Kamati ya Maadili ya Bunge leo inaendelea kumuhoji Askofu Gwajima

Kweli ni hiyari Komredi......

Na wengi tu wanaitetea hiyari yao hiyo.....

Ila.......

Mh.Gwajima alianza kwa KUWALAANI VIFO MADAKTARI wetu wote ambao wanahimiza chanjo dhidi ya UVIKO huku akisema kuwa VIONGOZI WAMEHONGWA MAPESA YA NJE kuhimiza chanjo na akataja kuwa KIPINDI CHA URAIS WA HAYATI JPM hayakuwepo hayo.....je hapa hajamshambulia Rais na mwenyekiti wetu wa chama ?!!

Hili kwako ni dogo Komredi wangu ?!!!

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#SiempreJMT
 
Bado fikra za mwenyekiti zinalindwa mpaka leo hata kama ni useless? Mbona yeye mwenyewe anataka kukosolewa, kwanini wewe umsemee
 
Bado fikra za mwenyekiti zinalindwa mpaka leo hata kama ni useless? Mbona yeye mwenyewe anataka kukosolewa, kwanini wewe umsemee
Mwenyekiti anaweza kukosolewa kwa STAHA na mwanachama wa CCM....si kwa ZODO ,DHIHAKA NA MASHAMBULIZI.....

Hayo utayapata kwenye madarasa ya itikadi ya chama.....

IMANI YA PILI YA CHAMA>

*Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
 
Sioni sehemu yoyote aliyomshambulia mwenyekiti wa chama na Rais.

Ndio maana chama hakijawahi kumuita kumhoji.
 
Hizi itikadi za Kirusi au china ya kale ngumu kuendana na karne ya sasa ya kizazi huru
 
Bwana Yesu apewe sifa!

Kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge leo itaendelea kumhoji askofu Gwajima kwa tuhuma za kusema uwongo na kulivunjia bunge heshima.

Je, Askofu Gwajima atakwenda na kiti chake au atasimama?

Mungu ni mwema wakati wote.
Huyo ni tapeli tu,awadanganye MISUKULE yake,
Eti anakataa kiti na maiki anaomba abadilishiwe vingine na anayembadilishia na kumpa vingine Ni yuleyule aliyemwandalia awali,hiyo ni akili au matope?

Kama angekuwa na akili angeenda na kiti chake na maiki yake,
Hali nyama ya nguluwe sababu ni haramu lakini anaomba apewe mchuzi wa nguluwe eti ni halali!
 
Kwani ni uwongo kuwa Rais hajasaini pesa ili chanjo ziletwe?
Rais amesaini pesa za mkopo akaambiwa na masharti ya kufuata Kama vile kutoa takwimu ndipo tukaletewa chanjo, so Gwajima Yuko sahihi maana asingesaini na kukubali masharti tusingeletewa chanjo Kama ambavyo JPM alikataa hayo masharti ya hizo pesa za chanjo.
 
Huwezi kumjaribu Mungu,Yesu mnazareti alikataa mchezo huo alipoambiwa ajirushe kutoka juu eti malaika wangemlinda.
 
Wewe unayeanini unaweza kunywa sumu? Tafsiri yako ya uelewa wa biblia sio uniform kwa kila mkristo hivyo hupaswi kumlaumu mkristo mwingine anavyotafsiri tofauti na wewe.
 
Huko ni "kununuliwa" kwa mtu binafsi ambako Gwajima anakutuhumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…