Serikali imehimizwa kumsimamia mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani ili kuhakikisha anamaliza kwa wakati. Katika mradi huo hatua ya kwanza (lot one) ya ujenzi wa barabara ya Afrika Mashariki, kipande cha kilomita 34 kilichosalia cha Tanga-Pangani, ambacho kwa mujibu wa mkataba kinapaswa kukamilika ifikapo Juni 16, mwaka huu.
Aidha, imeelezwa kuwa mkandarasi atakaposhindwa kumaliza mradi huo kwa wakati, atalazimika kuilipa Serikali fidia ya asilimia 0.01 kwa kila siku ya ucheleweshaji hadi mradi utakapo kamilika.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, Machi 14, 2025, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokagua mradi huu.
Waje wakague na barabara ya mwendo kasi Mbagala ambayo haijaanza kufanya kazi hadi leo na miundombinu ya barabara hiyo tayali imeanza kubomolewa. Mfano mzuri ni kituo cha Police Ufundi ambapo barrier zote zimeng'olewa