mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Hayo maswali hata kuyasogea hawezi kuthubutu! Hayo mapendekezo hasa lile la kwanza watakuwa wameelekezwa!Naomba hiyo Kamati ijibu maswali haya: -
Je,ukipata hiyo chanjo:-
(1)Unaendelea kuvaa barakoa?
(2) Unaweza kuambukiza au kuambukizwa Corona?
(3) Ni Nchi ngapi zilizotumia chanjo na hali ikoje baada ya kutumia hiyo chanjo?
(4) Kama kweli hiyo chanjo inasaidia, kwa nini huko Duniani Corona bado inasumbua sana?
Hivi inaingia akilini watu wazima wakiwa wamevaa barakoa (kwa kuogopa corona) halafu wanasema Serikali itangaze kuwa kuna corona! Sasa kama serikali haijasema uwepo wa corona kwa nini mnavaa barakoa?
Hivi ni kweli kuna mtanzania anayehitaji kutangaziwa na serikali kuwa kuna corona? Hivi kuna mtanzania asiyejua habari za corona? Serious! Kinachotafutwa ni Tanzania tubatilishe ukiri wetu kuwa Mungu ametuponya! Na kamwe hilo lisitokee!! Shetani anasubiri hilo kwa hamu!!