#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Mimi sina imani nao hao watu wa Laboratory tangu Hayati Dr Magufuli kuwapa Vipimo vya Mbuzi ,Damu ya kwale,mafuta ya dizeli na mafenisi yote hayo walipima hao Wana-Sayansi wa Laboratory. Na Wakakuta Vipo Positive Covid19?
Leo Mheshimiwa Rais Mama Suluhu amewapa hao hao Wana -Sayansi wa Laboratory kupima Chanjo ya Corona Virus? Unafikiri watasema haifai kuchanjwa? Au si Salama? Sisi Waafrika Akili zetu kitu kikitoka kwa Mzungu tuna imani kipo salama. Kumbe kina madhara makubwa sana.

View attachment 1790258
Hawajakataa "tiba mbadala" wala tafiti za kienyeji...
 
Alichokisahau yeye na waliomuunga mkono ni kuwa vingi vya mabeberu tunavyovitumia kv: "mionzi ya simu, magari, ndege zifushazo moshi angani zinapokatiza anga letu... vifaa tiba toka hukohuko kwa wazungu" walijiridhisha kuwa havina athari???
tunaangizwa kutumia akili mara nyingi.

lengo lao usishtuke,kama ambavyo wewe umelala namna hii.
 
Kama hakuna wagonjwa wa Corona
Kuna haja gani ya kukimbilia chanjo za majaribio?
 
View attachment 1789753
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud.

Kamati maalum ya Corona Tanzania iliyoundwa na rais Samia Suluhu Hassan mwezi uliopita imewasilisha ripoti yake hii leo huku ikisema kuwa chanjo dhi ya ugonjwa huo ni salama na zimeonesha ufanisi.
Kamati hiyo imeishauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa covax ulio chini ya mwamvuli wa Gavi.
Mpango wa covax unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi. Mwamvuli wa Gavi unaundwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya Duniani na baadhi ya serikali za nchi tajiri duniani.
"Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi," ameeleza Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili na Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Hata hivyo kamati imetaka mamlaka zilizo chini ya serikali kuendelea kutoa ushauri juu ya jambo hilo.
"Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo," ameeleza Prof Aboud.
Baada ya kamati kutoa ushauri wake, ni jukumu sasa la serikali chini ya Rais Samia kutekeleza mapendekezo hayo.
Mapendekezo ya kamati kuhusu chanjo ya corona yanapingana na sera ambayo nchi hiyo iliitekeleza wakati wa hayati rais John Magufuli ambaye alipinga chanjo hizo kabla ya kufariki akiwa madarakani mwezi Machi na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa makamu wake Mama Samaia. Msimamo wa Magufuli juu ya chanjo na kudhibiti ugonjwa huo ulipingwa vikali nadni na nje ya nchi hiyo.

Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19​

Kamati hiyo imependekeza matumizi huru ya chanjo nchini Tanzania, hii ikimaanisha kuwa hakutakuwa na mtu atakayeshurutishwa kuchoma chanjo hiyo kinyume na matakwa yake binafsi.
Hata hivyo, kamati pia imependekeza pale chanjo itakapoingia Tanzania kuwe na makundi maalumu

Kundi la kwanza ni wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji.
Kundi la pili ni wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50, kundi la tatu ni watu wazima wenye maradhi sugu mengine mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo.
Makundi mengine ni watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.

Vipi kuhusu takwimu na 'lockdown'?​

Kuhusu utolewaji wa takwimu wa mara kwa mara juu ya mwenendo wa ugonjwa huo, kamati imeitaka serikali kurejea katika utaratibu huo. Mara ya mwisho kwa takwimu za ugonjwa huo kutolewa kila siku ilikuwa ni mwaka mmoja uliopita.
"Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia," imeshauri kamati.
Profesa Said Aboud akisoma taarifa ya tume aliyoiongoza mbele ya waandishi wa habari Ikulu, Tanzania.

Maelezo ya picha,
Profesa Said Aboud akisoma taarifa ya tume aliyoiongoza mbele ya waandishi wa habari Ikulu, Tanzania.
Kuhusu kujifungia kama njia ya kudhibiti kasi ya maambukizi, kamati imeishauri serikali "kuendelea kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi."
Rais John Magufuli aliweka hadharani wakati janga hilo lilipoipiga nchi hiyo mwaka jana na kusisitiza mapema mwaka huu kuwa katu chini ya utawala wake asingetekeleza sera hiyo ya 'lockdown' kutokana na athari za kiuchumi ambazo zingejitokea. Hatua hiyo pia ilichangia kukosolewa vikali kwa utawala wake.
Kuhusu athari za kiuchumi kwa ujumla wake, kamati imeshauri wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa Tanzania. chanzo. 'Chanjo ya Corona ni salama na fanisi' - BBC News Swahili
Mnasema ni vizuri/lazima turidhie mikataba ya kimataifa tulio saini, lakini hapo hapo hamtaki WHO kufuata protocol za kuzindua dawa
 
Naona ripoti nene kweli kweli. Sijaona ripoti nene kama hii katika maisha yangu. Kweli SASH ataisoma yote hii?
Halafu wamefikiaje uamuzi wa kuwa chanjo ni salama? Nadhani wame google na kukusanya ripoti tu. Hakuna kitu maalum kilicofanyika Tanzania kilichothibitisha hilo. Ama sivyo watuambie methodology waliyoifuata. Hawa Maprofesa wa Bongo bwana!
Najua kuna shinikizo, na Tanzania pekee haiwezi kukataa, hasa ukiangalia kuwa wangeweza kuifungia watu wake wote wasisafiri.
Wanapenda kujaza mijitabu
Hivi wale wabunge wenzangu na mimi
Wataisoma kweli

Ova
 
Tanzania haina uwezo wa kujitenga na kaka yake dunia - shime ya pekee ni kuwa kuna uhiari wa kuchanja au kutochanjwa
 
Mwendazake alitupoteza sana, kusema chanjo ya Corona ina matatizo wakati chanjo nyingine za wazungu tunazitumia miaka mingi hakuwa sawa, hasa alipodai wazungu hawatupendi it was such a very primitive mentality.
Wazungu wenyewe wanasema hazifai....au hujawasikia ndugu...soma majarida ndugu...vitu vingi haviwekwi hadharani...you need to dig deep
 
Hii chanjo iliyo chini ya mpango wa covax ni ile iliyopigiwa makelele kila kona na wakaamua kuibadilisha hata jina! Nchi nyingi zimeipiga marufuku, halafu mtu anasema chanjo hiyo ni salama (huku akijua kuwa tunafahamu siyo kweli - sijui amewezaje kuikandamiza dhamiri yake!). Wakati baadhi ya watu wamekufa kwa damu kuganda muda mfupi baada ya chanjo hiyo. Pili hizo chanjo zote hakuna ajuaye madhara yàke ya muda mrefu!! Ninaamini hata huko ulaya sehemu kubwa watakuwa wamechanjwa placebo (maji) na wachache ndo wametolewa mhanga wafanyiwe majaribio!!
Niwapongeze kamati kwa kusema hiyo chanjo itakuwa ya hiari, kama majaribio ya chanjo yanavyokuwa.
Hapo kwa hiari wametuokoa...ila kusema ni salama naona haijakaa vizuri

Maana wazungu wenyewe wanasema hizi chanjo sio...na sio ya lazima...

HIV na Covid zote zinashambulia kinga ya mwili...kwanini HIV isiwe na chanjo iwe na dawa za kuboost immunity ila Covid dawa yake iwe chanjo...tutachanjwa magonjwa ambayo tutakuwategemezi wa dawa zao mpaka siku tutadumbukia ardhini....
 
Hayo ndiyo matumizi sahihi ya kodi za wananchi.
Watu walitaka kulazimishia kijiji kiwe jiji tuliona poa tukasema ni sehem ya Tanzania, halafu eti tuone ni dhambi serikali kulinda wananchi wake dhidi ya magonjwa.
Kwanini zisiletwe kisha anaetaka akanunue? Au we unadhani kila mtu yuko tayari kufanyiwa majaribio?
 
Kipi official hapo ambacho tulikua hatukijui?
Sio kwamba unajua au hujui.,
Tunaongelea serikali kiongozi aliyepita hakuwa interested na corona aliyepo ameona kuna haja kuchukua hatua ndio mana ilibidi aanze na hiyo tume ili kama serikali iwe ni starting point., tusahau tulikotoka.

Umekuwa kama darasa la kwanza
 
Kwanini zisiletwe kisha anaetaka akanunue? Au we unadhani kila mtu yuko tayari kufanyiwa majaribio?
Nafikiri niishie hapa.
Asante kwa muda wako, wanaohusika watachukia wanaloona linafaa na kuachana na wanaloona halifai.
Siku njema[emoji120]
 
Mimi sina imani nao hao watu wa Laboratory tangu Hayati Dr Magufuli kuwapa Vipimo vya Mbuzi ,Damu ya kwale,mafuta ya dizeli na mafenisi yote hayo walipima hao Wana-Sayansi wa Laboratory. Na Wakakuta Vipo Positive Covid19?
Leo Mheshimiwa Rais Mama Suluhu amewapa hao hao Wana -Sayansi wa Laboratory kupima Chanjo ya Corona Virus? Unafikiri watasema haifai kuchanjwa? Au si Salama? Sisi Waafrika Akili zetu kitu kikitoka kwa Mzungu tuna imani kipo salama. Kumbe kina madhara makubwa sana.

View attachment 1790258
Unamwamini mwendazake kukiko hawa wataalamu,mimi sinaimani namwendazake
 
Unamwamini mwendazake kukiko hawa wataalamu,mimi sinaimani namwendazake
Kama Huna imani na Hayati Magufuli basi ngojea mupigwe sindano za sumu za chanjo ya Corona wakati ulaya na Amerika Wananchi wanapinga kupigwa hizo sindano zenye sumu .Wanasema zina madhara makubwa sana.
 
Hvi toka lini kutumia chanjo ni kumdhalilisha Mungu? Hvi bila ARVs Tanzania wangekufa watu wangapi? Je kutumia ARVs ni kupinga uweza wa Mungu au ni precaution tu?

Cha kushangaza ukiugua malaria huendagi kuombewa ila unaendaga pharmacy ila linapokuja suala la Corona ndio pharmaceuticals zinageuka dharau kwa Mungu?
weird
Usilolijua ni usiku wa giza ,mambo mengne kama huna viwango vya kiroho huwezi jua
 
Wote tumeshuhudia ile kamati iliyoundwa na rais Samia kuhusu Corona ilivyopopolewa na kupingwa kila kona na watanzania.
Dunia ilitakiwa ije kujifunza Tanzania tunavyopambana na corona lakini sasa hivi kuna nguvu kubwa inalazimisha sisi watanzania tukajifunze namna ya kupambana na corona huko India na Marekani walikokufa wengi.

Kwa report hiyo maprofesa wataendelea kutukanwa na akina Kibajaji na Msukuma wataendelea kusikilizwa na wananchi.
Haiingii akilini maprofesa wanatoa report utafikiri ugonjwa wa Corona umeibuka mwezi wa 3 mwaka huu, maprofesa eti wanapendekeza waziri wa afya aanze kukaa kwenye makamera na kutangaza leo tumepata wagonjwa wa corona idadi kadhaa...!
Kuna kila dalili hao maprofesa wamehongwa ili waje na mapendekezo hayo ya kuwatia hofu watanzania wakati hofu tulishaikataa tangu mwaka 2019.

Kwa muktadha huo nakuomba rais wangu mpendwa Samia Suluhu ipuuze kamati hiyo na mapendekezo yao yote kwani hayana tija yoyote kwa nchi yetu.
 
Kwaiyo wewe unapendekeza ninii mwanawitu?
Kweli tumefikia hatua ya kupanga foleni kununua umeme?

Yani kwa wakati mmoja mfumo wa TRA unasumbua, mfumo wa bandari unasumbua, mfumo wa LUKU unasumbua na TFF nao wamekula hela za wananchi.

Hapa hutaona Lissu, Lema wala Mbowe wakilaani shughuli za wananchi kusimama na kupanga foleni ya kununua umeme.!!

Tunawasiasa wa hovyo kuwahi kutokea kwenye nchi hii, kwenye vichwa vyao wanajua wakilaani haya mapungufu watakuwa wamempromote hayati Magufuli.

Yani ni mijitu ya hovyo kabisa ndiyo maana wanaishi ulaya kwa jasho la wanaume wenzao.
 
Back
Top Bottom