Bunge la Ulaya hivi punde limejadili hali ya kisiasa nchini Tanzania kabla na baada ya uchaguzi, na kuzishauri nchi washirika kupunguza zaidi misaada inayotolewa kwa Tanzania.
Wachangiaji wengi wamependekeza kusitishwa au kupunguzwa kwa misaada inayotolewa na nchi washirika wa EU. Wanahoji nini maana ya misaada yao kama lengo lao la utawala bora halitekelezwi na watawala.
Msaada wa kibajeti uliokuwa unatolewa na EU umesitishwa hadi mwafaka wa kisiasa ufikiwe.
“No budget support until EU Commission sees a fundamental improvement in the political dialogue!” - H. Stausboll.
“We must consider ECONOMIC SANCTIONS TO TANZANIA because of the elections and the TERRORIST ATTACKS in the South of Tanzania and North of Mozambique” -PauloRangel_pt EPP.
“We have had a very difficult relationship with the government of Tanzania. We will reconsider Budget support unless we see a clear direction in the political environment “ - @HStausboll.
“The elections in Tanzania was a travesty of Justice. It was Lukashenko style type of an election. Can we still trust The Tanzania govt with aid?” - Gahler Michael, @Europarl_EN.
Wameshauri kuliko kuipatia serikali ambayo inaweza kuitumia vibaya kufifisha haki za binadamu ni bora kuvipatia moja kwa moja vikundi vinavyojihusisha na kutetea haki za binadamu.
Wamehoji EU kuipatia serikali ya Tanzania Euro 27m kwa ajili ya Korona ambayo serikali inasema Tanzania haina Korona.
Mkataba wetu na EU.