#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Naomba hiyo Kamati ijibu maswali haya: -
Je,ukipata hiyo chanjo:-
(1)Unaendelea kuvaa barakoa?
(2) Unaweza kuambukiza au kuambukizwa Corona?
(3) Ni Nchi ngapi zilizotumia chanjo na hali ikoje baada ya kutumia hiyo chanjo?
(4) Kama kweli hiyo chanjo inasaidia, kwa nini huko Duniani Corona bado inasumbua sana?
Hayo maswali hata kuyasogea hawezi kuthubutu! Hayo mapendekezo hasa lile la kwanza watakuwa wameelekezwa!

Hivi inaingia akilini watu wazima wakiwa wamevaa barakoa (kwa kuogopa corona) halafu wanasema Serikali itangaze kuwa kuna corona! Sasa kama serikali haijasema uwepo wa corona kwa nini mnavaa barakoa?

Hivi ni kweli kuna mtanzania anayehitaji kutangaziwa na serikali kuwa kuna corona? Hivi kuna mtanzania asiyejua habari za corona? Serious! Kinachotafutwa ni Tanzania tubatilishe ukiri wetu kuwa Mungu ametuponya! Na kamwe hilo lisitokee!! Shetani anasubiri hilo kwa hamu!!
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona...

Taarifa imejaa maneno yafuatayo:
Serikali ihuishe, Wadau mbalimbali, JMT na SMZ ziendelee kushirikiana ipasavyo, jukumu ipasavyo, maadili na taratibu zilizowekwa....n.k. Maneno kama haya hayapimiki, na unaweza kuyatekeleza unavyotaka maana hayana viwango. Hiyo ndo ripoti ya rais.

Huu ni uzembe wa juu sana. Mtu anajiandikia mambo ya mitandaoni bila hata uzoefu. Rais naye sijui kama anaichukua hii kama ndo kigezo cha kupambana na COVID-19. Kuna maneno meengi ya hovyo tu!
 
Naomba hiyo Kamati ijibu maswali haya: -
Je,ukipata hiyo chanjo:-
(1)Unaendelea kuvaa barakoa?..
Hawa wazembe hata hawakusoma taarifa za nchi zingine, hawakueleza hali ya nchi yetu wakati wa korona na manufaa tuliyopata, hawasemi muelekeo wa ugonjwa ni upi?

kwa ujumla ni ripoti ya kufurahisha mataifa wamuone rais yuko serious kuaminika, akiaamini JPM hakuaminika. Ndo akili mbovu ya wanasiasa wa kiafrika kuona sifa za nje ni muhimu kuliko za ndani ya nchi.
 
Hawa wazembe hata hawakusoma taarifa za nchi zingine, hawakueleza hali ya nchi yetu wakati wa korona na manufaa tuliyopata, hawasemi muelekeo wa ugonjwa ni upi? kwa ujumla ni ripoti ya kufurahisha mataifa wamuone rais yuko serious kuaminika, akiaamini JPM hakuaminika. Ndo akili mbovu ya wanasiasa wa kiafrika kuona sifa za nje ni muhimu kuliko za ndani ya nchi.
Sasa jiwe na yeye unamuona kama mtu timamu
 
Nawasalimu kwajina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ndugu zangu mheshimiwa Rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliunda tume ya Corona.

Taarifa ya tume imepokelewa Jana na wengi wanaendelea kutupa mrejesho ya kile kilichopo kwenye tume.

Naomba niseme taarifa ile sio yakwetu. Taarifa hii ni ya nchi iliyokumbwa na Corona na yenye hari tata sana. Taarifa hii nahisi ilikua ya Kenya sisi tumecopy na sehemu iliyoandikwa Kenya Tumeandika Tanzania.

Wote tunajua nchi hii kila pembe hakuna taarifa za hilo janga hata toka kwenye mitandao ya kijamii hatuoni wala kusikia. Sehemu nyingi nchini toka 29 June 2020 serikali iliporuhusu shule kufunguliwa raia tuliachana na tahadhari za Corona. Masuala ya sanitizers, barakoa, maji tiririka na kutokukusanyika yalipotea.

Watu wanakula bata, misibani tunashiriki, viwanjani tunajaa, maeneo yote yamikusanyiko yanajaa mpaka basi lakini vifo wala wagonjwa wa Corona hakuna.

Leo Dunia inaanza kutengemaa, ulaya viwanjani wameanza kuruhusu mashabiki, vifo vinapungua, lockdown zimeondolewa eti tume inapendekeza lockdown Tanzania seriously!

Niombe wananchi tuchukue tahadhari lakini hii tume ituambie walikokusanyia data.
 
Wewe unaonekana ni mtoto wa juzi,na bado haujaijua vizuri dunia.Hao wenye ABC yoyote kuhusu elimu ya afya, wengi tunao huku wamepata matatizo ya kiafya yasiyotatulika kwa hiyo elimu zao.
Ww Ni kilaza pro Max kwahiyo ukiwa na abc za hupati matatizo ya kiafya!??
Hakika ujinga Ni mzigo.
Don't quote me with your childish thoughts.
 
Nakubaliana na wewe wanaotaka chanjo wajiandikishe walipie hela kanisa halafu serikali iwaagizie pesa zetu za Kofi zisitumike kwenye huo ujinga .

Au hospitali binafsi waruhusiwe kuagiza hizo chanjo halafu wanaozitaka waende huko hospital binafsi wakachanjwe

Kodi zetu zisitumike kwenye huo utapeli
Kabisa, nasikia madalali wameweka cha juu karibia 500%, hii ni Escrow nyingine wanataka kupiga
 
Katika mila na desturi, mzazi au mlezi anaejali, yupo makini na usalama wa mtoto. Mara zote amlishapo chakula hukionja kwanza. Tabia au desturi hii yaweza tafsiriwa kuwa ni uroho, lakini hapana. Ni kutaka kujua usalama wa hicho chakula, hasa hali ya joto, ili asiungue. Akizembea, matatizo yampatayo mtoto humsumbua kwa gharama ya fedha na muda wakati wa kumtibu. Taarifa za chanjo ya corona zinatia matumaini, haina madhara. Ni vema tukaenda na jukumu la mama kuonja uji wa mtoto kwanza.
 
Nimekumanya ndugu yangu. Kwa mtazamo wako suala la chanjo makundi yaliyopendekezwa na tume yaachwe kwanza badala yake waanze viongozi wakisiasa!
 
Mimi naamini Mungu alishatushindia Corona
Sitachanjwa na wala sitaki barakoa wavae wapagani wasio amini Mungu

Kuvaa barakoa kwanza kunaharibu sura MTU USO unaonekana kama wa kinyago cha kimakonde
Mimi na familia yangu hatutachanja hiyo sijui Corona...na sitasafiri Tena nje ya nchi..Mimi siyo kibaraka wa mabeberu...athari ya chanjo itajitokeza baada ya miaka miwili kuanzia mtu anapochanjwa...
 
Ndio raisi wetu huyo haijalishi unapenda au hupendi,Hao unaowaita mabeberu wana mchango wao mkubwa kwenye bajeti ya nchi hii,hilo hulioni sasa chanjo ikija ni uhuru wako kuchanjwa au kutochanjwa ili umfurahishe yule mnae mwita mwamba eti wa Afrika nenda pale Chato kahiji.Lakini kwa unafiki wa mlio wengi wa aina yako utakuwa mstari wa mbele kuchanjwa kimya kimya.


Sawa...
 
Fuatilia VISIWA VYA SHERISHERI, kwa sasa upate kinachoendelea baada ya chanjo. Any way kwa vile wamependekeza chanjo ni hiyari basi kazi iendelee


Haitakuwa hiyari.. Vitaweka vi terms vya kukulazimisha indirectly
 
Mh Rais kwanza tunakupongeza sana kwa kutuundia kamati ya wataalam ya ugonjwa wa Corona waliochunguza na kukukabidhi ripoti yao.Ni ripoti ya kitaalam na kisayansi.Dunia nzima imefurahishwa na kazi nzuri ya kamati na mapendekezo waliyoyatoa.

Angalau sasa Dunia imeanza tena kutuona Tanzania imerudi pahala pake.Hata gazeti maarufu la serikali ya kikoministi ya huko China Limesifu taarifa hiyo ya wataalam uliowachagua na mapendekezo waliyoyatoa.Sasa tunakuomba wewe na serikali yako muifanyie kazi ili tuweze kujumuika na Dunia kuendeleza uchumi wetu ulioterereka na covid 19.

Vikwazo kibao kwa wasafiri,wagonjwa,wafanya biashara,watalii,wawekezaji n.k kwa sababu tulijitenga na dunia tukajiona tunaishi mbinguni.Wengi hasa wafanya biashara wakubwa na watalii original walisusa kuja kwa kuogopa gonjwa la corona.tukadhihakiwa sana wakati waziri wa afya anasema dawa ya corona ni kujifukiza na bila aibu akaonyesha mbele ya vyombo vya habari vya nje na ndani.kuhusu chanjo kamati imependekeza mambo ya maana sana na yule asiyetaka shauri yake.MH RAIS TURUDISHE IMANI ILI MAENDELEO YA WANANCHI YAPATIKANE.

Wapo wapuuzi wanaodai tumtangulize Mwenyezi Mungu mbele hili halina ubishi MOLA ni wa kutangulizwa mbele Daima na Milele.Ugonjwa huu umezikumba mpaka sehemu takatifu za ibada kama Makkah,Vatican,Jerusalem,mahekalu ya wayahudi na hivi karibuni India.Hata Hayati JPM alianza kuonyesha na kukubali hatua za haraka zichukuliwe.

Nchi za jirani zikifungua mipaka ndio hapo wale wajinga wachache wataanza kutambua athari za gonjwa hili hatari Corona.

#Salaam za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

#Kazi iendelee.
 
Haikusemwa ovetly kuwa haipo ila impliedly. Na hii ilifanya watu wengi wasitilie maanani kuwa ipo. Serikali ilikuwa inaona kigugumizi gani kusema korona ipo na wtu wanakufa (japo si wengi lakini ni uhai wa watu)? Hata akifa mmoja ni issue!!!! Why the secrecy?
Kwani nilini watu waliacha kufa,kwani kufa kumeanza baada ya corona?watu walikuwa wanakufa kila siku hata Kabla ya corona,sema corona ilivyokuja kila aliyekufa walisema kafa kwa corona, corona ilivyokuja magonjwa yote yakaacha kuua ikabaki corona tu
Yaani bila mzungu hata sasa hivi mimi na wewe tusingekuwa tunachat realtime!!!! Mwizi mkamateni lakini sifa yake mpeni!!!!
Hili ndilo tatizo la africa wengi wanaona bila mzungu dunia isingekuwe, kwani kabla ya mzungu kuleta simu watu walikuwa hawawasiliani?kwani akina kinjeketire/Mkwawa, walikuwa wakiwasiliana vipi kwenye uwanja wa mapambano? Africa tumeshindwa Kuwa wabunifu kwasababu akili zetu tumewakabidhi wazungu watuamlie kila kitu,leo hii mnadhalau limau/matangawizi,eti havikusaidia kutibu corona kisa,avijadhibitishwa na mzungu, lakini dawa zao wanazodunga watu mpaka damu inaganda makorokoro kibao bado mnaona zinafaa, Wafrica tutaendelea Kuwa watumwa mpaka mwisho wa dunia.
 
Haikusemwa ovetly kuwa haipo ila impliedly. Na hii ilifanya watu wengi wasitilie maanani kuwa ipo. Serikali ilikuwa inaona kigugumizi gani kusema korona ipo na wtu wanakufa (japo si wengi lakini ni uhai wa watu)? Hata akifa mmoja ni issue!!!! Why the secrecy?

Wewe hujui consquences za kuwatia hpfu unao waongoza. Tena hofu yenyewe ya kifo. Au hujui corona ni silaha ya shetani na mawakala wake inayotumia hofu kama nyenzo yake kuu. Tunatakiwa tuwe na hofu juu ya Mungu wa Mbinguni tu anaye weza kuua Mwili na Roho zetu.

Heri kukosa mali na fahari zoylte za dunia hii kuliko kukosa hekima ya kumcha, kumwamini, kumtegemea, kumtumainia na juu ya yote kuwa na hofu juu ya Mungu wa Mbinguni. Wengine wamekuwa na hofu ya Mzungu na huu upuuzi wake.
 
Kwanza huyu ni Rais wa Katiba tu,Kama sio kubebwa na Magufuri Nani angelikubari Samia awe rais wetu,rais gani nyoronyoro hivi,aende kwao zanzibar sie Watanganyika tulisha choka,kwanza ni mvivu.anawaza misaada tu.
Relax.
 
Back
Top Bottom