajukuu wengi watapoteza babu na bibi zao endapo wimbi lingine kali zaidi litaibuka huku watu wakiwa hawana chanjo.

Hatua za haraka zichukuliwa.Kamati ya Rais imekwishatoa mapendekezo yake, ni wakati wa kuharikisha chanjo sasa kwa wale wenye kuzihitaji na kuwaacha wapingaji waendelee kucheza kamari na maisha yao.

Wapinga Chanjo na wanaojivuta kwenye chanjo. COVID itawalimisha kwa meno kama bado itaendelea kuwepo wepo.
 
... Rais na Mwenyekti wa Kamati kwenye makabidhiano ya ripoti (just two people) wamevaa barakoa halafu kapuku mwenzangu unajitoa ufahamu eti hakuna korona! Watch out!
Na duniani kote wanaojimwambafy kuwa hakuna korona walishaenda zao!!!!
 
Back
Top Bottom