Kamati ya mashindano ya kombe la Mapinduzi inahujumu mashindano na kuyafanya yawe kituko mbele ya mataifa mengine yaliyo serious na kukuza soka

Kamati ya mashindano ya kombe la Mapinduzi inahujumu mashindano na kuyafanya yawe kituko mbele ya mataifa mengine yaliyo serious na kukuza soka

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Kamati ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi ilikuwa na nafasi kubwa ya kufanya haya mashindano yawe na heshima na hadhi ya juu kimataifa, lakini figisu na kukesa weledi kunafanya mashindano yaonekane kituko hasa kwa timu wageni tunaowaalika.

Ushauri wangu kwa kamati ya mashindano haya, isiundwe na Watanzania peke yake (Tanganyika na Zanzibar) bali kamati iundwe na wataalamu wa soka kutoka kwenye nchi zote zitakazoshiriki mashindano.

Pia waamuzi watoke kwenye mataifa shiriki ili mashindano yawe na ladha zaidi na kubeba sura ya kimataifa zaidi.

Hii ni fursa, mashindano yakiboreshwa, timu zitaleta mashabiki wao. Mashabiki watakula, watalala na kutalii kwa gharama zao na kutunisha sehemu ya pato la taifa hususan upande wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Wito wangu:-
Fanyeni muwezavyo muwaombe radhi APR na muwaeleze ni kwa jinsi gani mtaboresha mashindano yajayo.

Ondoeni siasa kwenye mpira, eti lazima timu ya Zanzibar icheze fainali hata kwa kubebwa, hii ni aibu kubwa sana kwa soka la Zanzibar.
 
Hakuna wa kukuskiliz bongo hii, hawahtaj ushaur wa mtu ila maamuz yao binafs kikubw iwe furaha kwao wabeba vitambi wa mbogamboga
 
Maneno yote haya kisa Simba kashinda. Tupunguze unafiki.
 
1704967316220.jpg
 
Vipi na Kamati ya tff waliosimamia ngao ya jamii ?
Instructions ndiyo mtihani wenyewe. Ukishafeli kuyaelewa maelekezo na kila kitu umekosa.

Mtu anazungumzia Mapinduzi wewe unaleta za tff. Yeye akusaidieni nini!

Kwanini usianzishe thread yako ukawahoji hao Tff.

Nb: Unakuwa na akili za kijinga kama shabiki wa Yanga ambao kila ukiongea nao ilikuwaje wakatolewa mapinduzi cup jibu lao tuliwafunga simba 5 sasa unashangaa kuna uhusiano gani
 
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi mapinduzi cup akiwa anahojiwa na vyombo vya habari anasema, Baada ya mechi ya Simba vs Singida kumalizika Kamati walijaribu kupitia marejeo ya tukio la Kona ya utata iliyo zaa goli na walibaini haikustahili kuwa Kona.
Kilichotokea ni makosa ya kibinadamu.
 
Mashabiki wa Tanzania ni kama waumini wa TB Joshua na Mwamposa.

Mpo kama majongoo!
 
Back
Top Bottom