Kamati ya Maadili TFF yampiga Haji Manara marufuku kujihusisha na Mpira. Apigwa faini Milioni 9

Mkuu! Kipindikile Dola ya Kimarekani dhidi ya Shilingi ya Kitanzania ilikuwa haijapanda....

Unachokiona hivi sasa ni matokea ya kupanda kwa dola.Ndio maana Muro alitozwa Mil 3 na Manara Mil 9.
..
 
Msemaji wa Klabu Kongwe ya Simba ndugu Haji Manara amehukumiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa milioni 9.
Adhabu hiyo imetolewa na TFF kutokana na matamshi ya msemaji huyo ambayo kwa mujibu wa TFF yanaenda kinyume na kanuni na taratibu za TFF.
 
Kuhusu swala la Manara huu ni upuuzi maana TFF wakiambiwa ukweli wanatoa adhabu za kipuuzi kabisa zisizo endana na kosa kama kumkomoa mtu, kwa utaratibu wa kichovu kama huu hatuwezi kufika mbali kisoka na kwa mfumo ilionao TFF kwa sasa sina uhakika kama watawatunza wale vijana wetu ili waendelee kucheza soka zuri kama wanavyofanya sasa.
 
Hahahaha huyu jamaa alifurahi sana muro alipofungiwa ...
 
Hivi hii tifuatifua inaongozwa na MAZOMBI au watu? Faini milioni 9 wamezikokotoaje? TFF is led by a bunch of twits!
 
Hiyo adhabu ni sawa.
Manara amekutwa na makosa 3 . Jerry muro alikuwa na 1. 3×3,000000= 9M.
Haji kaleta issue za kizamani za ukabila ili hali nafasi za TFF ni za kuchaguliwa kama Wabunge.

Hiyo hela ikilipwa napendekeza isaidie kupunguza lile deni pale TRA.
 
Lakini pengine kuna kaukweli
1. Kiongozi mkuu wa TFF ni kutoka Kagera inakotoka timu iliyomchezesha mchezaji kinyume cha taratibu
2. Mtendaji mkuu wa TFF ambaye kwa kawaida hupendekezwa na Rais wa TFF naye anatoka Kagera
3. Rais wa TFF ndiye pia Mwenyekiti wa TFF mkoa wa Kagera inakotoka Kagera Sugar
4. Watendaji wakuu wa TFF ambao ni RAIS na KATIBU mkuu wote ni ma ex katibu wakuu wa Yanga yenye maslahi ya pekee katika maamuzi yaliyofanywa
5. Kwa kuzingatia hoja za Manara na 1-4 hapo juu, haitoshi tu kufanya maamuzi ya pupa na kujipumbaza ati manara ametamka maneno ya kibaguzi. Bahati mbaya siku hizi BMT haina meno lakini vinginevyo rufaa ya kagera sugar ilitakiwa ipelekwe huko na si kwa wateule wa Rais wa TFF mwenye maslahi ya moja kwa moja na suala hili.
 
utakua hufatilii mipira ya nje, kocha anapigwa fine tu kwa kusema tu kuwa hana iman na refa itakua hayo maneno ya manara? tuache ushabiki bhana
 
simba mmezoea kulalama,shindenm na c kuililia point za mezani
 
Siamini kama Simba ilimtuma Manara kuzungumza vile. Maneno yale yanamvunjia heshima yeye mwenyewe Manara Simba na familia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…