acha tuwe na huo ukurutu tu bora mara 2000. mnaleta mambo ya ujima apa? mmemwaga mboga upinzani mwageni ugali wote kabisa...kama mbwai iwe mbwai tu.Wizi ulikuwepo au la kushabikia vikwazo kwenye nchi yako ni ukurutu wa mawazo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
acha tuwe na huo ukurutu tu bora mara 2000. mnaleta mambo ya ujima apa? mmemwaga mboga upinzani mwageni ugali wote kabisa...kama mbwai iwe mbwai tu.Wizi ulikuwepo au la kushabikia vikwazo kwenye nchi yako ni ukurutu wa mawazo.
Mbarikiwe sana ndugu zetu wapendwa Wazungu. Mwaaaa!Amani iwe nanyi tena wadau!!
Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.
Napenda tu kusema yafuatayo
1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania
2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania
3. Wamehoji hadi kwanini walitoa hela za ku support harakati za Covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free
4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwanini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?
5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.
Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂
Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.
... lakini ndio hivyo mtafika 2025 kwa dabo hazard ... kama mbwai na iwe mbwai tu mlitegemea mterezo dadeki na bado ...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha wanafikiri hili litawatoa kimasomaso,
Hili gari limeshaondoka hadi 2025.
Wanajijua wemyewe mchezo waliokuwa wanataka kuufanya , sheria kali zingefuatwa sasa hivi wangekuwa wameshapata kisingizio cha kuleta vurugu. Mbona hakuna hata mtu mmoja aliyeandamana kudai haki yake.Ni mpinzani yupi alikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na kura fake?(Niwekee source/link)Hao watuhumiwa walipandishwa mahakamani lini?Ni sheria ipi inasema kuwa akikamatwa mtu kwa kosa la jinai ambalo ni very serious kama vile kupeleka kura fake vituoni anaweza kuachiwa na Polisi kwa ubinadamu hata kabla hajafikishwa mahakamani?Unafanya mzahaa na mimi?
Wakatishe tuu huo ushirikiano wao, tuashikana na marafiki zetu wa kihistoria walewale tumefungia bank yao. Na vile wanawaogopa sasa😁😁😁😁Bomba sana, sasa bado watakwambia tungeendelea kuwa chini ya mkoloni eti tupate maendeleo?! Aise tuna vichwa vya ajabu Tz?!
Msiseme mliishinda korona ilihali imeua watu muhimu kuliko hata majirani zetu wa EAC. Anayetufuatia kwa mbali ni Burundi!Sasa wanahoji nini?!
Sasa kumbe ni hivyo tu, walale mbele hatutaki misaada yao. Huu ni wakati wa kupiga kazi.Bunge la Ulaya hivi punde limejadili hali ya kisiasa nchini Tanzania kabla na baada ya uchaguzi, na kuzishauri nchi washirika kupunguza zaidi misaada inayotolewa kwa Tanzania.
Wachangiaji wengi wamependekeza kusitishwa au kupunguzwa kwa misaada inayotolewa na nchi washirika wa EU. Wanahoji nini maana ya misaada yao kama lengo lao la utawala bora halitekelezwi na watawala.
Msaada wa kibajeti uliokuwa unatolewa na EU umesitishwa hadi mwafaka wa kisiasa ufikiwe.
“No budget support until EU Commission sees a fundamental improvement in the political dialogue!” - H. Stausboll.
“We must consider ECONOMIC SANCTIONS TO TANZANIA because of the elections and the TERRORIST ATTACKS in the South of Tanzania and North of Mozambique” -PauloRangel_pt EPP.
“We have had a very difficult relationship with the government of Tanzania. We will reconsider Budget support unless we see a clear direction in the political environment “ - @HStausboll.
“The elections in Tanzania was a travesty of Justice. It was Lukashenko style type of an election. Can we still trust The Tanzania govt with aid?” - Gahler Michael, @Europarl_EN.
Wameshauri kuliko kuipatia serikali ambayo inaweza kuitumia vibaya kufifisha haki za binadamu ni bora kuvipatia moja kwa moja vikundi vinavyojihusisha na kutetea haki za binadamu.
Wamehoji EU kuipatia serikali ya Tanzania Euro 27m kwa ajili ya Korona ambayo serikali inasema Tanzania haina Korona.
Mkataba wetu na EU.
View attachment 1629980
Ndivyo mkataba unavyosema?Ni hivi, rudisheni pesa za wanaume.
Hoja za yule mjumbe wa sijui bunge la EU [emoji1099] kwa kweli nzito.... 1.anataka kujua fedha zimetolewa kwa kigezo gani ikiwa dunia ilijulishwa kwamba sisi ni Corona free, tulikataa kutoa takwimu za Corona, na tulikataa kutumia WHO Corona guidelines... Yaani mzungu Kakomaaa huyooo....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha wanafikiri hili litawatoa kimasomaso,
Hili gari limeshaondoka hadi 2025.
bujibuji hao wazungu hatuhitaji misaada yao, wakae nayo huko huko kwaojohnthebaptist mfikishie babu yako salamu, kwamba jahazi limetoboka, atafute mbeleko ya kubebea kwaya yake ya kusifu na kuabudu.
Mkuu hili siyo jukwaa la dini na hamna sehemu nimehusisha dini Mimi labda Kama kiswahili kwako ndo tatizo.Taifa teule? Unajua maana ya Taifa teule?
Tatizo mnachanganya mambo ya kiimani na mambo ya utendaji.
Labda huenda kuna pesa tunategemea kujenga barabara 80 km kwa msaada wa mabeberu.
Inabidi kwanza tuache ulafi wa hela zao ndio wataacha kutufuatilia, kwani situliambiwa na kiongozi wako sisi ni dona kantrii..??Bila kupoteza Muda naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja,
Leo nilitenga muda wa kusikiliza kile kilichokuwa kinajadaliwa na Hawa Viumbe wa "EU" (External affairs), Kama tulivyo taarifiwa juzi katika vyombo vya habari vya kwao huko na baadhi ya nyuzi hapa JF.
Ila Nimesikitika Sana kuwa nilichotarajia kukisia kutoka kwao na nilichosikia ni Kama "Vatican na Saud Arabia" (quit different).
In summary; Hiki ndo nilitarajia kukisikia kutoka kwa hawa Nguri wa Hoja duniani;.
1.Uchaguzi wa 28Oct202.
Nilitajia kusikia maswali kama; Kwanini CCM imeishinda kwa asilimia kubwa vile kuliko vyama vingine?
Je baada ya Matokeo Wananchi waliopiga Kura hizo wameridhika na Matokeo Yao au hapana na Kama Ni hapana, Kuna ishara yeyote waliyoionyesha kutokubaliana na walichokichagua( Hapa Wapigiwa kura hawahusiki).
Je baada ya Matokeo wagombea nafasi wa upinzani walioshindwa waliyachukulia je matokeo, Kama Ni ndio sawa na Kama Ni hapana, je Kuna njia zozote za kisheria walizochukua kupinga Matokeo hayo ili kupata haki Yao(ukiondoa ya Matokeo ya urais).
2. Ukandamizwaji wa haki za binadam na Ugaidi;
Nilitarajia kusikia hoja Kama hizi kutoka kwao;
Kwanini msumbuji imeshindwa kuwathibiti Wana mgambo walioweka makazi kwenye nchi yao mpaka Wanasababisha maafa na kukandamizwa kwa haki za binadam nchi jirani Kama Tanzania(Mtwara Kama walivyotaja wao)?. Na Wala siyo kuilaumu Tanzania kisa inapakana na sehemu ambayo magaidi wapo. Nikweli EU hawajui kuwa Msumbuji ni nchi huru na ina mipaka na jeshi lake ambalo haliwezi ingiliwa na jeshi lolote lile pasipo ruhusa?.
3. COVID19.
Nilitegemea kusikia ni, njia gani ilizotumia Tanzania kuondokana na janga la Corona mpaka kufikia hatua ya watu wake kuendelea na maisha yao Kama kawaida bila vifo Wala athari yeyote?
Na wala siyo kulialia kwanini Tanzania haina Corona na tunaipatia pesa, Mara pesa za Corona zimetumikatumika je, Mara Sijui Nini ,
Hapa kwakweli imeonesha wazi kabisa jinsi gani mataifa ya ulaya yalivyo na wivu mkubwa juu ya Tanzania hasa katika suala hili la Covid19.
My take; Tanzania ni nchi yangu na Nina ipenda Sana na Sina shaka na Kiongozi wangu mkuu Yani "JIWE" juu ya kudili na Mabeberu naamini nachokiwaza mimi kuanzia Sasa na kuendelea ndo anachokiwaza Rais wangu. Hizi hoja za Leo niza kupuuza na kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea maana inaonekana watu wenyewe wamejadili huku mioyo yao ikiwa imejaa chuki binafsi na wivu juu ya Tanzania pamoja na kulialia pasipo kuwa na "deep Intelligences".
Na nilichokugundua Tangu tupate Rais jiwe kwelikweli Tanzania imekuwa femous sana ndani na nje ya Mataifa ya Ulaya. Na wanavyotenga muda wao kutujadili namna hiyo kwetu ni faida kubwa Sanaa maana Kupitia wao ndo wana tangaza na soko letu la utalii na kuwafanya watu wengi zaidi kuja Tanzania kujionea uteule wake.
Mfano; Suala la kututangaza juzi Kati kwenye media zao kuwa "Tanzania ndo nchi pekee dunian ambayo haina maambuzi ya Corona kwa takribani wiki46" na leo walivyosema kwenye mkutano wao kuwa, "tunawapa je Msaada Tanzania angali hawana Corona". Hii itaongeza idadi ya watu wengi Sana wa ulaya waliochoka na lockdown kuja kula maisha kwenye Peace land ya Tanzania huku soko letu la utalii likipanda siku Hadi siku.
#Mungu Mlinde Jiwe, Mungu tulinde Watz wote, Mungu ilinde nchi yangu.
#I love my country [emoji1241].
Hiyo ni mikwara mbuzi tu bwashee!
Utawala unafitinika automatically!Alipewa tafiti za kweli toka kitengo kuwa hata nusu ya asilimia 58 alizopata 2015 hazifiki hivyo kama ana Nia ya kukalia kiti afanye mapema, amri ikatolewa Kwa Mahera ushindi usipungue asilimia 80 shauri ya papara wakasahau takwa la kikatiba kuhusu upinzani. Matokeo- Aibu ya mwaka.
Kuishinda haimaanishi kwamba hakuna walioathirika.Msiseme mliishinda korona ilihali imeua watu muhimu kuliko hata majirani zetu wa EAC. Anayetufuatia kwa mbali ni Burundi!
Serekali ya Magufuli ilipochukua hizo hela za EU walitii masharti pamoja na vigezo vya european union pamoja na WHO vya kuchukua na kutumia hizo hela kama vile kutoa ripoti kwa umma kila siku ya idadi ya watu waliopimwa,idadi ya watu waliokutwa na corona na idadi ya watu ambao hawakukutwa na corona kama vile rais wa EU alivyobainisha vigezo hivyo leo?Wazungu wanapaswa kuelewa kuwa Tanzania tulipambana na Corona na tukaishinda hivyo msaada tuliopewa na EU ulikuwa ni halali yetu.
Nani asiyejua hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali kupambana na Corona ikiwemo social distancing, kuvaa barakoa, kuweka sehemu za jamii kunawa mikono, kufanyia kazi nyumbani, shule na vyuo kufungwa nk nk.
Wazungu watafute sababu nyingine za kutubania misaada lakini hili la Covid 19 wanatuonea bure.
Maendeleo hayana vyama!
Na pia tulipata kwa vigezo vipi??Wanschotaka kujua ni hayo matumizi yake.... Mdije mkawa mmezipeleka kwenye SGR.
Sema wewe ndio una hali mbaya sababu hufanyi kazi wala hutafuti lkn wanaotafuta wanatanua mjiniAmani iwe nanyi tena wadau!!
Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.
Napenda tu kusema yafuatayo
1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania
2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania
3. Wamehoji hadi kwanini walitoa hela za ku support harakati za Covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free
4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwanini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?
5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.
Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂
Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.
[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23]Ile ya kupimia mapapai?