Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

Hivi hii Inshu hahjaisha tuu??
alisikika mwana kijiwe nongwa mmoja hivi...
 
Bro umeongea kama vile hauvijui vilabu vyetu vya Yanga na Simba pamoja na Tff yao ni jinsi gani walivyokuwa na janja janja

Binafsi siamini kama Fei hakuwahi kuwambia Yanga kuhusu hatua anazotaka kuchukua za kuvunja mkataba

Kama Tff waliona Fei hakufuata protocol za kuvunja mkataba kwa nini wasimwambie ukitaka kuvunja mkataba wako fanya hivi ndio Sheria inavyotaka badala yake wanamlazimisha aendelee kuichezea Yanga?
 
Umeongea vizuri kwani hata yanga wanajua feitoto kavunja mkataba ila hakufata utaratibu lakini kamati badala ya kujadili hoja ya yanga ya kuangalia kama feitoto kafata taratibu au la imeenda kutoa maamuzi mengine kabisa
 
Duh mmeamua kujitoa ufahamu. Kama ni kuvunja aje tukae mezani tujadili na sio kuamka na kuweka hela kwenye account na kusema amevunja.

Huko duniani unakosemea waarabu na wachina wangekua wananyanyasa sana vilabu vya Ulaya.
Kama kuna kipengele kwenye mkataba kilichomruhusu kufanya hivyo, huu utetezi wenu ni ujinga mtupu.
 
Mmejaa ujinga mwingi sana, kama mambo yangekuwa mepesi kama mnavyojaribu kujidanganya, hao TFF na Kamati yake wasingepoteza muda ili kuwabeba, utetezi wenu kwenye hii issue ni ujinga mtupu.
 
Mmejaa ujinga mwingi sana, kama mambo yangekuwa mepesi kama mnavyojaribu kujidanganya, hao TFF na Kamati yake wasingepoteza muda ili kuwabeba, utetezi wenu kwenye hii issue ni ujinga mtupu.
Mbumbumbu uliye bobea ainisha eneo ambalo Yanga wame bebwa na Tff. Kesi ya Feisal ni eneo ambalo lilikua alihitaji usomee Sheria Ili utambue kama Feisal kapigishwa shoti.

Ao wanasheria wame tumia mapungufu ya uelewa ya Yusufu Bakresa na familia ya Feisal kujipatia fedha ya Bure uku wakijua iyo kesi wanakwenda kushindwa.

Familia ya Feisal imetumika kufanya jaribio la kuuwa kipaji Cha Feisal Kwa tamaa ya Fedha na Mali.
Ata katika biblia Yuda Iskariote aliye muuza (msaliti) Yesu Kwa vipande vya fedha alipotulia aligundua ameharibu na mambo hayarekebishiki tena na fedha aliyopewa haikua na maana tena.
Aliamua kujinyonga.
 
Nimemsikia akiSISITIZA kwamba hata MIKIA FC aka makolo wako behind the scene. Huu nao ni ushahidi wa wazi. Siamini kama taifa lina watu wawajinga kiasi hiki
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Mkataba unajieleza umeuona wote na vifungu vyake? Nyie ndio mbumbumbu wanaosemwa na Sudy unabeba kakipengele kamoja ndio unaruka nako ujui mkataba ni mjumuiko wa vipengele vingi
 
Hakuna mahali popote kwenye mkataba wa Feisal panapotamka suala la kukaa mezani kuzungumza kwanza ikiwa Feisal atataka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama za mkataba wake.

TFF ni wajinga na wapuuzi.
Leta huo mkataba tuone ukoje acha kudandia treni kwa mbele
 
Wewe ni Mbumbunbu OG, Al Nassr ndio wameterminate mkataba na kumrelease Vincent ili wapate nafasi ya kumuaccomodate Ronaldo tena baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
 
Hakuna mahali popote kwenye mkataba wa Feisal panapotamka suala la kukaa mezani kuzungumza kwanza ikiwa Feisal atataka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama za mkataba wake.

TFF ni wajinga na wapuuzi.
Kwani Feisal kwenye mkataba wake aliokuwa nao kuna saini za pande zipi?

Tuanze hapo.
 
Hata hili ni la kuambiwa na TFF kweli ,kwani ktk kesi yake nani alimwambia atafute wakili wa kumtetea?

Halazimishi kucheza Yanga,bali mkataba unamfunga aliosaini ndio unambana kucheza Yanga.
 
Ingekuwa na suala la kutaka au kutotaka mikataba isingelikuwa na maana kusaini.
 
Wabobezi wa Sheria,ninaomba Mwongozo,
-Mimi ni mtumishi wa taasisi moja ya umma, kwenye mkataba wangu,kuna kipengere kinachosema,nikitaka kusitisha mkataba,nitoe notisi ya miezi 2 au nilipe mshahara wa mwezi moja, kusitisha mkataba mara moja.
-Nimepata kazi kwenye taasisi ya kimataifa, mshahara wangu ni mara nne ya mshahara wangu wa sasa na ninatakiwa kuripoti mara moja.
-Ninaomba Mwongozo Kama kuna ulazima wa kukaa meza moja na mwajiri wangu wa sasa tujadiliane suala la kuacha kazi kwenye hiyo taasisi ya umma.
- Kama nitatimiza takwa la (kwenye mkataba) kulipa mshahara wa mwezi mmoja na kutoa taarifa ya kusitisha mkataba nikiambatanisha na vielelezo vinavyotakiwa nitakuwa sahihi?
-Watumishi wengi wanapopata malisho ya kijani ( Green Pasture) huwa wanawasilisha barua za kujiuzuru.
-Huwa inakera kwa mwajiri,(hasa kama mtumishi alikuwa tegemeo katika taasisi).
-Lakini ni haki ya mtumishi kutafuta malisho ya kijani.
-waajiri wengi wanajua kuwa wanawanyonya watumishi wazawa na wanawalipwa vizuri watumishi wa kigeni.
-Ushauri :waajiri wawalipe vizuri watumishi au wachezaji wazawa kulingana na ubora wao au waruhusiwe kutafuta changamoto na fursa Sehemu nyingine.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wameshindwa kuweka vifungu TFF sembuse mtoa uzi
 
Hakuna majadiliano..unachotakiwa kupeleka ni uthibitisho tu kwamba umelipa mishahara/mshahara wao.
 
Amua wewe basi. Maana kubweka bweka tu humu jukwaani, hakubadilishi chochote.
 
Dunia gani ambayo ukiamka asubuhi unasema nimevunja mkataba siendi kazini? Wanasheria waliofaulu nchi hii wako 26 tu wewe ni miongoni mwa Mbumbumbu 612.
 
Nilikuwa sijaona NB yako. Kumbe wewe ni Mbumbumbu wa kiwango cha juu? Aliyekwambia Vincent Abubakar kavunja mkataba Kwa kutakiwa na Man Utd ni Nani? Huyo Vincent keshasajiliwa na Man U? Tukwambie tu hujui, ni kwamba Idadi ya Wachezaji Kwa sheria za nchi ilizidi na Kwa vile kibiashara Al Nasry wanamuhitaji Ron zaidi kuliko Vincent wakamwita mezani wakafikia makubaliano ya pande mbili wakamwacha.
Mfano wako Kwa Kambole ndo wa ovyo zaidi. Yanga wangetaka kumwacha Kambole kijinga wangefanya unavyosema wewe, lakini ni dhahiri wangekumbana na rungu la FIFA. Walimwita wakakubaliana akaenda alikokwenda. Huwezi kuamka tu kwako ukasema nimevunja mkataba utadhani unacheza soka la ridhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…